This is not good kwa wazazi wako na walezi wako. ni sawa na vijana wengi wanaokoka na wanawakataa wazazi wao.
Kwa umri wako na kwamba umemaliza chuo, ungepaswa kuji establish na kutafuta links mbalimbali kama vijana wengi wanavyofanya na si kutegemea wazazi wetu "masikini" 100% mnakuwa na mvutano usio na sababu na hata wazazi wanaona shule haijakusaidia.
unaweza kupinga michango ya harusi na graduation lakini kwa namna nyingine (it is a social issue, very complicated) si rahisi kama unavyofikiria. uliza wanaosoma social antropology au masomo mengine ya social.
you seem anti-social. next time ukiona mnatofautiana sana na wenzio sometimes unakuwa flexible
Kwani kuvaa joho kulihitaji hizo milioni? Kwa nini usingeenda kujumuika na wenzako chuoni (ambayo haihitaji hela) and then ukaendelea na msimamo wako wa kususia sherehe? Ni sawa na bwana harusi asusie ndoa kanisani, akidhani atakuwa amesevu gharama, kumbe angeweza kuhudhuria kanisani na kufunga ndoa halafu asiingie ukumbini kwenye sherehe, sasa wewe ni sawa na kusema hukufunga ndoa na hukuhudhuria sherehe eti kisa unaweza kuishi tu na mkeo/mmeo bila wasi wasi !!Ni kweli, ingawaje nina elimu ya chuo kikuu lakini sijawahi kuvaa joho!! Hata hivyo, hadi leo sijajutia uamuzi wangu!!!!
Hapa mimi sikupongezi hata kidogo!
Wewe mkuu unaonesha ni mkatili na huambiliki. Hivi umewezaje kuwakatili wazazi wako, ndugu jamaa na marafiki waliotaka kusherehekea mafanikio yako? Unachoshindwa kuelewa ni kuwa hiyo pesa waliyochanga ni yao, na hivyo huna mamlaka nayo. Narejea tena kusema ulichofanya si sahihi.
Next time usirudie huo mchezo
Nakuelewa mkuu.
Tatizo linakuja kwamba watu huwa tunaangalia tu monetary value, rather cost, ya sherehe. Hatuangalii factors nyingine. Tuna zi-ignore, kitu ambacho si kizuri.
Sasa angalia kama huyu mdau, hakufikiria kabisa hisia za wazazi wake waliomtangulia kuliona jua. Wametaabika kumlea na kumsomesha, sasa roho zimetulia walau wanaona kijana amepevuka na mbali zaidi amepata cheti au shahada juu. Wanataka walau washerehekee mafanikio yake ambayo pia ni yao, ili kujituliza na kujipongeza.. lakini kijana anawakatili..hii si kadhia ya kuifagilia..!
Ile thread iliyozungumzia michango ya harusi sijui (ya bwana harusi kuomba apewe kodi ya miezi sita) sijui imepotelea wapi!! Hat hivyo, thread hii imenikumbusha jambo linalofanana na hilo!! Nilipomaliza chuo, nilikaa mtaani karibu miezi tisa bila hata angalau ya tempo!! By the way, my first option ilikuwa ni kujiajiri mwenyewe, but i'd no capital! Wazazi nikawaomba angalau milioni moja (it was 2003) nianze na kabiashara, wakanitolea nje! Miezi 5 baada ya kumaliza chuo, kukawa na graduation ambapo family wakapanga budget ya sh. 1.5 m kwa ajili ya sherehe!!!! But still, muda huo nilikuwa mtaani!! Nikawaambia ni kwanini basi hizo pesa wasinipe mimi nianzishe biashara, hata kama ni ya kufuata mchele mkoa!! Wakanichomolea!! Hata nilipowaambia kwamba sioni maana ya mimi kuserebuka usiku halafu asubuhi naamkia mkunguni( hapa ndo kilikuwa kijiwe chetu majanki!) bado sikueleweka!!! Nami kuonesha kwamba hicho kitu hakikuwa muhimu sana kwangu as compared to my propasal, nikasusia sherehe za graduation!!! Mama yangu alinikasirikia karibu miezi miwili, lakini sikujali!!! Ni kweli, ingawaje nina elimu ya chuo kikuu lakini sijawahi kuvaa joho!! Hata hivyo, hadi leo sijajutia uamuzi wangu!!!!
Sasa Kususa Kwako kulikufanya ukose yote! Mtaji ulikosa, sherehe hukufanya (ukainyima raha nafsi yako) na pia uliwakosea wazazi kwa kutowasikiliza.