Migiro arejea na uzoefu kibao

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,298
33,083
dr%20migiro.jpg

Dk. Asha-Rose Migiro


Wakati Dk. Asha-Rose Migiro, anarejea leo nchini baada ya kumaliza muhula wake katika nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), amesema nafasi hiyo imempatia uzoefu mkubwa katika nyanja mbalimbali za kimataifa.

Akitoa tafakuri yake juu ya muhula wake katika nafasi hiyo, uliodumu kwa miaka mitano na nusu, Dk. Mingiro amemshukuru Katibu Mkuu wa UN, Ban Ki-moon, kwa kumpa fursa hiyo, Rais Jakaya Kikwete na Watanzania kwa kumpa moyo na kumuenzi wakati wa utumishi wake.

Dk. Migiro alisema kwa kufanya kazi na UN, amepata fursa ya kuchangia juhudi za pamoja za kuimarisha umoja huo kutekeleza majukumu yake katika kipindi kigumu kimataifa na chenye changamoto nyingi.

“Utumishi wangu katika Umoja wa Mataifa ulikuwa fursa adhimu iliyonipa uzoefu wa pekee. Kazi hii imeujaza moyo wangu unyenyekevu wa dhati kwani niliingia Umoja wa Mataifa wakati ambapo dunia inachagizwa na madhila makubwa makubwa yakiwemo maradhi, umaskini wa kupindukia, kutokuwapo kwa usawa wa kijinsia,…na changamoto nyingine nyingi,” alisema.

Hata hivyo, Dk. Migiro alisema wakati akimaliza muhula wake, anatiwa moyo na taarifa kuwa juhudi za kupambana na umaskini duniani zimeanza kuzaa matunda licha ya ukweli kuwa dunia kwa sasa inapita katika kipindi kigumu kiuchum kuliko wakati mwingine wowote kwa miaka ya karibuni.

Katika tafakuri yake, Dk. Migiro alizungumzia mafanikio pia changamoto kwenye nyanja mbalimbali ambazo yeye na watumishi wenzake kwenye taasisi hiyo ya juu kimataifa wameyafanyia kazi.

Baadhi ya maeneo aliyoyazungumzia ni pamoja na Malengo ya Maendeleo ya Milenia barani Afrika, mkutano wa Rio + 20, usawa wa kijinsia, afya ya jamii, mageuzi katika menejimenti ya UN na utawala wa sheria.

Kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa wa Naibu Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa, Dk. Migiro alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa katika Baraza la Mawaziri la kwanza la Rais Jakaya Kikwete.





CHANZO: NIPASHE

 
Mbona inasemekana ameboronga UN? nafasi ya unaibu katibu mkuu huwa muda wake unaisha kabla ya muda wa katibu mkuu kwisha???
 
Kama maadili ya UN kwa viongozi wa ngazi za juu wakistaafu hawatakiwi kujihusisha na siasa katika nchi zao kwa muda fulani; sasa mimi nataka kujua kipimo cha muda huo, yaani labda miezi au miaka kadhaa. Naomba utuambie huo muda fulani ni miaka mingapi kabla hatujamuuliza bwana Ki-moon!

Source: Habari leo 10/07/2012
 
Dr.Asha-Rose Migiro,aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amerejea nchini. Aliporejea tu,akadakwa na wana-CCM mbalimbali ili wajikombe kwake na wamuombe agombee Urais 2015.Anaonekana 'Msafi' pekee aliyebakia CCM. Kitu ambacho si cha uhakika. Ugonjwa wa CCM hauna kinga wala tiba.

Kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari jana,Dr.Migiro amesema yeye anarejea UDSM kufundisha Sheria. Akapokelewa na Mwajiri wake,Prof. Rwekaza Simpho Mukandara kurejea kazini.Tayari amerejea kwenye nyumba yake iliyopo UDSM Sehemu ya Mlimani. Je, kauli yake ni dhabiti au danganya-toto? Tujadili...
 
Ni bora afanye kazi ya kufundisha, hapo ndio impact yake kwa jamii itakuwa kubwa zaidi. Hakuwa wa msaada mkubwa kwa Ki-Moon. Akikubali kuingia ktk siasa basi ajue kuwa ataimarisha au kuunda kundi jingine ndani ya CCM. Mwisho haitakuwa na tija coz serikali imetumia vibaya reasources za nchi wakati ikijaribu kukinzana na kambi kadhaa ndani ya CCM!! Watakaokuwa victims ni wananchi watazamaji.

She was very poor in the UN. Very!! She did not choose to step down, her hand was forced. Including a few others, sio yeye tu.
 
Dr.Asha-Rose Migiro,aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amerejea nchini. Aliporejea tu,akadakwa na wana-CCM mbalimbali ili wajikombe kwake na wamuombe agombee Urais 2015.Anaonekana 'Msafi' pekee aliyebakia CCM. Kitu ambacho si cha uhakika. Ugonjwa wa CCM hauna kinga wala tiba.

Kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari jana,Dr.Migiro amesema yeye anarejea UDSM kufundisha Sheria. Akapokelewa na Mwajiri wake,Prof. Rwekaza Simpho Mukandara kurejea kazini.Tayari amerejea kwenye nyumba yake iliyopo UDSM Sehemu ya Mlimani. Je, kauli yake ni dhabiti au danganya-toto? Tujadili...

sekondari za kata nazo hazina walimu, kwani lazimA afundishe sheria mlimani udsm?
 
Hata Prof. Mwandosya alisema bora rais amuache arudi UDSM akafundishe. Lakini Rais JK akamteua kuwa Waziri asiye na Wizara maalumu.

BTW, UDSM sasa hivi nayo imekuwa kichaka cha CCM. Nakumbuka Dr. Masumbuko Lamwai walimukatalia kurudi UDSM baada ya kuwa katika siasa. Sasa kwanini huyu Dr. Asha Rose Migiro akubaliwe? UDSM sio ile tuliokulia sisi, It will never be the same again "Chachu ya Fikra Mpya"
 
Back
Top Bottom