Miaka 50 ya uhuru tanzania tunahitaji katiba mpya sio propaganda

samseuya

New Member
Nov 20, 2011
1
0
Wakubwa,Kusema kweli billa kuingiza itikadi za siasa kwa nchi kama Tanzania ambayo imepata uhuru wa bendera miaka 50 iliyopita hatuwezi kuendelea kufumbia macho upungufu mkubwa uliopo kwenye katiba ya jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977.
Binafsi sioni kwa nini viongozi wetu wanapata kigugumizi kutuongoza kuingia kwenye mchakato wa kupatakatiba mpya sio kwa jina bali kwa maudhui yake.

Kwa maoni yangu mchakato tulioanza sasa hivi hauna nia yoyote ya kutupatia katiba mpya,labda kwa jina tu.
Hivi,hebu tujiulize
  1. tutawezaje kupata katiba yenye matakwa ya watanzania kwa kutumia tume ya Raisi?
  2. tutawezaje kupata katiba mpya wakati mswada wenyewe wa katiba mpya unatuzuia kujadili au kuhoji mambo ambayo yanagusa maisha yetu kila siku kama madara makubwa ya viongozi na muungano wa nchi mbili uliozaa nchi mbili (tunaambiwa 1/2+1/2=2)halafu haturuhusiwi kuhoji ? tunatakiwa kuboresha tu ? hii ni haki kweli?
Mio sio mtaalamu wa sheria lakini pamoja na upofu wangu wa sheria naweza kutilia shaka vifungu vingi vya katiba ya sasa,
sitaki kuamini kwamba walioko kwenye mfumo wa utawala hawayaoni,tena wengi wao ni wasomi waliobobea kwenye taaluma ya sheria.

Aaah,mie sijui bwana,ninyi mtanikosoa kama nakosea.


Wadau angalieni vifungu vifwatavyo halafu nyie wenyewe mtaniambia mnavionaje?


MAKOSA YALIYOPO KWENYE KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Kutangaza
Jamhuri ya
Muungano
Sheria ya 1984
Na.15 ib
1. Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano.

Tangazo la nchi
yenye Mfumo wa
vyama vingi
Sheria ya 1992
Na.4 ib.5
(1) Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na
ya kijamaa, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa.
(2) Mambo yote yahusuyo uandikishaji na uendeshaji
wa vyama vya siasa nchini yatasimamiwa kwa mujibu wa
masharti ya Katiba hii na ya sheria iliyotungwa na Bunge kwa
ajili hiyo

Haki ya kumiliki
mali
Sheria ya 1984
Na.15 ib.6
24.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya sheria za nchi
zinazohusika, kila mtu anayo haki ya kumiliki mali, na haki ya
hifadhi kwa mali yake aliyonayo kwa mujibu wa sheria.


Utekelezaji wakazi na shughuli
za
Rais, n.k Sheria
ya 1984 Na.15
ib.9
Sheria ya 1992
Na.4 ib …
Na.20
ib.12,
Sheria yua
1994 Na.34 ib.6
37.-(1) Mbali na kuzingatia masharti yali yomo katika Katiba
hii, na sheria za Jamhuri ya Muungano katika utendaji wa kazi na
shughuli zake, Rais atakuwa huru na hatalazimika kufuata
ushauri atakaopewa na mtu yeyote, isipokuwa tu pale
anapotakiwa na Katiba hii au na sheria nyingine yoyote kufanya
jambo lolote kulingana na ushauri anaopewa na mtu au mamlaka
yoyote.
Sifa za mtu
kuchaguliwa wa
kuwa Rais
Sheria ya 1992
Na.4
Sheria ya 1994
Na.13 ib…
Sheria ya 1994
Na.34 ib….
Sheria ya 2000
Na.3 ib.7
39.-(1) Mtu hatastahili kuchaguliwa kushika kiti cha Rais wa
Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kama-
(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa
mujibu wa Sheria ya Uraia.
(b) ametimiza umri wa miaka arobaini;
(c) ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na
chama cha siasa;
(d) anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge au Mjumbe
wa Baraza la Wawakilishi,
(e) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya
Uchaguzi Mkuu hajawahi kutiwa hatiani katika
Mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa
kodi yoyote ya Serikali.



Utaratibu wa
uchaguzi wa
Rais Sheria
Na.20 ya 1992
Na.20 ib.5
Sheria Na.34
ya 1994
Na.34 ib.10
41.-(1) Baada ya Bunge kuvunjwa au kukitokea jambo jingine
lolote lililotajwa katika ibara ndogo ya (2) ya ibara ya 38 na
inalazimu uchaguzi wa Rais kufanyika, kila chama cha siasa
kinachopenda kushiriki katika uchaguzi wa Rais kitawasilisha
kwa Tume ya Uchaguzi, kwa mujibu wa sheria, jina la
mwanachama wake mmoja kinayetaka asimame kama mgombea
katika uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na jina la
mwananchama wake mwingine kinayempendekeza kwa nafasi
ya Makamu wa Rais.
(2) Mapendekezo ya majina ya wagombea katika uchaguzi
wa Rais yatawasilishwa kwa Tume ya Uchaguzi katika siku na
saa itakayotajwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge, na
mtu hatakuwa amependekezwa kwa halali isipokuwa tu kama
kupendekezwa kwake kunaungwa mkono na wananchi wapiga
kura kwa idadi na kwa namna itakayotajwa na sheria iliyotungwa
na Bunge.
(3) Endapo inapofika saa na siku iliyotajwa kwa ajili ya
kuwasilisha mapendekezo ya majina ya wagombea, ni mgombea
mmoja tu ambaye anapendekezwa kwa halali, Tume itawasilisha
jina lake kwa wananchi, nao watapiga kura ya kumkubali au
kumkataa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii na ya sheria
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
34
iliyotungwa na Bunge.
(4) Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano utafanywa
siku itakayoteuliwa na Tume ya Uchaguzi kwa mujibu wa Sheria
iliyotungwa na Bunge.
(5) Mambo mengine yote yahusuyo utaratibu wa uchaguzi wa
Rais yatakuwa kama itakavyofafanuliwa katika sheria iliyotungwa
na Bunge kwa ajili hiyo.
(6) Mgombea yeyote wa kiti cha Rais atatangazwa kuwa
amechaguliwa kuwa Rais iwapo tu amepata kura nyingi zaidi
kuliko mgombea mwingine yeyote.
(7) Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi
kwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basi
hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya
kuchunguza kuchaguliwa kwake.


Kinga dhidi ya
mashataka ya
na madai
Sheria ya 1984
Na.15 ib.9
Sheria ya 1992
Na.20 ib…
46.-(1) Wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika
madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii, itakuwa ni marufuku
kumshitaki au kuendesha mashataka ya aina yoyote juu yake
mahakamani kwa ajili ya kosa lolote la jinai.
(2) Wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka
yake kwa mujibu wa Katiba hii, haitaruhusiwa kufungua
mahakamani shauri kuhusu jambo lolote alilolitenda au alilokosa
kulitenda yeye binafsi kama raia wa kawaida ama kabla au
baada ya kushika madaraka ya Rais, ila tu kama angalau siku
thelathini kabla ya shauri kufunguliwa mahakamani, Rais
atapewa au ametumiwa kwamba taarifa ya madai kwa maandishi
kwa kufuata utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria
iliyotungwa na Bunge, na taarifa hiyo ikiwa inatoa maelezo
kuhusu chanzo cha shauri hilo, kiini cha madai yenyewe, jina
lake na anwani ya mahali anapoishi huyo mdai na jambo hasa
analodai.
(3) Isipokuwa kama ataacha kushika madaraka ya Rais
kutokana na masharti ya ibara ya 46A(10), itakuwa ni marufuku
kumshtaki au kufungua mahakamani shauri lolote la jinai au la
kumdai mtu aliyekuwa anashika madaraka ya Rais baada ya
kuacha madaraka hayo kutokana na jambo lolote alilofanya yeye
kama Rais wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya Rais
kwa mujibu wa Katiba hii.
Hii hapa…46A(10) Endapo Bunge litapitisha azimio kuwa mashtaka dhidi ya
Rais yamethibitika na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti
cha Rais, Spika atawafahamisha Rais na Mwenyekiti wa Tume
ya Uchaguzi juu ya azimio la Bunge, na hapo Rais atawajibika
kujiuzulu kabla ya kuisha kwa siku ya tatu tangu Bunge
lilipopitisha azimio hilo.)

Uteuzi wa
Mawaziri
Sheria ya
1984 Na.15
ibara 9
55.-(1) Mawaziri wote ambao ni wajumbe wa Baraza la
Mawaziri kwa mujibu wa ibara ya 54 watateuliwa na Rais baada
ya kushauriana na Waziri Mkuu.
(2) Pamoja na Mawaziri waliotanjwa katika ibara ndogo ya (1),
Rais aweza, baada ya kushauriana na Waziri Mkuu, kuwateua
Naibu Mawaziri. Naibu Mawaziri wote hawatakuwa wajumbe wa
Baraza la Mawaziri.
(3) Rais aweza kuteua idadi yoyote ya Naibu Mawaziri ambao
watawasaidia Mawaziri katika utekelezaji wa kazi na shughuli zao.
(4) Mawaziri na Naibu Mawaziri wote watateuliwa kutoka
miongoni mwa Wabunge.
(5) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (1) ikitokea
kwamba Rais anahitajiwa kumteua Waziri au Naibu Waziri baada
ya Bunge kuvunjwa, basi aweza kumteua mtu yeyote ambaye
alikiwa Mbunge kabla ya Bunge kuvunjwaMasharti ya
kazi
ya Wabunge


Sheria ya
1984 Na.15
ib.13
Sheria ya
2000
Na.3 ib.14
74.-(1) Kutakuwa na Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya
Muungano ambayo itakuwa na wajumbe wafuatao watakaoteuliwa
na Rais:-
(a) Jaji wa Mahakama Kuu au Jaji wa Mahakama ya
Rufani, ambaye atakuwa mwenyekiti;
(b) Makamu Mwenyekiti ambaye atakuwa mtu
anayeshika, aliyewahi kushika au anayestahili
kuteuliwa kushika madaraka ya Jaji wa Mahakama
Kuu au Jaji wa Mahakama ya Rufani;
(c) wajumbe wengine watakaotajwa na sheria iliyotungwa
na Bunge.
(2) Rais atamteua Makamu wa Mwenyekiti wa Tume ya
Uchaguzi kwa kufuata kanuni kwamba endapo Mwenyekiti ni mtu
anayetoka sehemu moja ya Muungano, Makamu wake atakuwa ni
mtu anayetoka sehemu ya pili ya Muungano.
(3) Watu wafuatao hawataweza kuteuliwa kuwa wajumbe wa
Tume ya Uchaguzi yaani-
(a) Waziri au Naibu Waziri;
(b) mtu mwenye madaraka ya aina yoyote iliyotajwa
mahsusi na sheria iliyotunga na Bunge kwamba ni
mwiko kwa mtu mwenye madaraka hayo kuwa
mjumbe wa Tume ya Uchaguzi;
(c) Mbunge, Diwani au mtu mwingine mwenye madaraka
ya aina yaliyotajwa na sheria iliyotungwa na Bunge
kwa mujibu wa masharti ya aya ya (g) ya ibara ndogo
ya (2) ya ibara ya 67 ya Katiba hii.
(d) Kiongozi wa chama chochote cha siasa.
(4) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, Mjumbe
wa Tume ya Uchaguzi atakoma kuwa Mjumbe litokeapo lolote
katika ya mambo yafuatayo-
(a) Ukimalizika muda wa miaka mitano tangu
alipoteuliwa; au
(b) ikiwa litatokea jambo lolote ambalo, kama
asingekuwa Mjumbe wa Tume, lingemfanya asiweze
kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi.
(5) Rais aweza tu kumwondoa katika madaraka Mjumbe wa
Tume ya Uchaguzi kwa sababu ya kushindwa kutekeleza kazi
zake, ama kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote, au
kwa sababu ya tabia mbaya au kupoteza sifa za kuwa mjumbe.
(6) Majukumu ya Tume ya Uchaguzi yatakuwa ni(12)



74(12)Hakuna mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya
kuchunguza jambo lolote lililotendwa na Tume ya Uchaguzi katika
kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.





 
Tusahihishe hapo. Tanzania haijawahi kuwa koloni la nchi yoyote. Koloni linalotimiza miaka 50 ni Tanganyika. Yote haya yanatokana na katiba mbaya. Nenda Canada au Marekani kila nchi ina serikali yake. Ni kitu kisichokubalika kusherehekea miaka 50 wa Tanganyika ikiwa imezikwa.
 
Back
Top Bottom