Mifuko ya kijamii (NSSF, PPF) na kuifadhili CCM tena uchaguzi wa 2015

Kwa hiyo CDM wakiingia madarakani hii mifuko inakuwa kama benki, watu wanaweka na kuchukua kama upatu, DECI, ukitaka unapat pesa yako bila usumbufu hata hujafikisha umri maana ni yako, au siyo? wewe usitake kuharibu chama chetu, huu usha biki mwingine wa kijinga kabisa, nani ataruhusu pesa za pensheni ziende CCM, huu ni wehu kabisa, fikrazilizo lala hizi, sioni aibu katika hili, mnakuwa kama hamjui kwa makusudi, pesa ya hifadhi ya jamii leo iwe kama benki kweli? nchi gani tutakuwa tunatengeneza hii, mimi nakubaliana na unemployment benefits kama serikali inaweza lakini hizi za uzeeni zibakie jamani mtakuwa na hli ngumu huko mbeleni, shauri zenu endeleeni kutumia masaburi kufikiria.
Huu ni uwizi wa wazi wa mchana kweupe! Hatukubali
 
jamani kwa kweli kwa jinsi ninavyoifahamu Tanzania hii ya serikali ya ccm tutalalamika weeeee alafu yataisha,itabaki tu kuwa ulikuwa ni upepo.PLZ JAMANI KWA HILI EBU TUPEANE MODARITY NINI CHA KUFANYA ILI HATA KAMA NDO MWISHO WA HII SERIKALI DHALIM LIWALO NA LIWE.....EBU SASA TUJE NA NINI CHA KUFANYA,KULALAMIKA INATOSHA SASA.
 
yule kiongozi wa shirikisho wa chama cha wafanyakazi, mbona amepiga plasta mdomo kwenye hili???

Papaa Mgaya? Achana naye keshageuka mnara vwa chumvi!!!...........mbayuwayu mkubwa kabisa.

cuf5.jpg
 
jk anawakomeshaje wafanyakazi,sindio huyu alisema kama na kura zenu (wafanyakazi) hazitaki.sasa mnasubiri nini?
 
pamoja na mambo mengine nashauri kuchukua takwimu kutoka kwa wabunge wetu waliokubaliana na sheria hii kwa kuwauliza watakapofika majimboni kwetu au kwenda kupata ufafanuzi ktk ofisi zao. baada ya zoezi hili ndo tutawajua wachawi na waumiani wetu. hatua inayofuata ni kuweka mkakati wa pamoja kwa wafanyakazi katika kila jimbo kutomrudisha bungeni mbunge aliyepitisha mswada na baadae sheria hiyo. na kwa wale wabunge wasiokubaliana na sheria hii kuendelea kupigia kelele sheria hii bungeni na kwenye mikutano ya hadhara kwa kuwahamasisha wafanyakazi wote nchini kuunganisha nguvu zao na kuwaorodhesha wafanyakazi kukusanya saini zao kwa wote wasioafikiana na suala suala hili na kuwakabidhi wabunge kuliwakilishakatika kwenye vyombo vya maamuzi(bunge) .
 
Ndibalema@ si mbaya kwanza watu wakapeana ufahamu kuhusu kadhia hii kwani na hakika watu wengi tulikuwa hatuna ufahamu na mabadiliko haya ya sheria za hii mifuko ya hifadhi za jamii,sasa kupitia haya mathread yanayokuja kila siku ufahamu wa kadhia hii unakuwa bayana.Lakini pia ni vema basi wengine wakija na topic ya NINI KIFANYIKE kama ulivyoliona mkuu.Mimi naona cha nini kifanyike inabidi wafanyakazi waanze strike katika sehemu zao za kazi kugomea waajiri wao kuwakata michango hiyo na ni rahisi kiasi kwa wafanyakazi wa sekta binafsi kupitia vyama vyetu vya mahali pa kazi,hii itasaidia kuibua presha ya kadhia hii kutoka kwa waajiri kisha wafanyakazi wakipata sapoti ya waajiri hakika mwanzo wa suluhu utakuwa umepatikana.
 
Kwanza hawa wabunge halipi kodi, ina maana tunawalipia sisi.....hii ni haki kweli, na bado watufuate kwenye kidogo wanachowekwa, maana hakizai... interest wachukue wao, wewe unakuja kutoka na ile hela uliyoiweka tena imepoteza thamani, Ni nani wa kututetea??? Ikiwa nchi zilizoendelea, mtu akistaafu ana furahi na ni neema, kwa namna ile hela yake ilivyozaliswa and he is part of it...wanakuwa na shares, sasa sisi hizo investments zinamfaidisha nani??? Halafu walijadili lini bungeni??? Mungu tusaidie kutoka kwenye vinywa vya mamba. Tuungane wafanyakazi kwa hili; tusikubali....tumechoka....
 
Toeni mikakati; cha kufanya nini?? Maana wabunge wametusaliti, wametudharau....wametupuuza....kwa kupitisha kitu hata wadau wenyewe hawana habari wala kuulizwa...
 
Back
Top Bottom