Migomo na Ubabe wa Serikali, nini hatma ya Maisha ya Watanzania?

HorsePower

JF-Expert Member
Aug 22, 2008
3,612
2,566
Kwa muda mrefu sana tumekuwa tukishuhudia serikali yetu ikishindwa kuwasaidia wananchi wake na mara kwa mara ikijikuta inatumia nguvu nyingi sana kuwalinda na kuwatetea viongozi wasio na sifa za uongozi na pia hata wale walioingiza serikali kwenye hasara ya mabilioni ya shilingi ya wavujajasho wake.

Tumeshuhudia haya kwa namna ambavyo walioingiza Tanzania kwenye mikataba feki ya Richmond jinsi ambavyo wamelindwa, na wale wa Kigoda, Deep Green, mikataba ya Radar na benki kuu na mambo mengine mengi yanayoitesa mioyo ya watanzania wengi.

Kwa sasa madaktari wameingia kwenye mgomo kudai kuondolewa kwa viongozi wawili wa ngazi za juu wa wizara husika ya afya. Serikali inajaribu kutumia nguvu kuwalazimisha madaktari kurudi kazini kwa kutumia vyombo vyake kama mahakama badala ya kusolve tatizo dogo tu la kuwaondoa viongozi wanaolalamikiwa kushindwa kutekeleza majukumu yake. Ni nani hasa serikali inapaswa kumsikiliza au kumtetea, ni mwananchi aliyeiweka serikali madarakani au kiongozi?

Nimekuwa najiuliza maswali mengi kuhusu serikali, hivi wananchi tumeiweka serikali madaraka kwa maslahi ya nani hasa? Ni sisi wananchi au kuwalinda wale walioingia madarakani kwa njia za rushwa na kushindwa kutekeleza au kutuwakilisha wananchi ipasavyo? Hivi tutavumilia hali hii mpaka lini? Ni nini sasa hatma ya maisha yetu watanzania?
 
nasubiri kuona outcome....haswa baada ya amri ya mahakama..... ila mwisho wa siku walalahoi ndo tutaumia...wao na familia zao watatibiwa india...
 
Back
Top Bottom