Miayo

Washawasha

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
16,638
13,052
Habari zenu madk bingwa,nilikuwa naomba kufahamishwa,hivi ni kwann binadamu tunapiga miayo na je? wanyama wengine nao hupiga miayo
 
Kwa nini tunapiga miayo ? sina jibu la kitaalam; subiri utajibiwa...
Wanyama kupiga miayo ? ndio wanapiga, wewe chunguza mwenyewe ....paka, mbwa hasa pale wanapokua katika hali ya uchovu, usingizi au njaa.
 
Kwa nini tunapiga miayo ? sina jibu la kitaalam; subiri utajibiwa...
Wanyama kupiga miayo ? ndio wanapiga, wewe chunguza mwenyewe ....paka, mbwa hasa pale wanapokua katika hali ya uchovu, usingizi au njaa.
Nashukuru,nitafanya uchunguzi huo
 
Yaani nilivyoisoma tu hii Thread miayo imenijia mfululizo..
Nadhani uchovu pamoja na kuwa na usingizi ni miongoni mwa sababu..
Lakini kuna mazoea ya mtu kupiga mwayo pale anapoona mwenzake amepiga, sijui huwa inakuwaje hapo....
Wataalamu hebu tupeni majibu ya kitaalamu tafwadhali....
 
Habari zenu madk bingwa,nilikuwa naomba kufahamishwa,hivi ni kwann binadamu tunapiga miayo na je? wanyama wengine nao hupiga miayo
Kupiga miayo, kunahusishwa sana na uchovu, stress, overwork, lack of stimulation, and boredom. Tafiti chache zimefanywa kuhusiana na sababu ya upigaji miayo...!


  • Tafiti zilizofanywa za kiadhari kwenye fizioloji, wanasema kuwa upigaji miayo kunasababishwa na upungufu wa hewa ya oksijeni kwenye damu. Kuna watafiti wengine wanalipinga ili, kwani wao wansema kuwa upigaji wa miayo kunapunguza uchukuwaji wa hewa ya oksijeni mwilini ukilinganisha na upumuwaji wa kawaida.

  • Wale wenye kuunga mkono nadharia ya mageuzi ya kimaumbo, Evolution Theory, wao wanasema kuwa upigaji miayo ni urithi kutoka kwa mababu zetu wa kale (ancestors), ambao walikuwa na tabia ya kukenua vinywa vyao na kuonyesha meno yao ili kuwatisha wengine, kwa ufupi hapa, wanajaribu kutufahamisha kuwa upigaji wa miayo ni urithi tu, kutoka binadamu wa kale.

  • Pia kuna wale wenye kuamini nadhalia ya uchovu: Hawa wanasema kuwa upigaji wa miayo kunasababishwa na uchovu au utepetevu. Ni kawaida kupiga miayo kama tunaonyesha dalili ya uchovu au usingizi, lakini nadhalia hii haielezi kwanini wanariadha wengi upiga miayo kabla ya kuanza mashindano.

Tafiti bado zinaendelea....!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom