Midomo ya viongozi italivunja taifa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,125
Maoni ya Katuni
Mazingira ya kisiasa na uwezekano wa uendelezaji wa shughuli za maendeleo au uwekezaji umeingia mashakani katika maeneo kadhaa nchini, kutokana na jazba zinazoongezeka, na kuwa hulka halisi katika maeneo hayo, kutokana na kauli za viongozi maeneo tofauti.

Matukio mawili muhimu ni kuchomwa makanisa mjini Zanzibar baada ya polisi kuwakamata viongozi wa maandamano ya Jumamosi, na huku wimbi linaendelea wilayani Meru kuvamia na kuteketeza mali katika mashamba ya maua, ambayo ni

muhimu kwa mauzo ya nje katika sekta ya kilimo. Matukio hayo mawili yalitokana na matamshi, kauli.
Serikali ya Zanzibar ilielekea kupata ganzi isiweze kufanya kazi pamoja katika kujiuliza nini kimetokea, hadi Rais Dk. Ali

Mohamed Shein alipotoa hotuba na kusema vitendo vya uvunjifu wa amani havitavumiliwa.
Haikupita hata siku nzima kikundi cha mihadhara kikajibu kuwa mihadhara yao itaendelea, ambao ina maana kuwa

ikizuiwa fujo zitaendelea, huku wakikanisha kuhusika na kuchoma makanisa.
Ni hali ambayo inaanza kutoka mikononi mwa uongozi wa kisiasa na kuwa ya kipolisi, na kwa vile sasa mapambano ni ya kidini kwa kivuli cha Muungano, yataenea vile vile Tanzania Bara punde.

Ukiangalia kwa karibu unakuta kuwa mabadiliko haya katika mazingira ya siasa na uchumi nchini kwa upande mmoja ni ya kimsingi, kutokana na wimbi la kukata tamaa kimaisha na kulazimisha majawabu, iwe ni kunyang’anya mashamba au ni kuvunja Muungano.

Lakini kabla ya kufikia hapo kulikuwa na matamshi ya viongozi wa ngazi za juu ambao wanaaminiwa kikamilifu na wale wanaowasikiliza, hivyo wakisema hili lazima lifanyike, au jambo fulani ni baya kwetu, hakuna tena nafasi ya ‘kutoa elimu’ kwa wananchi kuzuia wasijichukulie sheria mkononi. Wanayemwamini ameshawaambia jambo hilo, basi.

Matamshi mawili muhimu yalitolewa kabla ya hali kuchafuka hivi karibuni, kwa upande wa Zanzibar ni matamshi ya viongozi waandamizi wa Chama Cha Wananchi, yaani katibu mkuu Maalim Seif na naibu wake upande wa Zanzibar, Ismail Jussa Ladhu.

Walisikitishwa kushindwa uchaguzi mdogo wa Baraza la Wawakilishi ambako mgombea wa CCM alishinda akifuatiwa na wa Chadema, wakadai kuwa sababu ya matokeo hayo ni wingi wa makanisa Visiwani. Sasa yakitokea mazingira ya

mtafaruku wa kisiasa kati ya wanamihadhara na polisi, na hata kama Maalim Seif hajui kinachoendelea, si watatoka huko vijana watatu au wanne, wakikumbuka alivyosema kiongozi wao mpendwa, wakayachoma hayo makanisa?

Mashindano ya kiimani na hata imani za kisiasa ni hali ambayo mtu hawezi kuizuia, kwani ndiyo hasa chachu ya imani na mashindano ya kisiasa, hasa kwa kipindi hiki cha mjadala mgumu wa hatma ya taifa kupitia uandikaji mpya wa Katiba.

Na pia yapo mashindano ya kiitikadi na kuaminiana kisiasa wakati wa uchaguzi, kwa mfano kutoa ahadi kwenye chaguzi za ubunge na hata urais, lakini tatizo la kuvuka mpaka katika matamshi linajitokeza katika maeneo hayo pia.

Rais Mstaafu Benjamin Mkapa aliwaahidi wananchi wa Meru kuwa atamshauri Rais Jakaya Kikwete kuwaondoa wawekezaji wa maua ili mashamba hayo yarudishwe kwa wananchi; walipoanza kuyachoma, kuna lolote la kushangaza hapo?

Na kwa njia hiyo hata viongozi wa dini wamesaidia kufikisha nchi hapa ilipo, kwa kutumia mimbari zao baada ya uchaguzi mkuu uliopita, kueneza uvumi kuwa mgombea wa Chadema alishinda kwa kura nyingi lakini zikaondolewa na

Usalama wa Taifa, hali iliyojenga mazingira ya kupigiwa debe kwa nguvu kwa hoja ya kutaka Katiba iandikwe upya.
Kwa hali hiyo kila kundi limepata fursa ya kulazimisha – si kutoa maoni kama wengi wanavyoendelea kuota – kupata

Katiba wanayoitaka, hali inayoonyesha mashaka, kwani siyo Wazanzibari tu walio na nia ya kulazimisha Katiba wanayoitaka.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
Back
Top Bottom