Miaka 50 ya Uhuru, Tulipata Uhuru Kweli au Tulibadilishiwa Mfumo wa Ukoloni?

LINCOLINMTZA

JF-Expert Member
Mar 15, 2011
1,639
516
Tarehe 9-12-1961, Tanganyika ilipata uhuru kutoka kwa wakoloni, wanyonyaji, mabebapari na jina lolote mbaya waweza kuwaita kwani si watu wema kwa uvamimizi na matendo waliyowatendea dungu zetu wa damu kabisa. Hawa watu walituvamia nchini kwetu na mara nyingi walitumia nguvu ukiachilia mbinu kama za Magungo, zilizopelekea hasara kubwa kwa wananchi ikiwemo kupoteza maisha ya watu wengi kwa vita, biashara ya utumwa, n.k.

Maswali ya kujiuliz:
1) Je, tunasherekea kama washidi zidi ya wakoloni au kwa kupewa uhuru tuliokuwa tumenyangwa?
2)Je, tunayakumbuka maovu waliyowafanyia babu zetu na jinsi gani tunafikiria kuwashitaki au kuwatia adabu hawa wakoloni?
3) Kweli baada ya uhuru, walituacha kuwa huru au walikuja na mbinu mpya za kututawala na kutunyonya maliasili zetu?
4)Sisi tumeweza kuzielewa vizuri hizo mbinu mpya na jinsi ya kupambana nazo?
 
Wa heri wale weupe kuliko hawa CCM wezi, wanyanganyi, wanaotupiga kwa mabomu ya kodi zetu!!!!!
 
Back
Top Bottom