Mabagala
JF-Expert Member
- Nov 27, 2009
- 1,477
- 325
Nimekuwa na matatizo ya miguu kuuma, hali hii hunituokea pale ninapokuwa nimekaa kwa muda mrefu ama asubuhi ninapoamka. Ninapokuwa nimekaa muda mrefu, basi itauma pale ninaponyanyuka hadi nitakapoanza kutembea tu mwendo kama wa hatua 100 ivi inatulia kuuma, sana sana inauma sehemu za goti hasa hasa kwenye joints. Nikiamka asubuhi pia hali ndo hiyo hiyo. Sijaenda hospitali bado, wataalamu hapa mnaweza mkanisaidia, au kunielekeza kituo cha tiba ambacho naweza kwenda kupata tiba, Nafanya mazoezi mepesi mepesi lakni bado haijatulia