Migiro arejea na uzoefu kibao

huyu mama angekua mchapa kazi basi angekaa term hii nzima ya pili ya ki-moon inaelekea kazi zilimshinda huko na hii siasa ya ccm na kina lowassa huyu mama hataiweza watamrushia sumu akimbie..bora ajifungie huko mlimani

Wanaweza kumwakyembe anatakiwa kuwa makini vinginevyo aachane na siasa!!!!

Kumbe alikuwa amejenga nyumba kule mlimani? I stand to be educated. Hicho chuo cha mlimani ni family business whereby you can go to the moon for whatever period and come back to "teach" if things don't turn out well up there for some strange reason or other, au ni ajira kama nyingine?
 
Binafsi naona hiyo ndio last choice aliokuwa nayo vinginevyo ingebidi akae tu nyumbani after poor performance alioionesha UN. Kwa mtu wa kariba yake sio wa kwenda kufundisha tena Darasani hilo kimsingi nakataa kabisa. Kwa level aliokuwa amefikia alitakiwa Taasisi zingine za UN ziwe zinamgombea kama mpira wa kona, au hata International NGOs lakini sio kurudi down to the bottom kuripoti kwa Mkandara Rwekaza. Sasa kama yeye katoka UN anarudi to that level JK akitoka Ikulu ataenda wapi?

Ki ukweli mama nakupa pole sana. kwa hali hii hata Ubunge tu haukufai sembuse Urais!
 
Mbona Condoleza huwa anafundisha?
 
Ndio kwanza ameng'atuka huko UN. Mpe muda. Atabebeshwa majukumu mengi tu kama unavyomwona Koffi Annan sasa. Usishangae akawa mwanamke wa pili Mwafrica kupata Nobel Peace Prize. Huyu mama ana sifa zote za kuwa KIONGOZI wa kitaifa na kimataifa. Hana udini (kaolewa na mkristo), hana ukabila (kaolewa na Mkara), hana makundi wala maswahiba wa nguvu.
 
Mbona Condoleza huwa anafundisha?
Endeleaaa hajui hilo. Hata Mikhail Gorbachev aliyekuwa Rais wa USSR anafundisha. Kufundisha ni WITO, ni KIPAJI na ni HOBBY. Anataka huyu mama awe mfanyabiashara achafuke. Awe fisadi. Apige ma-deal kama akina Mkapa. Mimi huwa nawashangaa maprofesa tulionao pale Bungeni. Badala ya kuomba vipindi pale UDOM wanabaki kukimbizana na vyangudoa wa DOM na Dar.
 
Wabongo eti wanaona kazi ya kufundisha atakuwa anajishusha, how absurd!

Kweli kuna watu wanadharau.
 
Dr.Asha-Rose Migiro,aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amerejea nchini. Aliporejea tu,akadakwa na wana-CCM mbalimbali ili wajikombe kwake na wamuombe agombee Urais 2015.Anaonekana 'Msafi' pekee aliyebakia CCM. Kitu ambacho si cha uhakika. Ugonjwa wa CCM hauna kinga wala tiba.

Kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari jana,Dr.Migiro amesema yeye anarejea UDSM kufundisha Sheria. Akapokelewa na Mwajiri wake,Prof. Rwekaza Simpho Mukandara kurejea kazini.Tayari amerejea kwenye nyumba yake iliyopo UDSM Sehemu ya Mlimani. Je, kauli yake ni dhabiti au danganya-toto? Tujadili...

why bothered??? be it true or not why troubled??
 
Kama hataki siasa usimlazimishe. Listen to what the Lady wants.

Siasa anapenda sana. Siasa ni kama bangi, ukiishahonja tu kuiacha ni kaaaaazi! Only that the lady is very strategic, politically. Na ninafikiri kukaa kwake UN na pia ku-experience utamaduni wa siasa wa US vinamsaidia sana katika kuwa strategic - angaa hapa amejitofautisha na kujibainisha kidogo na magamba wenzake.
 
Huyu mama hawekezi kwenye SIASA. Anatumia TAALUMA yake zaidi. Anajua pia wenzake wa CCM walivochafuliwa na SIASA. Hauwezi kumfananisha na mwanamke yeyote nchi hii aliyewahi kuwa mwanaSIASA na akashika madaraka makubwa ya kiwango chake. Jana pale UDSM alipokelewa na watu wa ngazi zote.
 
Bora akashike chaki pale mlimani na endapo ataamua kurudi kwenye siasa fasta tutamuokota msitu wa Mabepwande akiwa Mfu
 
..there is a lot she can do academically.

..mimi napendekeza hata aanze kwa kuandika kuhusu experience yake alipokuwa UN.

..pia anaweza kuendelea kupewa kazi maalum na makatibu wakuu wa UN.

..hakuondoka pale kwa kashfa au mahusiano mabaya na bosi wake, au mataifa makubwa.

..nakumbuka katibu mkuu wa muda mrefu wa Commonwealth, Dr.Shridath Ramphal, alirudi nchi kwake na kushika chaki. siyo kitu cha ajabu hata kidogo.

..lazima kuwe na utaratibu na mazoea ya wasomi kwenda kwenye sekta binafsi, siasa, NGOs,etc na kuweza kurudi tena kufundisha.

NB:

..Condeleza Rice pia amerudi kufundisha.

..Madeleine Albright naye amerudi kufundisha na ameandika vitabu kadhaa.

..Raisi Kaunda, na Raisi Amani Karume, walikuwa Harvard Univ kwa program maalum ya kufundisha.

..Kwanini viongozi wetu hawataki kwenda kufundisha vijana wetu??

..pia majuzi, Dr.Henry Kissinger, nguli wa diplomasia ya US, secretary of state aliyefungua mashirikiano ya China na USA, ameamua kutoa nyaraka za shughuli zake alipokuwa serikalini kwa chuo kikuu cha Yale.
 
UN wakitaka kukutoa kiaina wanasema unajua tuna review miundo na mifumo-then you are sacked with your kifuta jasho!
 
*Huyu mama bado ni dhaifu na mwoga sana kisiasa,kifupi hana record yoyote ya utendaji wa kijasiri.
*Kipekee ni mtulivu, msikivu na msomi mzuri wa sheria japokuwa hana mchango wowote ktk changamoto tunazozikabili kwa sasa.
*Anna tibaijuka na Magreth Sita walikuwa jasiri zaidi lakini baada ya kuingia kwenye system ya CCM wamekuwa dhaifu kama Vasco da Gama.
*Migiro ni mtu wa kubebwa,kuongozwa na kupangiwa kila kitu. Tazama nafasi zote za uongozi alizoshika ni za mlango wa nyuma au Upendeleo tu(ubunge 2X, Uwaziri2X, Unaibu katibu mkuu UN) mwanamke mtanzania yoyote angeweza kuzipata tu kama akiwezeshwa!!
*Mahali pekee panapomfaa kisiasa kwa sasa ni kujipanga kugombea ubunge jimbo la Mwanga tena kupitia Upinzani kwani Prof.Maghembe na CCM yake kwa sasa wapare wa Mwanga wamewachoka.
Kwa uraisi bado sana na hafai kabisa.
*Suala la kurudi kufundisha UDSM ni la muda tu na tena ni danganya toto,lengo ni kutulia,kusubiri na kusoma upepo. Kwa kuwa hajasema anaachana na siasa kabisa kabisa,basi ujue anasoma mchezo wa siasa za Bongo kabla hajaziingia kwa kasi.
*Kifupi hakuna mtu aliyeingia kwenye siasa kwa miguu miwili kama yeye halafu arudi kwenye professional yake ya awali,ukishaingia kwenye siasa unazeekea na kufia hukohuko!!
 
Naamini una chuki binafsi na huyu mama wa watu,yaani hata akirudi UDSM ambako ndiko alikopita na records zake zinajulikana vema pale UDSM wewe hutaki,kesha sema hataki u rais basi tuliza mzuka ndgu.

Imani yako kuwa ninamchukia si lazima iwe na ukweli. Ninamfahamu kama ASG, sio kama waziri wa mambo ya nje au mhadhiri chuo kikuu. Alisema anapumzika na tukaamini hivo, kumbe anarudi kwenye kazi yake ya zamani. Maana yake ana nguvu bado za kufanya kazi. Yeye pamoja na watu wengine walishindwa kufanya maamuzi katika mambo waliopewa. Kwa wenzetu kuna kitu wanaita "Result-Base Performance". Hakutoa matokea yaliyokusudiwa!!

Ndio ugonjwa wetu huko nyumbani, hakuna vipimo kati ya matarajio na matokeo. Tunaona watu wanahamishwa kutoka sehemu moja kupeleka matatizo sehemu nyingine badala ya kuwaondosha!!
 
Bora akashike chaki pale mlimani na endapo ataamua kurudi kwenye siasa fasta tutamuokota msitu wa Mabepwande akiwa Mfu

Si wanasema ana undugu na marehemu Baba wa Taifa labda watamuogopa kwa hilo.
 
Hivi watu mna akili gani? Kuamua yeye kufundisha mbona ni topic kwenu? Halafu nyie nyie ndo mnataka mabadiliko. Kweli nabii hakubaliki kwao. Ni mtanzania wa kwanza kushika nafasi hiyo tulipaswa kujivunia. Sasa unayeongea kuhusu rekodi ya utendaji wake akiwa UN wewe unafanya kazi wapi?
Mbona tunapenda ku speculate tu mambo. Yaani tunashadidia vitu kimbea kimbea. Halafu mtu anajiita Great thinker. Mwàcheni mama wa watu apumzike. Nyie mmeifanyia nini Tanzania zaidi ya kulalamika tu mpaka mnaboa. Great mind discuss ideas. But here you are discussing people.
 
Watu wamekaa kimbea mbea tu.kama ameamua kuridi kufundisha ni maamuzi yake. Sasa kuanza kumnchafua inasaidia nini. Wewe unayesema ame underpaerfom ni kitu gani ambacho umekifanya amabacho kweli kina manufaaa kwa hata mtaa unaoishi. Kazi kulaumu tu. Lazima tujifunze kuheshimu na kuenzi watu waliopeperusha bendera yetu kimataifa.
 
Back
Top Bottom