Miaka 50 ya uhuru Tanzania imepiga hatua, nchi nyingine je?

mzamifu

JF-Expert Member
Mar 10, 2010
6,377
3,823
Ni jambo lisilopingika kuwa tanzania imepiga hatua kubwa katika maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na hata kijamii. Lakini tunajisifu kanakwamba ni sisi pekee tumefanikiwa zaidi kuliko nchi nyingine.
Nionavyo mimi ingefaa tujilinganishe na nchi nyingine ili kupima kasi ya aendeleo yetu maana tunaweza kujigamba sana kumbe kasi ya maendeleo yetu ni ile yamwendo wa kobe.
Kuna nchi ambazo wakati wa uhuru sisi tulikuwa juu yao au tulikuwa sawa lakini sasa tunaziomba msaada.
Hii ni kusema kwamba kuendelea kwa nchi ni jabo la kawaida tu. Nchi ikishakuwepo haiwezi kuwa vilevile mara zote. La msngi ni je, hatungeweza kupiga hatua kubwa zaidi ya hii tuliyonayo? Na je, nchi ambazo maendeleo yao ni makubwa zaidi ingawa hatukupishana sana wakati wa uhuru zimetumia mbini zipi kufanikiwa ili nasi tuige?
 
mkuu umesema kitu mabacho kila leo nimekuwa nikiwaambia watu wengi.kwamba hata kama ww ni masikini ipo siku utaongeza kijiko nyumbani kwako.sasa hyo ndo kusema ni umeendelea sana mpaka ujitangaze........Tanzania ilitakiwa ijipime level ya maendeleo na nchi yenye rasilimali kama zake, nchi zilizo pata uhuru miaka kama yake. siyo maendeleo ya kulinganisha shule zilizo kuwepo miaka ya 1961 na hii leo huku unajua lazima tuongeze shule kwani idadi ya watu inaongezeka. tanzania haina haja ya kukaa chini kuangalia tumekosea wapi kwani huo mda haupo.kikubwa ni kuwaondosha walioshindwa kutufikisha kwenye dunia ya pili.
 
Back
Top Bottom