Miaka kumi ya Ndoa kwa Amani na Historia nzuri....

Nashukuru Mungu mwaka huu ninatimiza miaka kumi toka kufunga ndoa na mke wangu mpendwa..Mwenyezi Mungu ametujalia kupata watoto wawili mpaka sasa..Tunawapenda na wanatupenda sana! Licha ya tofauti za hapa na pale,lakini nimekuwa na wakati mzuri ktk maisha ya ndoa;sijawa mkamilifu kwa asilimia zote,mara kadhaa nimedondoka na kuinuka...nilijitahidi, kudondoka kwangu kusiwe kikwazo ktk uhai na afya ya familia yangu!Hakika ktk hili nimekuwa muangalifu sana,mana natambua familia kwa maana ya mama watoto na watoto wananihitaji sana.... Mara ya kwanza kukutana na mama watoto wangu ni kama utani..ilikuwa mwaka 1992,wakati huo nikiwa kidato cha tano Tabora School,yeye akiwa kidato cha tatu Tabora Girls...sikuwa mjuzi wa kumwaga sumu kwa wadada,hii ni kutokana na malezi na exposure ya maisha yangu ya nyuma!nilisoma Seminary kwa miaka 5,sikuwahi kuwa karibu na viumbe hivi....nilipomaliza Form 4 nilichaguliwa Tabora Wavulana..enzi za jeshi la Afande Chacha. Kwa mara ya kwanza naingia ktk dunia mchanganyiko,nimefika nakutana na Disco la karibisha FormV...sijui nicheze vipi,nifanyaje na nani wa kucheza nae,kwangu ulimwengu wa disco ni msamiati mpya,tena disco la mchanganyiko?kila aliyekuwepo ktk darasa langu ana "partiner" wake;nilijikakamua kwa soni na woga kumuomba dada mmoja nicheze nae.....Oooops kumbe that was my real wife,a today's mother of my children!!Tukaendelea kila disco tunacheza wote,mikusanyiko ya dini na mengine tukawa pamoja..badae nkamaliza na kupanda gari Moshi kurudi kwetu,tukabaki kukumbukana kwa waraka wa barua(mana simu hazikuwepo)....hali hii ilikwenda miaka miwili(mana yeye advance alipelekwa Weruweru Girls)...hatimaye nikamaliza chuo na kupata kazi...nilimsubilia nae amalize adi chuo kikuu...then tukajipanga kwa miaka kadhaa..hatimae 2002 tulikata shauri na kuwa mwili mmoja!Namshukuru Mungu this was my first woman that made me to knw the world of love...and real i was the first to her!japo baadae wapo waliopandia Manzeshe wakashuka Magomeni..lakini uyu ndo tuliyetoka nae Ubungu tukiwa na nia ya kufika Posta mwisho wa safari! Namshukuru Mungu amenipa afya njema..nimeshuhudia watoto wangu wakikua na kuanza shule....Halaa to my clasmate at Tabora school,Udsm and other Co-Workers....Mungu atupe uzima tuwashuhudie watoto wa watoto wetu na tuwape michapo ya Upendo Wetu....Gracia el Tutti..

Hongera mkuu, ila siku nyingine weka paragraph bana, dah.
 
Back
Top Bottom