Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,759
- 12,175
Kifo cha mkulima pale Ikwiriri kilichosababishwa na mfugaji ni dalili tosha kuwa sasa vita ya ardhi imeanza rasmi kuinyemelea mikoa ya kusini!
Itakumbukwa kuwa wafugaji wengi walihamishwa kutoka Ihefu na kupelekwa mikoa ya Lindi na Pwani. Zoezi hili lilifanyika bila kuweka miundombinu muhimu kwa ajili ya mifugo kama majosho, maeneo ya malisho, maji kwa ajili ya mifugo na matumizi ya nyumbani, maeneo ya makazi ya wakulima na wafugaji nk.
Changamoto kubwa ni uhaba wa maji hasa wakati wa kiangazi ambapo madimbwi yote ya maji na mito mingi ambayo hutumika kunyweshea mifugo hukauka na hivyo wafugaji kulazimika kupeleka mifugo yao katika makorongo ya mito sehemu ambazo pia wakulima ambao ni wakazi asili wa huko wamekuwa wakitumia kupata maji kwa matumizi yao ya nyumbani. Hali hii imekuwa ikisababishwa ugomvi ukubwa baina ya jamii hizi mbili za wafugaji wenye asili ya wasukuma na wenyeji.
Hivyo wakati umefika kwa viongozi wa kisiasa, wizara zinazohusika na maswala ya jamii, halmashauri za wilaya wakakaa pamoja na wananchi kutafuta ufumbuzi wa changamoto hii vinginevyo tutegemee vifo vingi zaidi vya wananchi na mifugo yao, uharibifu wa mali na mazingira.
WAKATI NI HUU HAKUNA MUDA WA KUPOTEZA!