Mianaume ndo tulivyo......hovyoooo!

Leo humu ni balaa
Wanaume tumevamiwa
yaani wamepata pa kushika

Wala hamjavamiwa kipenzi ndio jinsi mlivyo haswaaaa wala hajakosea tena kuna mengi tu yameachwa mimi nikiongezea yana nikumbusha machungu tu.
Na nyie wanaume mnaojisifia kuwa mnapenda sana familia zenu ndio wakuogopwa mno,mnapenda kujitutumua mbele za watu wakati ni uongo mtupu!!!!
 
Hahahaaa yaani natamani ningetengeneza bango kabisa halafu nilibandike sehemu kila mwanaume anaepita alisome. Kwa kuongezea
16. Unarudi nyumbani saa tisa usiku halafu hutaki kufunguliwa gate na mtu yoyote zaidi ya mkeo na kwa masharti kuwa ukishaingiza gari ndani mkeo afunge gate na hakuna kuingia ndani mpaka wewe ushuke kwa gari muingie wote. Wakati huo unakua ndani ya gari unamalizia kuongea na simu(ambayo kwa vyovyote vile itakua unamwambia hawara nimefika salama).
Kuna watu mnaweza kudhani hii ni utani lakini hii ilinikuta mwenyewe wala sijasimuliwa mie.

nina uhakika sio mimi hapo
Pole sana my wife
 
Ni kweli Mkuu, hata mimi nakuunga mkono kwamba hayo yanatokea katika baadhi ya familia. Kwa jinsi ulivyoandika inaonekana kuwa ni wanaume wote wana tabia hizo. Rejea kicha cha habari.....Mianaume ndivyo tulivyo..........Kwa jinsi ulivyoandika, inawavunja moyo hata wale ambao hawana hizo tabia. Aidha, tubaliane kwamba wanaume kama binadamu wamezaliwa na kulelewa katika mazingira na hali toufuti tofauti, na kwa kawaida binadamu anabadilishwa na aina ya malezi na mazingira aliyokulia kwa maana hiyo hawawezi kufanana wote. .....Kama ungesema baadhi ya wanaume, ningeunga mkono hoja 100%........
masikhara tuyaweke kando,hivi kuna binadamu ambaye ni perfect humu duniani?
hii mada mi naona tuichukulie positively,isaidie kutu provoke tujiangalie mara mbili mbili,penye matatizo turekebishe,palipo sawa tupaimarishe.
 
Wala hamjavamiwa kipenzi ndio jinsi mlivyo haswaaaa wala hajakosea tena kuna mengi tu yameachwa mimi nikiongezea yana nikumbusha machungu tu.
Na nyie wanaume mnaojisifia kuwa mnapenda sana familia zenu ndio wakuogopwa mno,mnapenda kujitutumua mbele za watu wakati ni uongo mtupu!!!!

Sidhani kama kuna kujisifia
Kuna kujisifia hata kwenye maandishi ukisoma between the line unajua kabisa kuwa huyu anadanganya na haya anayoyasema hayafanyi huko kwake
Ila kwa kweli to me my family is everything na niko tayari kufanya lolote kwa ajili ya familia yangu
naitetea na naipenda kwa kuwa ni part ya maisha yangu na yote ninayofanya kama sitaipa raha familia yangu ni kazi bure
 
mwanaume fulani ivi mwenye tabia nyingi ulizoziorodhesha
yaani umemgusa kabisa
kudadadeki....print umpelekee huko huko aliko,mwambie kuna baba mmoja anaitwa Bishanga Abashaija kanipa nikuletee,and then check his reaction akishasoma.
 
masikhara tuyaweke kando,hivi kuna binadamu ambaye ni perfect humu duniani?
hii mada mi naona tuichukulie positively,isaidie kutu provoke tujiangalie mara mbili mbili,penye matatizi turekebishe,palipo sawa tupaimarishe.

Wise say mkuu na huu ni ukweli maana najua na naamini hakuna hata mmoja ambaye ni perfect
Ila hii thread isaidie kutubadilisha na kuyaangalia ni yapi tunafanya ambayo kwa wake zetu na familia zetu yanawakwaza
na ni wapi tumerudi nyuma katika kuheshimu na kuziona ndoa zetu za maana na kuwaona kama wake zetu ni watumwa wetu au watu wasio na hisia
Au ule ukuu wa familia tumeutumia isivyo kwa kuwa zaidi dictator zaidi ya baba
 
Sidhani kama kuna kujisifia
Kuna kujisifia hata kwenye maandishi ukisoma between the line unajua kabisa kuwa huyu anadanganya na haya anayoyasema hayafanyi huko kwake
Ila kwa kweli to me my family is everything na niko tayari kufanya lolote kwa ajili ya familia yangu
naitetea na naipenda kwa kuwa ni part ya maisha yangu na yote ninayofanya kama sitaipa raha familia yangu ni kazi bure

Good....Na Mwenyezi Mungu akuzidishie mapenzi ya kweli na uendelee kuijali familia yako.
 
Hahahaaa yaani natamani ningetengeneza bango kabisa halafu nilibandike sehemu kila mwanaume anaepita alisome. Kwa kuongezea
16. Unarudi nyumbani saa tisa usiku halafu hutaki kufunguliwa gate na mtu yoyote zaidi ya mkeo na kwa masharti kuwa ukishaingiza gari ndani mkeo afunge gate na hakuna kuingia ndani mpaka wewe ushuke kwa gari muingie wote. Wakati huo unakua ndani ya gari unamalizia kuongea na simu(ambayo kwa vyovyote vile itakua unamwambia hawara nimefika salama).
Kuna watu mnaweza kudhani hii ni utani lakini hii ilinikuta mwenyewe wala sijasimuliwa mie.
Mama Tuli,mbona haya tunayaona kila siku? mbona kuna wanaume anadiriki hata kuingia ndani na hawara yake na anamwambia mke ampikie,jamani watu wengine ubishi tu,yanatokea haya.
 
Yani nataman baba yangu mtambuzi asome huu uwi nione atasemaje maana yy kakomaa na sie tu!
Yani leo sibaduki hapa kwa hii faraja ninaipata ya kusoma koment za hawa jamaa!
Asante sana bishanga na sie leo tupumzike lol!
Mbona raha leo!
kwa raha zenu,acha kina Aspirin wavimbe wapasuke.
 
namuona rocky ndio anaongea ongea. Wapi wanaume wengine?

Asilimia kubwa wanaogopa maana humu tumekuwa tukiwalalamikia wake zetu kuwa ndio chanzo cha matatizo yote
Sasa leo kuwekewa thread ya makosa tunayoyafanya kama wanaume ndani ya familia zetu inakuwa ni ngumu kumeza
 
hapo kwenye na 8 mtoto akiumwa anaita mama kayai angalia mwanao anaumwa kidogo anadeka lakini akiumwa yeye balaa nyumba haikaliki mtakimbiza ndani hapo hapatoshi
Bishanga asante kwa thread........wasomaji mapovu yanawatoka
ndo uzuri wa jf,mwenye kutaka kujifunza ili aimprove mahusiano yake itamsaidia,atakayeamua kuvimba na kuwa defensive itakula kwake.
 
Back
Top Bottom