Migodi mitano yaanza kulipa kodi

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

Saturday, 31 March 2012 09:45

Mwandishi wetu

WAZIRI wa Madini na Nishati, William Ngeleja, amesema miongoni mwa mafanikio ya sera na sheria mpya ya madini, migodi minne imeanza kulipa kodi ya mapato.

Akizungumza Dar es Salaam juzi, Ngeleja alisema sera na sheria hiyo vimewezesha kampuni za Geita Gold Mine (GGM), Resolute, Tulawaka na Tanzanite One kuanza kulipa kodi ya mapato ya asilimia 30.

Ngeleja alisema hivi sasa Serikali inamiliki hisa kwenye migodi na kwamba, sheria ya zamani ilikuwa haitoi nafasi hiyo. Tayari, inamiliki asilimia 45 ya hisa bila kuwekeza chochote kwenye mgodi wa Buckreef Geita, Mchuchuma na Liganga asilimia 20 na Mradi wa Mkaa Ng'aka asilimia 30.

Alisema miongoni mwa mafanikio ya sheria mpya ya madini ni kutaka kila mgodi nchini kusajili sehemu ya hisa zake kwenye Soko la Hisa Dar es Salaama (DSE).

"Hadi Desemba mwaka jana tumetoa leseni 20,000 kwa wachimbaji wadogowadogo, sasa hivi vitu watu wanajifanya hawaoni kwa lengo la kupotosha umma, nafikiri kwa lengo la kujipatia umaarufu wa kisiasa lakini Serikali iliahidi na imetekeleza," alisema.

Waziri Ngeleja alisema tayari Serikali imeanzisha utaratibu wa kuwezesha wachimbaji wadogo kupitia vituo vya Londoni Singida, Rwamgasa Geita, Bagamoyo na Mikocheni Dar es Salaam.

"Lakini tumeagiza migodi yote kununua mahitaji kutoka ndani (Tanzania) hasa maeneo ilipo, lengo ni kuondoa dhana ya wananchi ambayo kwa kweli ilikuwa ni sahihi kwamba hawanufaiki na kuwapo kwa migodi hiyo," alisema Ngeleja.

Kuhusu mikakati ya kusimamia nishati hususan gesi asilia, Ngeleja alisema wanatarajia kuanza ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam na kwamba, tayari Wizara ya Fedha imekamilisha upatikanaji wa fedha kutoka China.

Alisema kutokana na usimamizi mzuri ndiyo maana hata Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, ilipongeza Serikali kwenye taarifa yake bungeni Februari mwaka huu baada ya kuridhishwa na hatua zilizochukuliwa.

Pia, Ngeleja alisema miradi ya umeme inaendelea kwenye mikoa 16 nchini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (Rea), utekelezaji wa kusambaza umeme kupitia Mradi wa MCC kwenye mikoa ya Mwanza, Dodoma, Morogoro, Iringa, Tanga, Mbeya na Kigoma.
 
kodi pekee haisaidii sehemu zenye migodi kupata maendeleo, nadhani kodi zenyewe zinaingia serikali kuu.

Wangewawezesha wananchi katika maeneo hayo wawe na miradi inayotegemewa na migodi.

Hadi maembe wanaagiza toka South Africa!!
 
kodi pekee haisaidii sehemu zenye migodo kupata maendeleo, nadhani kodi zenyewe zinaingia serikali kuu.

Wangewawezesha wananchi katika maeneo hayo wawe na miradi inayotegemewa na migodi.

Hadi maembe wanaagiza toka South Africa!!
Hapo unamaanisha nini?
 
Hii kweli imetia fora. Kwamfano: Geita Gold Mine (GGM) ipo tangu 1890, kwahiyo sasa tusubiri mpaka 2200 ndiyo nayo BARICK ianze kulipa kodi.
 
Nikifikiri mambo yanavyo kwenda nchi hii,napata presha tupu.
Hii kweli imetia fora. Kwamfano: Geita Gold Mine (GGM) ipo tangu 1890, kwahiyo sasa tusubiri mpaka 2200 ndiyo nayo BARICK ianze kulipa kodi.
 
Back
Top Bottom