Miaka 50 ya uhuru

Lutala

JF-Expert Member
Jun 17, 2010
848
103
Salam ndugu wanaJF,

Nina tambua kuwa maandalizi ya weekend yashapamba moto kwa serious issue ni vigumu kuzijadili.

Kinachonisumbua ni kuona kuwa watanzania wenzangu kukosa ule uthamini kwa taifa lao.

Mwaka huu nchi yetu inatimiza miaka 50 lakini mpaka sasa sijaona jitihada za kuhamasishana na kujitambia utaifa wetu. Najua viongozi wanaogopa kuzungumzia miaka 50 kwa kuwa mnajua hawana mpya sana sana wananchi wataanza kuwadai waonyeshe waliyoifanyia nchi kwa kipindi chote.

Ukiangalia mataifa mbalimbali kutimiza miaka 50 ni kitu kikubwa sana na kwa kawaida maandalizi yanatakiwa kuanza mapema ili kuweza kupata vitu vinavyoweza kuweka kumbukumbu kwa kizazi kijacho.

Vitu hivyo vinaweza kuwa nyimbo, majengo na hata majina ya watoto kuweza kutunza kumbukumbu hiyo. Mtakumbuka kuna majina kama "Uhuru, Madaraka, TANU, etc yalikuja kutokana na hamasa zilizokuwepo wakati huo na hasa katika kuthamini utaifa.

MOD naomba uweke thread itakayowezesha wanaJF kuchangia mawazo na busara zao kuhusiana na miaka 50 ya utaifa wetu. Ukumbuke kuwa viongozi kadhaa wanatembelea mtandao huu kila siku kwa hiyo wataweza kujifunza kitu kutoka kwa "great thinkers".

VIVA TANZANIA
 
Watasema nini wakati CHADEMA imewashika pabaya? CCM wanashindwa kujenga hoja za mafanikio ya miaka 50 ya UHURU wa nchi yetu sababu ya kile kinachoitwa kuoneana haya.......Hawana jipya bora waendelee kuwa kimya tu.
 
Mwavilenga upo sahoihi sana kuwa hawa jamaa hawana jipya. je, na sisis wananchi tunasemaje kuhusu miaka 50 ya Uhuru?
 
Salam ndugu wanaJF,

Kinachonisumbua ni kuona kuwa watanzania wenzangu kukosa ule uthamini kwa taifa lao.

Mwaka huu nchi yetu inatimiza miaka 50 lakini mpaka sasa sijaona jitihada za kuhamasishana na kujitambia utaifa wetu. MOD naomba uweke thread itakayowezesha wanaJF kuchangia mawazo na busara zao kuhusiana na miaka 50 ya utaifa wetu. Ukumbuke kuwa viongozi kadhaa wanatembelea mtandao huu kila siku kwa hiyo wataweza kujifunza kitu kutoka kwa "great thinkers".

VIVA TANZANIA

Mkuu.
Unatuchanganya...nchi iitwayo Tanzania ina miaka 47...nchi iitwayo Tanzania bara imezaliwa 1977..nchi ya Tanganyika ambayo ndio inatimiza miaka 50 imefichwa...sasa huu utaifa wa miaka 50 au nchi yetu unakusudia nini?
Kama hatulijui tatizo lenyewe hatuwezi kutatua tatizo hilo.

Wazo lako ni zuri lakini haliko sahihi. Tuidai nchi yetu kwanza.
 
Back
Top Bottom