Miaka Mitatu sina Mtoto

Pole. Pamoja na ushauri wote ulioupata nakushauri pia uende kanisani uombewe. You never know, may be God has allowed it for a reason. Usikate tamaa, kuna watu walipata watoto baada ya muda mrefu wa ndoa. Miaka 3 mbona kidogo aiseee. Kwenda nje ya ndoa kutakuletea majuto ya milele mpaka siku unaenda kaburini. VIPI KAMA MKEO NAE AKISEMA ATOKE NJE YA NDOA ILI APATE MTOTO? Hiyo ndoa itabaki salama.
unaweza toka nje ya ndoa na bado usipate mtoto na hata akipatikana utajuaje ni wa kwako maana ni nje ya ndoa...
 
Kaka pole kwa kusubiri bila kupata mtoto. Mimi nilikuwa na tatizo kama lako. Mimi na wife wangu tulikaa miaka minne bila mtoto. Tulienda hospitali ya TMS Kariakoo na kufanya vipimo vyote, tukapewa dawa mbalimbali zikiwemo za kufungua mirija ya uzazi na kurutubisha mbegu, baada ya muda tulifanikiwa kupata mtoto. Kwa sasa tuna watoto wawili.
 
Kwa imani yote yanawezekana bado una muda mzuri tu wa kupata mtoto.mungu ni mwema
 
Pole bwn Ramos.

Nakushauri usianze kutafuta mtoto nje ya ndoa kama kwamba ndiyo jawabu pekee. Kwanza kabisa muende Hospitali mkapime mjue tatizo ni nini na analo nani. Mkishamaliza hilo ndo ufikirie njia zingine. Maana unaweza kutoka nje ya ndoa still usizae, na wengine (wanaume) wamediriki kuacha wake zao ikajabainika kuwa tatizo ni wao.

Fanyeni vipimo vyote vinavyotakiwa.
 
Pole ndugu yetu,
Kuna kamchezo siku hizi watu wanatest kwanza siku ya harusi unakuta bibi harusi kavimba, hapo hapo tunajua mdau alikuwa anatest ishu kama productive hapo inabidi uvumilie tu linaweza kuwa tatizo kwako alafu mkeo akajaribiwa nje ikawa noma. Mfarijiane tu.
 
...mie niliwahi kuuliza hapa,sijaolewa na ninajijua sina uwezo wa kuzaa mtoto..je ndoa niseme ndio basi??...ama why do we get married????

...BTT:ukitoka nje ya ndoa,ukakuta tatizo ni lako utafanya nini???

...kuna watoto kibao,wanahitaji 'homes' suala la kuadopt tusiliache kuwa ni la wazungu na culture yao!
 
Hivi wajameni MILA ZETU zinasemaje kwenye hali kama hii? Mi namshauri akawaconsult wazee nyumbani watampa mawili matatu.

Lakini pia miaka mitatu sio mingi ya kuanza kuingiwa na wasi wasi ijapokuwa katika hali ya kawaida angekuwa na mtoto au watoto sasa hivi...sema ndo hivo hatulingani ndugu
 
Pole ndugu yetu,
Kuna kamchezo siku hizi watu wanatest kwanza siku ya harusi unakuta bibi harusi kavimba, hapo hapo tunajua mdau alikuwa anatest ishu kama productive hapo inabidi uvumilie tu linaweza kuwa tatizo kwako alafu mkeo akajaribiwa nje ikawa noma. Mfarijiane tu.
Daah, sasa ndo umeamua kumwaga mchele hapa !? Halafu ile thread kuhusu yule binti wa SAUT nimeona kwenye newspaper moja la udaku, sasa sijui walikuomba ruhusa kuchapisha habari yako au la!!
 
Karibu JF, Naomba usiogope katika hilo ambalo wewe unafikiria kuwa tatizo, Si tatizo kubwa sana, Miaka mitatu ni midogo, Officemate wangu yeye amekaa na mke kwa miaka 10 Bila mtoto, sasa hivi wana mtoto wa miezi 5 . Uvumilivu na maombi ni silaha kubwa, lakini kuna mambo mengi yanaweza changia, Kupima Afya ni Muhimu lakini Pia kuna mambo mengine yasiyousiana na Afya,Kama Mambo ya kimila , Kurogwa, Mapepo n.k., Hayo mambo mengine hatuyawezi katika hali ya kibinadamu, Silaha yetu ni Maombi. Nina shuhuda nyingi za watu ambao walikaa bila watoto kwa siku nyingi na tumewafanyia maombi na wana watoto, shuhuda ni nyingi sana. Mara nyingi mapepo yanakaa katika matumbo ya uzazi kwa wakina mama na kuzuia mimba. Na kwa wanawake wengine majini maaba ni tatizo pia, huzuia sana wakina mama kutunga mimba.
 
... Pole sana - Hii hali huwa ni mtihani mkubwa na inahitaji uvumilivu wa kupita kiasi
Pole ndugu...sina ushauri ila nitawaweka mikononi mwa Mungu na Mungu atawasaidia!
Pole sana ndugu yangu;
Pole sana mkuu...
Ramos, pole sana kwa hii hali.
Pole sana Ramos, ...
Pole ndugu yetu,...
Hivi wale washauri nasaha huwa wanatoa pole kwa mshauriwa?
 
Ndugu yetu Ramos; karibu sana JF siongezi chochote zaidi ya kuwashukuru wenzangu waliokupa ushauri hapa! JF ni kisima cha UPENDO; Msiba wako ni wetu pia na Furaha yako ni yetu pia!

Mungu akubariki!
 
...kuna watoto kibao,wanahitaji 'homes' suala la kuadopt tusiliache kuwa ni la wazungu na culture yao!

Wala suala la kua adopt si la wazungu peke; labda wao walifanyia marekebisho na kuliwekea sheria

Huko Mara walikuwa nazo na bado wanazo ziitwazo NYUMBA NDOBU! Ni form mojawapo ya kuadopt ukiacha hizi za kulelea watoto wa ndugu ambazo ni very common huko kwetu!
 
Hi wanaJF
Mimi ni mwanaume, nimeoa miaka mitatu iliyopita. Kwa sasa nina miaka 32 ya umri. Mimi na mke wangu hatuna mtoto kwa miaka hiyo mitatu. Tatizo ni kuwa siku hizi nimeanza kuingiwa na kaushawishi ka kutafuta mtoto nje ya ndoa. Najua ni hatari kiafya lakini najishawishi kuwa nitafanya taratibu zote za kuwa mwangalifu. Siku zote kila ninapowaza hilo la kwenda nje ya ndoa nakumbuka siku ile pale kanisani nilipoahidi mbele ya mashahidi, mbele ya padre na mbele ya mungu kumpenda na kumlinda mke wangu katika SHIDA na raha. Kinachonishangaza ni kuwa hiyo consiousness siku hizi inapungua, nazidiwa na ushawishi. Nikisikia rafiki zangu wakiongelea watoto wao, nikisikia stori kuwa kuna watu hawakuwa na watoto kwenye ndoa, wakajawapata nje, na nikiwaza kuwa nina kazi nzuri kidogo itakayonofanya pengine niwe na raslimali zitakazohitaji kurithishwa baadae najihisi kama nitashawishika. Jingine kubwa ni kuwa mke wangu nae ni mkubwa kidogo (miaka 31) na siku zinakwenda.

Tulishachukua hatua ya kucheki kama tuna matatizo kiafya, lakini sote hatukuonekana kuwa na matatizo, ingawa ni katika vipimo vile vya kawaida hospitali zetu ziliweza kuhandle (najua kuna vipimo complex nje ya nchi ambavyo uchumi hauturuhusu kuvipata). mi na mke wangu tunaheshimiana sana, tunapendana sana lakini naogopa na sijawahi kuonyesha hali yoyote kwake kuwa nawaza kutafuta mtoto nje.

WanaJf naombeni ushauri wenu...

mie ni bachela ila Nina mfano hai wa mama aliyepata kichanga akiwa na miaka 54(na baada ya mateso na manyanyaso makubwa toka kwa ndugu wa mumewe)...!! maumivu yako ni maradufu kwa mkeo...!! chukueni likizo..nenda kwa wataalam wa nasaha za ndoa..kuleni vizuri..muombeni mungu...MTAFANIKIWA!!
 
Ndugu Ramos jaribu ya fuatayo

(i) Ongea na mwenza wako hilo hitaji la kupata mtoto
(ii) mjadiri kwa pamoja jinsi mzunguko wa siku zake unavyokwenda (kawaida mzunguko huanza kuhesabiwa siku ya kwanza ya bleed na kwa wanawake ambao mzunguko wao ni siku 28 siku ya kuanza kutafuta mtoto ni siku 5 kabla ya ovulation na siku 1 au 2 baada ya ovulation)
(iii) ukisha uelewa mzunguko wake na tumai utakuwa unaelewa ni siku gani hasa ambazo mkikutana mtoto anaweza kupatikana
(iv) anza maandalizi kwa kula vyakula vinavyoongeza sperm count kama karanga mbichi au zilizokauka unaziloweka kwenye maji kwa masaa halafu unazitafuna kama karanga mbichi
(iv) Kwa upande wa mwenza wako mnaweza kupima Ph level na kama iko juu aweza kuanza kula vyakula vya kuishusha ili iwe katika viwango vinavyokubalika (maana ikizidi uua sperms kabla hazijalifikia yai)
(v) siku za kutafuta mtoto hakikisha umetengeneza mazingira mazuri kisaikologia kwako na kwa mwenza wako na hakikisha kila mmoja wenu ana afya njema kwa ajili ya tendo hilo. Fanya tendo la ndoa kwa kiasi kila siku katika siku za kutafuta mtoto. Na kwambia hakika mwenzi unaofuata dalili za ujauzito mtaanza kuziona

Natumai ukifuata masharti haya utafanikiwa kama hakuna tatizo lolote. Huna haja ya kwenda nje ya ndoa.
 
Everything is God's plan na lazima aseme ndio, every thing happens in God's time - lkn tatizo sisi kama binadamu huwa tunaona it must be on our plans and time. Wewe na mke wako muendelee kusali na Mungu anamajibu 3 ndio, hapana na subiri. He always knows the right answer for all of us.
 
Hi wanaJF
Mimi ni mwanaume, nimeoa miaka mitatu iliyopita. Kwa sasa nina miaka 32 ya umri. Mimi na mke wangu hatuna mtoto kwa miaka hiyo mitatu. Tatizo ni kuwa siku hizi nimeanza kuingiwa na kaushawishi ka kutafuta mtoto nje ya ndoa. Najua ni hatari kiafya lakini najishawishi kuwa nitafanya taratibu zote za kuwa mwangalifu. Siku zote kila ninapowaza hilo la kwenda nje ya ndoa nakumbuka siku ile pale kanisani nilipoahidi mbele ya mashahidi, mbele ya padre na mbele ya mungu kumpenda na kumlinda mke wangu katika SHIDA na raha. Kinachonishangaza ni kuwa hiyo consiousness siku hizi inapungua, nazidiwa na ushawishi. Nikisikia rafiki zangu wakiongelea watoto wao, nikisikia stori kuwa kuna watu hawakuwa na watoto kwenye ndoa, wakajawapata nje, na nikiwaza kuwa nina kazi nzuri kidogo itakayonofanya pengine niwe na raslimali zitakazohitaji kurithishwa baadae najihisi kama nitashawishika. Jingine kubwa ni kuwa mke wangu nae ni mkubwa kidogo (miaka 31) na siku zinakwenda.

Tulishachukua hatua ya kucheki kama tuna matatizo kiafya, lakini sote hatukuonekana kuwa na matatizo, ingawa ni katika vipimo vile vya kawaida hospitali zetu ziliweza kuhandle (najua kuna vipimo complex nje ya nchi ambavyo uchumi hauturuhusu kuvipata). mi na mke wangu tunaheshimiana sana, tunapendana sana lakini naogopa na sijawahi kuonyesha hali yoyote kwake kuwa nawaza kutafuta mtoto nje.

WanaJf naombeni ushauri wenu...

pole sana jamaa, tafadhali naomba uniPM (uniandikie Private Msg), kuna maswali ya papo kwa papo nataka kukuuliza and then ntajitahidi nikupe ushauri ambao umewasaidia wengi, na nina uhakika mtafanikiwa kupata mtoto, if and only if mlishawahi kwenda kuchekiwa na kuambiwa wote mko mswano
 
Utawasaidia wengi sana kama utaweka hapa; Na hili jambo muhusika keshaliweka wazi kwanini unataka kwenda mafichoni?
 
Back
Top Bottom