Mifuko ya NSSF /PPF ianze kutoa riba 10% kwa wafanyakazi waliostafu

Keneth

Senior Member
Sep 29, 2011
195
47
Tumsifu Yesu Kristo.
kumekuwa na malalamimko mengi hasa katika mifuko ya hifadhi ya jamii ,kuwanyima watu pesa zao kwa minajili ya kuwa serikali imetoa amri ya kutolipa wananchi watakaodai pesa zao baadaa kuachishwa kazi wakiwa chini ya miaka 50.

Hii imetokea hasa katika ofisi za NSSF/PPF Mtwara kuwa sheria imebadilika na mtu anatakiwa kulipwa mafao yake baada ya kufikisha miaka zaidi ya 50 licha ya kupata kazi ambayo haidumu kwa miaka zaidi ya mitano,kama wafanyakazi wa serikalini.

Hili limefanya watu wengi kupoteza fedha zao nyingi kufatilia mafao yao ambayo alikatwa kihiari kwa minajuli kuwa baaada ya kuachishwa kazi au kuacha kazi anaweza kufanya jambo la msingi au biashara zake kutokana na malengo yake.

Hii inafanya wananchi kuona hakuna faida ya kukatwa fedha zao kwenye mifuko ya jamii kutokana kuwa uhimili wa ajira zao haudumu kwa zaidi ya miaka zaidi ya 3 au 4.

kama mtu kafanya kazi kwa miaka zaidi ya miwili au tano na kuachishwa kazi akiwa na miaka 35 hawezi kusubiri kuchukua fedha yake baada ya miaka zaidi ya miaka 50.

Pia haya makampuni ya yanayowekeza Tanzania kwa miaka mitatu na kuondoka tutayapata wapi kuthibitisha kama mm nilikuwa mfanyakazi halali wa kulipwa kiwango hicho

Kama hyo haotafanikiwa basi haya makampuni yaweke interval ya kila mwanachama anayekuwa ameacha / kuachishwa kazi awe analipwa Riba ya 10% kila baada ya miaka mitano

. Tuwe makini na kama sheria hii haikujadiliwa na bunge iangaliwe upya maaana inaonekana kuanza kufanya kazi
 
Unaambiwa order imetoka kwa JPM, hela hizo zijenge viwanda alivyoahidi kwa wapiga kura!! Utaelewa hapo hapo!! Hela zetu ndio zijenge viwanda walivyoahidi!
 
1. Riba ni haram
2. Kuchangia hifadhi ya jamii kwa mwajiriwa ni lazima (kwa mujibu wa sheria).
 
Inasemekana Sheria hii ilipitishwa tangu mwaka 2012 ambapo fao la kujitoa liliondolewa ambapo nakumbuka kulikuwa na mjadala mkali sana bungeni.
Sasa baadae nikasikia imeruhusiwa fao la kujitoa liendelee. Inaonekana kumbe ni maamuzi ya kisiasa yaliruhusu fao hili liendelee ambapo kisheria bado halikurusiwa.

Tunayo kazi kubwa sana ya kupigania fao hili na kama waliruhu kulitoa bila sheria kuruhusu sio kosa letu wananchi ni,makosa yao.
 
Huu ndio ujua wa viongozi wetu kwa kuamua matakwa ya taifa kisiasa, hii nchi inahitaji mabadiliko ya mfumo na mfumo wenyewe uwe katika katiba
 
Unaambiwa order imetoka kwa JPM, hela hizo zijenge viwanda alivyoahidi kwa wapiga kura!! Utaelewa hapo hapo!! Hela zetu ndio zijenge viwanda walivyoahidi!
Hapa ndipo mie naona sisi watanzania ni Mazombies tu. Hakuna TUCTA kupinga hili. Hivi huyu Magufuli amekuwa Mungu wetu kila analolisema basi hakuna wa kulipinga? Hizi ni pesa zetu, pesa za jasho langu nililolitoa. Leo hii unanipangia matumizi ya pesa zangu kweli inakuja hii? Kwani life span ya Mtanzania ni miaka mingapi mpaka JPM aseme tulipwe mafao yetu? Nikifa kabla sijafikisha hiyo miaka je?
Eti nina nia njema na watanzania!! hii ni dhuruma. Hii siyo haki kabisa. sasa naanza kuwaelewa wapinzani wanachokisema kinaweza kuwa na ukweli ndani yake.
 
Sheria za kuzuia mafao ya kujitoa ilisainiwa na Rais mstaafu Mhe. JK wakati huo hata JPM hajui Kama atakuwa Rais!!! Acha UONGO!!!

Queen Esther

Unaambiwa order imetoka kwa JPM, hela hizo zijenge viwanda alivyoahidi kwa wapiga kura!! Utaelewa hapo hapo!! Hela zetu ndio zijenge viwanda walivyoahidi!
 
Back
Top Bottom