Miaka Mitatu Jela Kwa Kumlawiti Farasi wa Jirani Yake

Dr. Chapa Kiuno

JF-Expert Member
Sep 11, 2009
443
18
</SPAN>


Rodell Vereen

Mwanaume nchini Marekani ambaye alikuwa na tabia ya kumlawiti farasi wa jirani yake amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu.


Rodell Vereen wa South Carolina nchini Marekani amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu baada ya kukamatwa live akimwingilia farasi kinyume cha maumbile yake.

Vereen alionekana live akifanya kitendo hicho katika video za kamera za ulinzi zilizotegeshwa na mmiliki wa farasi hiyo baada ya farasi wake mwenye umri wa miaka 21 kuanza kuonyesha tabia za ajabu ajabu.

Mmiliki wa farasi huyo, bibi Barbara Kenley, alisema kwamba alianza kushuku kuna kitu kinaendelea baada ya farasi wake kuanza kuonyesha tabia zisizoeleweka na kuanza kupata maambukizi ya magonjwa mbalimbali.

Baada ya kutegesha video kamera za ulinzi, bibi Kenley alifanikiwa kumnasa mtu anayemharibu farasi wake na kumweka chini ya ulinzi wa mtutu wa bunduki mpaka polisi walipofika.

Mwaka 2007, bibi Kenley aliwahi kumkuta Vereen akiwa amelala pembeni ya farasi wake mmoja. Alikiri kosa lake na alipewa onyo.

Mbali na kutupwa jela miaka mitatu, Vereen ametakiwa kukaa mbali na wanyama na atapatiwa matibabu ya tabia hiyo akitoka jela.



Source: News Agencies
 
Back
Top Bottom