Migogoro ktk mapenzi ina nafasi gani?

Mzalendo wa ukweli

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
559
149
Ndugu wanajamvi, kama heading isemavyo; hivi migogoro katika mapenzi ina nafasi gani? Je inaimarisha penzi baada ya kusolve au inapunguza kiasi cha upendo kati ya wapendanao? mchango wako please!!!!!
 
Ndugu wanajamvi, kama heading isemavyo; hivi migogoro katika mapenzi ina nafasi gani? Je inaimarisha penzi baada ya kusolve au inapunguza kiasi cha upendo kati ya wapendanao? mchango wako please!!!!!

Kwa asilimia kubwa, migogoro ktk mapenzi inapunguza kasi ya mapenzi. Ndoa nyingi zilizovunjika chanzo chake huwa ni migogoro. Binafsi siamini sana ktk migogoro kujenga au kuimarisha penzi, ila naamini ktk uwazi wa ndani ya mapenzi nikimaanisha kuambiwa wapi nimekosea au kumwambia mtu wapi kakosea ili ajirekebishe, heshima, uaminifu, kusaidiana na upendo wenyewe kama silaha ya kulinda mahusiano.

Migogoro huleta chuki, huleta nyumba ndogo na vibustani, huleta kero, maudhi, majuto (Kwanini nilimuoa au kuolewa na fulani), magonjwa (stress, pressure, ugonjwa wa moyo, nk), vifo (wapo waliojiua na kuua kwa sababu ya ugomvi tu), yatima nk. Kwa kifupi sioni jambo jema saaana ktk migogoro kutumika kuimarisha mahusiano!
 
Ndugu wanajamvi, kama heading isemavyo; hivi migogoro katika mapenzi ina nafasi gani? Je inaimarisha penzi baada ya kusolve au inapunguza kiasi cha upendo kati ya wapendanao? mchango wako please!!!!!

Migogoro inayosababishwa na kulala na mwanamke/mwanaume mwingine mara nyingi inapelekea mapenzi kupungua kama si kuisha.

Hii ikitokea pale mnapokuwa kwenye mahusiano halafu mwenzi wako akawa anatembea nje ni hatari kabisa. Inaua mapenzi. Ila kama mligombana kwa muda na kila mtu akaendelea na maisha yake then mkarealize kuwa mnapendana, mkarudiana basi migogoro ya kuwa ulitembea na fulani mara nyingi si ya kubomoa mapenzi. Ni kukubaliana na hali iliyotokea na kusonga mbele.
 
Migogoro hupunguza mapenzi katika uhusiano, coz saa zingine mtu anapata majeraha/misukosuko kazini, kwa marafiki au kwingineko lakini akija kwako anajua anakuja kupumzika na kurelax mpaka stress kwishiney, sasa piga picha umegombana na boss, foleni halafu mkeo/mpenzi hamuongei si unakufa kabla ya siku zako?
 
Ukishasema kuwa ni migogoro basi hilo tu Neno migogoro si jambo la kheri, kwa ujumla haina tija katika ndoa.

Ndugu Miwatamu migogoro/misunderstanding ktk mapenzi ni kitu ambacho nadhani hakiepukiki 7bu si mara zote mtakuwa ktk hali ya kuelewana tu zipo nyakati ni lazima kutatokea tofauti/misunderstand, sasa inategemea mnazimalizaje hizo tofauti zenu.kama zikimalizwa vizuri mara nyingi hupelekea upendo kuimarika na kukua lakini endapo mtamaliza vibaya kuna uwezekano wa kupunguza kama sio kuua kabisa upendo. Kwa Kifupi nadhani upendo ni lazima uwe tested ili kuuimarisha. mtazamo wangu
 
Migogoro ni majaribio. No relationship is free of migogoro. Huwezi kusema hata siku moja hujawahi kukosana na ndugu yako hata mmoja. Mkikosana mnasuluhisha, yanaisha, maisha yanaendelea, mnasahau basi. Mapenzi hayapungui lakini uhusiano wenu unaweza ukawa na nguvu zaidi.

Ukikumbwa na mgogoro katika uhusiano kati ya mwenza wako, penzi linaongezeka kama reaction yenu itakuwa ni la kusuluhisha mgogoro na si kuliongezea matizo mengine ambayo pengine yatasababisha matatizo mengine. Kwa mfano, mume anahisi mapenzi yamepungua kutoka kwa mke wake baada ya miaka kadhaa ya ndo. Badala ya kukaa na kuongea na mkewe kuuliza kulikoni (labda kuna stress, au mabadiliko ambayo mke wake anapitia, you know us women!), anaamua kuenda kutafuta nyumba ndogo ambayo sio solution, na inaongeza matatizo mengine kwenye uhusiano. The best people in your life are the ones that will stick with you through thick and thin. Kwa maana, mahusiano YOTE yanapitia milima na mabonde lakini mkishikana mpaka mwisho wa safari uhusiano wenu utakuwa na nguvu na upendo mwingi mno!
 
Back
Top Bottom