Michelle Obama amtambua mbunifu kutoka Kenya

Muria

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
281
181
160617081222__obama_michelle_624x351_bbc_nocredit.jpg

Mkewe rais wa Marekani Michelle Obama amemsifu mjasiria mali kutoka Kenya mwanzilishi wa kampuni inayotengeza biadhaa za watoto bi Wanjiru Waithaka Waweru.

Katika dhifa ya jioni iliyoandaliwa kwa heshma ya wanawake bi Wanjiru Waithaka Waweru, ambaye ni mhandisi/Msanifu mijengo ambaye amegusa maisha ya wengi kwa njia yake ya kipekee ya ubunifu wake unaozingatia maslahi ya watoto.

Shirika lake la FunKidz, lilitajwa kama moja ya kupigiwa mfano na kuigwa kote duniani.

Funkidz ilikuwa moja kati ya mashirika yanayongozwa na wanawake 10,000 kutoka Afrika Mashariki, mataifa ya Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika yanayotambuliwa na Goldman Sachswhich kwa mchango wao.

Japo Bi Obama alikuwa ni mifano mingi tu ya kusimulia faida ya mikopo kwa wanawake inayotolewa na Goldman Sachs chini ya mpango maalum wa ''10000 Women'' bi Obama alichagua kusimulia kisa cha Wanjiru Waweru ambaye ubunifu wake wa kuunda bidhaa zinazozingatia hadhi ya mtoto mwafrika ni wa kuigwa.

Chanzo: Mkewe Obama amtambua mbunifu kutoka Kenya - BBC Swahili
 
Habari inamhusu bi wanjiru na ubunifu wake wewe unatuwekea picha ya mke wa obama.Hukupata picha ya wanjiru?Huo ubunifu unahusu nini hasa? (in detail)
Hii habari umeirashiarashia mno!
 
Habari inamhusu bi wanjiru na ubunifu wake wewe unatuwekea picha ya mke wa obama.Hukupata picha ya wanjiru?Huo ubunifu unahusu nini hasa? (in detail)
Hii habari umeirashiarashia mno!

Binafsi nimejiuliza hilo swali pia, ilifaa picha ziwekwe za ubunifu wenyewe na mbunifu. Japo nimejifunza msamiati "Msanifu mijengo"

Hongera zake mbunifu huyo ambaye ni mhandisi/Msanifu mijengo
 
Back
Top Bottom