NyepesiNyepesi
Member
- Mar 8, 2011
- 47
- 9
Taarifa za uhakika kabisa toka chanzo cha kuaminika ndani ya uongozi wa chadema jimbo la ukonga zinasema kwamba Bw. Mikael P. Aweda ambaye kwa sasa ni mwenyekiti wa chadema jimbo la ubungo, amechukua fomu za kuwania nafasi ya uenyekiti jimbo la ukonga.
Kwa mujibu wa katiba ya chadema bw Aweda atashikilia nafasi hiyo ya mwenyekiti wa chadema jimbo la ubungo hadi mwaka 2014 hapo utakapofanyika tena uchaguzi mkuu ndani ya chama.
Katika hali ya kushangaza mwenyekiti huyu amechukua fomu za kuwania uenyekiti wa chadema jimbo la ukonga. Jimbo la ukonga linatarajia kufanya uchaguzi wake mnamo tarehe 31/07/2011 kufuatia kugawanywa na NEC(tume ya taifa ya uchaguzi) kwa jimbo hilo kulikofanyika mwaka jana na kuzaliwa kwa jimbo la segerea.
Bw Aweda alianza kuonekana akipita pita katika matawi mbalimbali ya jimbo la ukonga pasipo hata kumfahamisha aliyekuwa mwenyekiti wa jimbo la ukonga mzee Binagi, na alienda mbali zaidi hadi kufikia hatua ya kushiriki na kusimamia baadhi ya chaguzi za matawi ya chadema ndani ya jimbo la ukonga.
Kutokana na hali hiyo ya bw Aweda kujitosa kuwania uenyekiti wa jimbo la ukonga, amesababisha mtafaruku miongoni mwa viongozi na wanachama wa ukonga wakihoji kulikoni akimbie kutoka ubungo kuja ukonga?? Na kitu cha kushangaza amechukua fomu kugombea ukonga huku akiwa hajajiuzulu nafasi yake ya uenyekiti jimboni ubungo.
Hii ni dalili mbaya kwa kiongozi mkubwa kama yeye anayepaswa kuheshimu katiba ya chama pamoja na imani kubwa aliyopewa na wanachadema wa ubungo. Kama ameamua kuwasaliti wanaubungo basi hata wanaukonga hawatomuamini, kwakuwa ameonyesha dalili zote za kutoaminika na usaliti wa demokrasia.
Ushauri wangu kwa uongozi wa juu wa chadema, kuanzia uongozi wa mkoa wa dsm hadi uongozi wa taifa ni kumuangalia kwa makini mtu huyu asijekuwa ana agenda za siri dhidi ya chadema kwani wakati huu ambapo uongozi wa jimbo la ukonga wamejipanga vilivyo kuhakikisha wanashinda chaguzi zote zijazo, wamekuwa wakifungua matawi maeneo mbalimbali kuanzia kitunda, kivule, ukonga, pugu na chanika lakini sasa bw Aweda anaonekana kuwakatisha tamaa na kuleta mvurugano hadi kusababisha mzee binagi kutorejesha fomu za kugombea uenyekiti wa jimbo.
Kwa kuwa bw. Aweda ni mdau hapa JF namuomba ajitokeze hadharani kukanusha habari hii kama sio ya kweli, ama vinginevyo athibitishe kama anagombea nafasi hiyo na atoe ushahidi kwamba amejiuzulu nafasi yake ubungo ili asionekane ni mtu mwenye tamaa na ubinafsi.
Naomba kuwasilisha.