Michango mashuleni: Waalimu wakaidi agizo la Waziri...............

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
Walimu Iringa wakaidi agizo la waziri


na Francis Godwin, Iringa


amka2.gif
WALIMU wa shule za msingi katika Manispaa ya Iringa wameonyesha kukiuka maagizo ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi yaliyotolewa na Naibu Waziri wake, Philipo Malugu, kuhusu agizo la wizara hiyo la kupiga marufuku michango kwa watoto wanaosoma elimu ya msingi baada ya walimu hao kudai kuwa wizara hiyo ilitoa agizo hilo kisiasa bila kujua sababu za uwepo wa michango hiyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti walimu hao walidai michango hiyo ilikuwepo hata kabla ya baraza jipya la mawaziri kuundwa, hivyo kupinga michango hiyo ni sawa na kuzuia jambo ambalo wizara hiyo halilijui.
Baadhi ya walimu wa shule za msingi mjini hapa ambao hata hivyo hawakupenda kutaja majina yao kwa madai kuwa wao si wasemaji wa Ofisi ya Elimu Wilaya ya Iringa, walisema wizara hiyo imekuwa ikitoa maagizo ya mdomo yasiyo na waraka wowote na kuwa wao hawawezi kusitisha michango hiyo hadi watakapopewa mwongozo wa kuendesha shule hizo.
Kuhusu wingi wa michango isiyo na risiti katika shule mbali mbali za manispaa hiyo, walimu hao walisema michango hiyo inatambuliwa hata na ofisi ya afisa elimu mkoa na ndiyo sababu ya wao kuendelea kuwafukuza wanafunzi wasiochangia.
Walitaja michango hiyo kuwa ni pamoja na michango ya mitihani, karatasi, walinzi, maji, umeme, posho kwa walimu na michango mingine ambayo ni fedha za ukarabati wa majengo ya shule na ununuzi wa madawati katika shule hizo.
Michango hiyo imeendelea kuwa kero kubwa kwa wazazi mjini Iringa ambao baadhi yao wamedai kuwa sehemu ya michago hiyo kama shule ya msingi Ipogolo wamekuwa wakimsaidia mkuu wa shule hiyo kutengeneza gari lake la kusambaza nyama mjini Iringa .
Hivyo walimwomba Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA) kusaidia kutatua kero hiyo ya michango kwa wazazi wanaosomesha watoto wao katika shule za msingi na kuiomba serikali kurudisha ada kuliko michango hiyo holela.
Kwa upande wake Msigwa alisema haungi mkono uwepo wa michango hiyo na kwamba atahakikisha wanananchi wanakutana na kamati za shule na kuhoji juu ya michango hiyo na kuimaliza kero hiyo.
Naye mbunge wa viti maalumu Ritta Kabati (CCM) alitoa kauli ya kupiga marufuku wazazi kuendelea kuchangia michango hiyo isiyo na risiti na kwamba kinachofanywa na walimu hao ni wizi mtupu.
 
Kwa upande wake Msigwa alisema haungi mkono uwepo wa michango hiyo na kwamba atahakikisha wanananchi wanakutana na kamati za shule na kuhoji juu ya michango hiyo na kuimaliza kero hiyo.
Naye mbunge wa viti maalumu Ritta Kabati (CCM) alitoa kauli ya kupiga marufuku wazazi kuendelea kuchangia michango hiyo isiyo na risiti na kwamba kinachofanywa na walimu hao ni wizi mtupu.

Wasishangae wizi unaanzia Ikulu na unateremka kila mahali.......................
 
Back
Top Bottom