Mikael P Aweda aanza kuivuruga CHADEMA

Navyojua mimi amehama jimbo la ubungo sasa anaishi ukonga'kwanini asigombee acha siasa za kizandiki'siku hizi mtu anakaa ukonga mwacheni agombee huko lakini jimbo la ubungo ataacha kuwa mwenyekiti'

Maelezo ya majanikv ndiyo yalipelekea mimi kuuliza haya maswali;

1.Unaweza kuthibitisha kwamba anaishi ukonga? anakaa kata gani ama mtaa gani??
2.Kwanini asijiuzulu kwanza nafasi yake ubungo ndipo aende kugombea ukonga? kwanini agombee ukonga wakati bado ni mwenyekiti wa ubungo?
3.Nani anayefanya siasa za kizandiki kama si yeye na wewe?

Baadaye ndipo ukaja na maelezo yako haya yaliyojitosheleza.

Mimi ni niligombea uenyekiti wa Chadema na kuwa mkiti wa kwanza wa kikatiba Ubungo nikiwa mkazi wa Ubungo- Ubungo kisiwani. Ni namwanachama ninayetumia muda na pesa zangu nyingi kuijenga Chadema kwa uwezo wangu wote.
Nilipoingia Ubungo haikuwa na uongozi wa kikatiba katika baadhi ya maeneo,(walikuwepo wa kukaimu) nikasimamia chaguzi zote kutoka kata ya Manzese hadi Kibamba(Nimetumia muda na pesa) Shahidi wa yote haya Mbunge mwenyewe (Mnyika). Nilifanya naye kazi kwa karibu sana.
Kabla sijaja ubungo, ubungo kulikuwa na vurugu nyingi sana. Nilipochaguliwa kuwa Mkiti na baada ya waleta vurugu kutimuliwa na makao makuu. Ubungo tumekuwa moja hadi tukashinda chaguzi zote hizo za madiwani na ubunge chini ya Uongozi wangu.

MCHAKATO WA KUNG'ATUKA.
Kabla sijaondoka niliwashirikisha wazee ubungo na secretariet ya jimbo chini ya Katibu. Hakukuwa na tatizo.
Baadaye nikakaa na viongozi wa kata zote. Wote wakanielewa.

Kuhusu kujiuzulu ubungo.
Mimi nimejiuzulu uenyekiti wa Ubungo 1/7/2011. Nakala nimempa katibu wa Chadema mkoa wa kinondoni na Katibu mkuu Taifa. Barua nilimwandikia katibu wa Jimbo la Ubungo.

Kwanini nimjizulu?
A) Nimehama kimakazi kutoka Ubungo, mtaa wa Kisiwani manisipaa ya Kinondoni hadi hadi Manisipaa ya Ilala. Makazi yangu ya kudumu yatakuwa Kitunda. Sidhani kama ni busara nichome mafuta kutoka Ilala kutoka kwenda ubungo. It is a waste of Time and Money unnecessarily.
On the other hand, katiba ya Chadema inaniruhusu mimi kupima mwenyewe baada ya kuhama kimakazi-haisemi lazima nijiuzulu au lazima nibaki. Kwa hiyo, mimi nikaongea na wazee wa Jimbo la ubungo, na viongozi wengine akiwepo Mbunge Mnyika wakanielewa. Tatizo liko wapi?

B) Ubungo ni Imara kimtandao na kiungozi. Jimbo la ubungo lina Mbunge Mnyika na Madiwani wa kutosha (7) bila kutaja wabunge wawili ambao nao ni madiwani. Kamati ya utendaji Ubungo ina wajumbe kama Dr Kitila, Mbunge na Suzana Lymo. Si Busara kuacha jimbo la Ukonga ambako ndiko ninakotumia muda wangu mwingi na kuendelea kuja ubungo imara. Nimezunguka kata zote, za ukonga na nimegundua inahitajika uimarishaji. Baadhi ya viongozi waliopo ( wakiwepo viongozi wa jimbo) wanakaimu nafasi zao.

C) Ubungo ina ruzuku ya zaidi ya Sh mil moja kwa Mwezi ( Ruzuku ya Chama na mchango wa Mbunge). Ukonga wana ruzuku ndogo sana around laki mbili na kidogo. Kwa hiyo, Uongozi uliopo Ubungo unaweza kujenga chama wakishirikiana na madiwani na Mbunge bila mimi. Busara yangu ni kwamba nikatumie uzoefu wangu wa kuongoza ubungo muda mrefu bila ruzuku (before uchaguzi mkuu) na kufanikiwa kushinda ktk jimbo (ukonga) ambalo sasa lina matatizo ya fedha kama tuliyokuwa nayo sisi kabla ya uchaguzi mkuu.

Mwisho; Chanzo cha Fitina.
Baada ya Makao makuu kutangaza kuwa Jimbo la Ukonga lazima lifanye chaguzi zote upya, viongozi wengi wa kata tano kati ya nane ambazo viogozi wake wananifahamu kutokana na kuwepo kwangu ukonga muda mwingi kikazi na kimakazi waliniomba nigombee nafasi ya M/kiti. Nikawakubalia. Mkiti aliyepo anauwezo wa kugombea au kutogombea ni haki yake ya kikatiba.

ALUTA CONITINUA.

Na baada ya maelezo haya nikakujibu hapa na kukushukuru kwa ufafanuzi wako;

Ahsante kwa ufafanuzi wa kina,

Ieleweke kwamba hakuna fitna wala chuki, isipokuwa ulishindwa kuwa muwazi tangu mwanzo.

Nilikuandikia kutaka kufahamu ukweli wa jambo hili lakini hukutaka kunijibu nikaona nije public ili nifahamu ukweli.

Kwakuwa kulishaanza kuibuka taarifa mbalimbali zinazokuhusisha wewe kuleta malumbano miongoni mwa viongozi waliokuwepo sasahivi, basi ilikuwa ni muhimu kuliweka hili sawia ili kama wanachama wakiridhia kukukabidhi dhamana ya uongozi wa jimbo basi upate ushirikiano wa kutosha toka kwa viongozi wa zamani pamoja na wanachama wote kwa ujumla.

Tuko pamoja.

Sasa unataka niseme nini tena??

Sasa we Nyepesi nyepesi hutaki kuamini kwamba mimi nimeondoka Kinondoni na sasa ninaishi manisipaa ya Ilala? Nipigie nikupeleke ktk makazi yangu ya kudumu.
Pili, kama nilivyojiuzulu ubungo kwa hiari, kugombea Ukonga pia ni Hiari in regard to geografical location. Si lazima nikae ktk kata mojawapo. Ninaweza nikakaa jimbo lolote ktk manisipaa ya Ilala nikagombea ukonga. Hata kwa mujibu wa sheria ya serikali za mtaa, Mtu anaweza akakaa kariakoo akagombea udiwani Chanika. Ruksa. Kwa hiyo, tafuta makazi yangu manisipaa ya Ilala na siyo lazima ndani ya ukonga. Hata hivyo, makazi yangu ya kudumu ni mtaa wa Magole kata ya kitunda jimbo la ukonga.

Tatu, Katiba ya Chadema imetupa uhuru huo wa mahali anapokaa kiongozi kama ilivyo kwa sheria za serikali ktk nafasi kama ya ubunge.

Unaweza kuwa unaishi manispaa ya ilala eneo la tabata ambalo ni karibu na ubungo kwahiyo hoja yako ya umbali9 ikawa haina mashiko.

Btw, hoja ya msingi nadhani imejibiwa ingawa kuna maswali machache hujayagusia na sina sababu ya kuyafuatilia, unakaribishwa ukonga ili kusaidia kuongeza ruzuku.
 
Asante kwa kunielewa. Sina taarifa ya kuleta mtafaruku wowote Ukonga. Ila ninafahamu kuna viongozi wa jimbo wanaoniunga mkona na wasioniunga mkono. Huo si mtafaruku. Hiyo ndiyo demokrasia.

Mtafaruku umetokana na wewe kusemekana kushirikiana na kiongozi mmoja wa jimbo na kum-bypass mwenyekiti.

Demokrasia izingatie uwazi, haki na wajibu.

Umesomeka.
 
Mtafaruku umetokana na wewe kusemekana kushirikiana na kiongozi mmoja wa jimbo na kum-bypass mwenyekiti.

Demokrasia izingatie uwazi, haki na wajibu.

Umesomeka.

sasa unaonekana umeishiwa hoja na kinachofuatia ni upuuzi
 
Nilikusamehe kwa kosa la kwanza,nikadhani walau utakubali kiutu uzima kuwa ulikurupuka (yes you did!). Kumbe licha ya kuwa mkurupukaji,mzushi na mchonganishi,lakini pia una dalili za UHUNI!
Matatizo ya kuanza kunywa gongo ukiwa na umri mdogo matokeo yake huwezi hata kusoma na kuelewa kilichoandikwa, mwenyewe kakiri hapo sasa wewe unalipuka kama teja!!
 
Btw, hoja ya msingi nadhani imejibiwa ingawa kuna maswali machache hujayagusia na sina sababu ya kuyafuatilia, unakaribishwa ukonga ili kusaidia kuongeza ruzuku.
Kumbe mapovu yote destination na jicho lako lote ni kwenye ruzuku na si maendeleo ya wana ukonga.
 
sasa unaonekana umeishiwa hoja na kinachofuatia ni upuuzi

Nilikusamehe kwa kosa la kwanza,nikadhani walau utakubali kiutu uzima kuwa ulikurupuka (yes you did!). Kumbe licha ya kuwa mkurupukaji,mzushi na mchonganishi,lakini pia una dalili za UHUNI!

Nyie wote wawili akili zenu zinafanana na si ajabu ziko kwenye "exhaust pipe" ndo sababu mnaharisha tu hapa,....

Haya maneno kayasema mwenyewe, mnabisha hata msichokijua.

Asante kwa kunielewa. Sina taarifa ya kuleta mtafaruku wowote Ukonga. Ila ninafahamu kuna viongozi wa jimbo wanaoniunga mkona na wasioniunga mkono. Huo si mtafaruku. Hiyo ndiyo demokrasia.
 
Kumbe mapovu yote destination na jicho lako lote ni kwenye ruzuku na si maendeleo ya wana ukonga.

Ukisikia akili za kushikiwa ndo hizi, mimi nimemkaribisha kwa ajili ya kuongeza ruzuku ukonga kwakuwa yeye mwenyewe kasema kwamba ubungo kuna ruzuku ya kutosha lakini ukonga hakuna ya kutosha, na amekiri kwamba anatumia pesa zake na muda wake mwingi kwa ajili ya chadema, sasa kwanini nisimkaribishe ukonga??
 
Ina maana asingekuwa anatumia pesa yake usingemkaribisha.
 
Ina maana asingekuwa anatumia pesa yake usingemkaribisha.

Ningemkaribisha, kwakuwa amezitanguliza basi sina sababu ya kuzikataa.

Najua kutakuwa na vikao vingi vya kupanga mikakati ya maendeleo kwahiyon sitting allowance itakuwa haisumbui tena.
 
Nyie wote wawili akili zenu zinafanana na si ajabu ziko kwenye "exhaust pipe" ndo sababu mnaharisha tu hapa,....

Haya maneno kayasema mwenyewe, mnabisha hata msichokijua.

nilisema umeishiwa hoja na kinachofuatia ni upuuzi .... yaliyoandikwa yametimia

kunguru hawezi kuwa kuku hata siku moja ...... let you praise your own soul full of foolishness
 
nilisema umeishiwa hoja na kinachofuatia ni upuuzi .... yaliyoandikwa yametimia

kunguru hawezi kuwa kuku hata siku moja ...... let you praise your own soul full of foolishness

Assuming kwamba uko sahihi, una maana kwamba nimeishiwa hoja baada ya hoja yangu kujibiwa na mhusika.

Sasa wewe na huyo mpuuzi mwenzako hamkuwa na hoja na bado hamna hoja mnaendelea kuharisha tu kwenye hii thread.
 
mkuu ni vyema ukaonyesha hekima yako.

sawa mkuu, hekima yangu imeshaonekana tangu post ya mwanzo kwenye thread hii,
na wewe fanya hivyo kuficha upumbavu wako, cdm haijengwi na majungu, hadi sasa hakuna kanuni wala taratibu zilizovunjwa, omba radhi wanachama wa cdm na aweda mwenyewe kisha funga thread usiendeleze uchochezi.
 
Assuming kwamba uko sahihi, una maana kwamba nimeishiwa hoja baada ya hoja yangu kujibiwa na mhusika.

Sasa wewe na huyo mpuuzi mwenzako hamkuwa na hoja na bado hamna hoja mnaendelea kuharisha tu kwenye hii thread.

i have never ever argued with a paranoid

i wish you luck in your foolishness project

bye
 
Amekiuka utaratibu wa chama,

Anagombea uenyekiti ukonga wakati bado ni mwenyekiti ubungo.

Ni kweli mimi sina popularity yeyote ukonga lakini najaribu kuangalia kama utaratibu na kanuni za uchaguzi ndani ya chama zinazingatiwa.

umeshazisoma zinasemaje?
 
sawa mkuu, hekima yangu imeshaonekana tangu post ya mwanzo kwenye thread hii,
na wewe fanya hivyo kuficha upumbavu wako, cdm haijengwi na majungu, hadi sasa hakuna kanuni wala taratibu zilizovunjwa, omba radhi wanachama wa cdm na aweda mwenyewe kisha funga thread usiendeleze uchochezi.

Naona mzee wassira amekupa msemo, wacha niwe kama gazeti la mwananchi!!!
 
ISOMENI HII BARUA YA AWEDA MWENYEWE ACHENI UZUSHI
]Sababu za kung'atuka uenyekiti jimbo la ubungo.[/h]
Kuna watu wameandika thead ihusuyo kujiuzulu kwangu, ndani yake kuna ukweli lakini pia kuna upotoshaji wa baadhi ya mambo. Naomba nitoe maelezo sahihi.

Mimi nimekuwa mwenyekiti wa Chadema ubungo na mkiti wa kwanza wa kikatiba Ubungo nikiwa mkazi wa Ubungo- Ubungo kisiwani. Ni mwanachama ni nayetumia muda na pesa zangu nyingi kuijenga Chadema kwa uwezo wangu wote.

Nilipoingia Ubungo baadhi ya viogozi waliokuwepo walikuwa wanakaimu nafasi zao ktk baadhi ya ngzi, nikamilisha chaguzi zote kutoka kata ya Manzese hadi Kibamba. Shahidi wa Yote haya Mbunge mwenyewe. Nilifanya naye kazi kwa karibu sana.
Kabla sijaja ubungo, ubungo kulikuwa na vurugu nyingi sana. Nilipochaguliwa kuwa Mkiti na baada ya waleta vurugu kutimuliwa na makao makuu. Ubungo tumekuwa moja hadi tukashinda chaguzi zote hizo za madiwani na ubunge chini ya Uongozi wangu.

MCHAKATO WA KUNG'ATUKA.
Nimewashirikisha wazee wa ubungo na secretariet ya jimbo chini ya Katibu wa Jimbo la Ubungo.
Baadaye nikakaa na viongozi wa kata zote. Wote wamenielewa.

Kuhusu kujiuzulu ubungo.
Mimi nimejiuzulu uenyekiti wa Ubungo 1/7/2011. Nakala nimempa katibu wa Chadema mkoa wa kinondoni na Katibu mkuu Taifa. Barua nilimwandikia katibu wa Jimbo la Ubungo.

Kwanini nimjizulu?
A)Nimehama kimakazi kutoka Ubungo, mtaa wa Kisiwani manisipaa ya Kinondoni hadi Manisipaa ya Ilala. Makazi yangu ya kudumu yatakuwa Kitunda. Sidhani kama ni busara nichome mafuta kutoka Ilala kwenda ubungo. It is a waste of Time and Money unnecessarily.
On the other hand, katiba ya Chadema inaniruhusu mimi kupima mwenyewe baada ya kuhama kimakazi-haisemi lazima nijiuzulu au lazima nibaki. Kwa hiyo, mimi nikaongea na wazee wa Jimbo la ubungo, wakanielewa.

B)Ubungo ni Imara kimtandao na kiungozi. Jimbo la ubungo lina Mbunge Mnyika na Madiwani wa kutosha (7) bila kutaja wabunge wawili ambao nao ni madiwani. Kamati ya utendaji Ubungo ina wajumbe kama Dr Kitila, Mbunge na Suzana Lymo. Si Busara kuacha jimbo la Ukonga ambako ndiko ninakotumia muda wangu mwingi na kuendelea kuja ubungo ambayo ni imara. Nimezunguka kata zote, za ukonga na nimegundua inahitajika uimarishaji. Baadhi ya viongozi waliopo (wakiwepo viongozi wa jimbo) wanakaimu nafasi zao. Busara ni mimi kuongeza nguvu ktk jimbo kama hilo.

C) Ubungo ina ruzuku ya zaidi ya Sh mil moja kwa Mwezi ( Ruzuku ya Chama na mchango wa Mbunge). Ukonga wana ruzuku ndogo sana – around laki mbili na kidogo. Kwa hiyo, Uongozi uliopo unaweza kujenga chama Ubungo wakishirikiana na madiwani na Mbunge bila mimi. Busara yangu ni kwamba sasa niende nikatumie uzoefu wangu wa kuongoza ubungo muda mrefu bila ruzuku ( kabla ya uchaguzi 2010) na kufanikiwa kushinda ktk jimbo ambalo sasa lina matatizo ya fedha kama tuliyokuwa nayo sisi kabla ya mwaka jana. Kwangu mimi huu ndio uamuzi wa Busara. Sitakiwi kung'ang'ania ubungo tena imara.

D) Viongozi na wanachama wa ukonga wameniomba nigombee ukonga,
Viongozi wengi na wanachama wa ukonga, baada ya kuona utendaji wangu walioniomba nigombee nafasi mojawapo ktk uchaguzi unaokuja hivi karibuni. Nikawakubalia. Hiyo nayo ni sababu mojawapo.

Mwisho;
Ni matumaini yangu kwamba yale mazuri tuliyoyafanya pamoja mimi na viongozi wenzangu watayaendeleza wenzangu wanaobaki.

ALUTA CONITINUA.

MIKAEL P AWEDA
 
Back
Top Bottom