Asha Rose Migiro anafaa kuingia ikulu kipindi kijacho kwa sababu ni safi, si fisadi, hana doa. Sababu kubwa zaidi ni kuwa akina mama hawana roho za ulafi wa mali ya umma kwani ni waoga, wanamwogopa Mungu na ni watii wa sheria. Atakuwa makini katika kuongoza nchi kama akina mama walivyo makini ktk kupanga budget za nyumbani kwao. Zaidi ya hayo ana uzoefu wa kimataifa.Vile vile hebu tumpe mwanamama sasa kwani TUNAWEZA tukipewa nafasi. Tangu tupate uhuru ni kinababa tu. Kwani marais wanawake nchi nyingine duniani wana nini ambacho wanawake wa Tz hawana? Wana JF nadhani hoja yangu imepita bila kupingwa.
Naomba kuwasilisha.
Ameshindwa nini? Kama kilaza angefika huko? Wewe umefanya nini cha maana mpaka kumwita mama wa watu kilaza, acheni dharau bana,wewe ukiambiwa mama yako ni kilaza utakubali?
Hayo yote ni kweli kabisa. Lakini je na hao waliokuwa marais walitumiwa na nani hadi kila wakimaliza kipindi cha uongozi wanasemwa vibaya tu? Pia marais watatu mfululizo walipokuwa wakipigiwa chapuo tuliambiwa ni safi, ni wenzetu, tuwape kura za ndiyo. Sasa je kiko wapi? Mbona sasa wanaitwa mafisadi? Bado nasema Migiro anafaa kuwa rais kwa sababu naye ni binadamu si malaika and no human being is perfect.Getrude mongella alipewa kuwa Rais wa bunge la Africa akaishia kutia aibu nchi kwa ubadhilifu!!! Mnapigiwa chapuo ili mpate madaraka sababu yenyewe ni kwamba hao watakaowafadhili wanajua ni rahisi kumtumia mwanamke akiwa kiongozi; mfano ni Anna Makinda anavyotumiwa na jakaya Kikwete kufanikisha matakwa yake binafsi yasiyokuwa na tija kwa nchi!! Asha Rose will be worse than Makinada.
Asha Rose Migiro anafaa kuingia ikulu kipindi kijacho kwa sababu ni safi, si fisadi, hana doa. Sababu kubwa zaidi ni kuwa akina mama hawana roho za ulafi wa mali ya umma kwani ni waoga, wanamwogopa Mungu na ni watii wa sheria. Atakuwa makini katika kuongoza nchi kama akina mama walivyo makini ktk kupanga budget za nyumbani kwao. *Zaidi ya hayo ana uzoefu wa kimataifa.Vile vile hebu tumpe mwanamama sasa kwani TUNAWEZA tukipewa nafasi. Tangu tupate uhuru ni kinababa tu. *Kwani marais wanawake * nchi nyingine duniani wana nini ambacho wanawake wa Tz hawana? Wana JF nadhani hoja yangu imepita bila kupingwa.*
Naomba kuwasilisha.
Sawa kabisa. Wanawake hawawezi kuperform vizuri. Je wanaume wanaweza? Mbona hao waliopita hawasifiwi? Kwa mantiki hiyo Migiro anafaa.ameshindwa kupewa 2nd term kwa kuwa ni kimeo. km kweli alikuwa ni mahiri, ban ki moon angempa kipindi cha pili. kachemka. wawmawake watz wote waliokwenda kufanya kazi kimataifa walichemka eg mama mongela, bongo hapa twaona jinsi makinda anavyochemka. kwa hiyo tuna precedent nzuri sana kuwa hawawezi kuperfom vzr. lakini mleta thread km unampenda sana migiro mwalike ukanywe nae chai.
Mwinyi, Mkapa na Kikwete walifanya kitu gani hadi wakapewa urais?Usafi na kukosa ufisadi si sifa. Hivi ndivyo kila mtu anavyotakiwa kuwa.
Dr. Migiro amefanya kitu gani kusema apewe urais?
Asante kwa kunielimisha. Na kwa mtazamo wako huo unafikiri ni nani anafaa kuwa rais kipindi kijacho?Mkuu mamayeyo,
Ni mawazo mazuri taifa kufikia muda kuwa na rais mwanamke hasa ukizingatia nchi hii haijawahi kupata rais mwanamke.
*Bahati mbaya mpaka sasa hivi hatuna mwanamke Tanzania anayeweza kushika nafasi ya uraisi hasa ukizingatia changamoto zinazokabili taasisi ya uraisi nchini, majukumu yanayomkabili rais wetu *ajaye na matarajio ya wananchi.
maadui wakubwa wa nchi hii baada ya uhuru-kama mara nyingi ilivyoainishwa na baba wa taifa *Mwl. Nyerere ni ujinga, umaskini na maradhi.*
Bahati mbaya kutokana na uongozi dhaifu hasa baada ya awamu ya Mwl.Nyerere, maadui hawa wamejijenga zaidi Na maadui wapya wameibuka. maadui walioongezeka ni Ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka na sasa hivi udini! matumizi mabaya ya madaraka yametokana na katiba mbovu Na sheria ambazo haziwezi kuwajibisha viongozi.*
Udini umeletwa kwa makusudi na baadhi ya viongozi ili kujipatia umasrufu Wa kisiasa kiurahisi.
kwa hiyo mkuu, Sasa hivi nchi yetu inahitaji kiongozi atakayeweza kukabiliana Na changamoto nilizizitaja hapo juu. Tunahitaji rais atakayeweza kupambana na mfumo wa kifisadi ambao ndio kikwazo kikubwa kwa nchi hii kuweza kupata Maendeleo-huyu candidate wako hili haliwezi. tunahitaji rais atakayejenga mfumo wa viongozi kuwajibika-huyu mtu wako hili haliwezi! tunahitaji mtu atakayeondoa matumizi mabaya ya madaraka, kuondoa katiba Na sheria zinazogandamiza wananchi-huyu mwanamama hawezi. tunahitaji kiongozi atakayesimamia rasilimali za nchi yetu zitumike kwa ajili ya wananchi Na Maendeleo Na nchi-chaguo lako hawezi. Vile vile Nadhani huelewi kwamba chaguo lako alishindwa ku-deliver UN ambako taratibu za majukumu ziko clear. Je hapa ambako kila kitu si clear atafanya nini?
Mkuu Nakukumbusha kuwa rais wa nchi, kwa nchi zenye kuhitaji Maendeleo, huchaguliwa kwa kuzingatia mahitaji halisi ya nchi wakati huo. Tofauti Na hapa mnachagua rais kwa kuzingatia uchama na ushabiki Wa kisiasa badala ya mahitaji ya nchi wakati huo Na uwezo Wa candidate ku-deliver.
halafu Mkuu, uwezo Wa mtu haupimwi kwa kuangalia mhusika ameshika nafasi zipi Na ngapi za uongozi, bali akiwa katika hizo nafasi amefanya nini katika kuleta Maendeleo ya watu anaowaongoza.
Nadhani Mkuu mpaka hapo ingawa nimeeleza kwa ufupi nadhani angalau *umepata mwanga kidogo ni kiongozi gani tunayemhitaji ili aokoe Jahazi letu la Tanzania ambalo linazama kwa kasi.
Ndio maana safari hii unatakiwa utuambie huyo mama kafanya kitu gani hadi apewe Uraisi? Hayo makosa kama yalifanyika huko nyuma, hayatakiwi kurudiwa tena, la hasha. Safari hii tunataka kuhakikisha mtu anayekacha mdahalo kama Kikwete hapewi nafasi kabisaa na katika huo mdahalo itabidi aeleze amewahi kusimamia nini na kwa kiwango gani cha ufanisi. Hivyo wewe hapa unatakiwa kutetea hoja yako kwa kutueleza ni kitu gani amewahi kukifanya huyo mama hadi apewe Uraisi, simple!Mwinyi, Mkapa na Kikwete walifanya kitu gani hadi wakapewa urais?
UN ni zaidi ya nchi 100 tofauti na katanzaniaun imemshinda, nchi ataiwezea wapi?
Ameshindwa nini? Kama kilaza angefika huko? Wewe umefanya nini cha maana mpaka kumwita mama wa watu kilaza, acheni dharau bana,wewe ukiambiwa mama yako ni kilaza utakubali?
Oh sorry mkuu, mie sina radio. Na kama kulikuwa na mjadala kama huo basi ni dalili nzuri.We mleta mada huu upumbavu umecopy na kupaste kutoka bbc matangazo ya jioni hii palikuwa na mjadala wa kipumbavu hivi hivi.