Miaka 50 ya kuigiza tamaduni na desturi za wengineo

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
kila mahali niendapo hapa nchini hujiuliza hivi utamaduni wa mtanzania uko wapi? Pamoja na sisiemu kuvibeza vyama vya upinzani kuwa ni fotokopi.......................lakini kila kitu ndivyo kilivyo humu nchini.........................nitataja baadhi tu ya ushahidi na wenzangu mtaongezea...........

fotokopi za kitaifa ni pamoja na:-

1) wimbo wa taifa nyerere bila ya kutuuliza aliunakili kutoka ANC.....................wimbo huu unahadithia utamaduni wa msauzi siyo historia ya mtanzania. hivyo tunajivunia fotokopi tu.................

2) mwenge wa uhuru ni fotokopi kutoka uchina.......................historia yetu iko wapi hapo?

3) hadi leo hatuna vazi la kitaifa hata kenya siku hizi wanalo....................jitihada zetu za vazi la kitaifa liliishia fotokopi ya unaijeria tu...............

4) katiba zote za vyama vya siasa ni fotokopi za chama cha komunisti vya USSR na uchina.......................kingunge ngombale Mwiru ambaye ndiye alifanya nukuu hizo ni shahidi hapa...


5) Taasisi zetu zote za kiserikali iwe kimuundo au kiutendaji ni urithi wa mwingereza...........na kidogo kutoka World bank na IMF..................mfano TRA, serikali za mitaa ukizifuatilia sana ni fotokopi ya mwingereza kwa maana ya indirect rule.....................

6) vibali vya polisi kwa mikutano ya kisiasa ni ubunifu wa mwingereza........................sisi pamoja na kudai uhuru tulidumisha huu ukandamizaji wa raia...........

7) polisi jamii ambayo hata maana yake hatuifahamu vinginevyo polisi wasingelikuwa wanapiga raia risasi za moto ni urithi tumeuibua kutoka nchi za magharibi...........................

8) elimu yetu ni ile ya kuwaandaa watoto wetu kwenda kuajiriwa kama wakati wa mkoloni alipokuwa anatuandaa kumtumikia yeye......................usidanganywe na kauli za viongozi ambao wameajiriwa wao pamoja na watoto wao lakini wanahimiza watoto wa wenzao wakajiajiri...........mkuki kwa mwanadamu lakini kwa nguruwe ni maumivu.

9) uhuru maana yake ulikuwa kuondoa matabaka kwenye jamii lakini sasa hivi tunajivunia kujenga matabaka ya kimapato na wanaohoji nyufa hizi za kitaifa tunawabeza kuwa wana udini bila ya kujibu hoja za kimsingi......

10)yapo mengi ambayo yananifanya nijiulize hivi mafanikio ya uhuru wa nchi hii yako wapi.....................au fotokopi sasa ni mafanikio...............kumbuka ya kuwa elimu ya kunakili kamwe haiwezi kututoa katika hema la unyonge............once a photocopy always a photocopy. ...............some say a photocopier seldom learns anything............
 
Back
Top Bottom