Miaka 50 na ulimbukeni wa rangi ya ngozi!

Nyambala

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
4,465
1,170
Ni miaka 50 tangu watanganyika baadae watanzania tulianza kujitawala na kujiamulia mambo yetu wenyewe. Ikumbukwe kwamba kabla ya hapo serikali yote kuanzia gavana (rais) wa wakati huo, mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa maeneo na hata wakuu wa shule na wasaidizi walikuwa wazungu. Waafrika kutokana na rangi ya ngozi yao walionekana na kuaminiwa kwamba hawakustaarabika, walikuwa wajinga, wapuuzi, wasio na thamani na wasiostahili kuongoza bali kuongozwa tu. Ilikuwa tofauti kidogo kwa waasia na hii ni kutokana na rangi ya ngozi zao wao wakawekwa daraja la pili, hawa kazi yao kuu ilikuwa ni kumsaidia mzungu kumtawala mwafrika.

Vijana wa enzi hizo hawakukubali na walipambana kuhakikisha udhalimu huu hauendelei walipigania kila alichowahi kukielezea mwanamapinduzi maarufu Martin Luther King Jr kwenye hotuba yake ya "nina ndoto". Alisema ntamnukuu kwamba "siku moja ndani ya taifa hili (Marekani)watoto wangu hawatahukumiwa kwa rangi ya ngozi zao bali kilichomo katika tabia zao". Ni kwa mtizamo huo wazee wetu walisimama na kumkabili mkoloni na hatimaye Desemba 9, 1961 tukapata uhuru. Tukaanza kujitawala na Viongozi wa serikali wakawa ni watu kutoka rangi zote katika jamii ya watanganyika wakati ule. Mengi yalitokea na yameendelea kutokea mpaka leo hii tunakaribia kutimiza miaka 50 toka tupate uhuru.

Kinachonisikitisha ni kwamba pamoja na kujitawala kufikisha miaka 50, lakini bado utaratibu ule ule wa watu kuhukumiwa kwa rangi zao unaendelea.

1. Inasikitisha kuona kwamba miaka 50 ndani ya uhuru lakini bado baadhi waafrika weusi wanajiona ni duni mbele ya wazungu.

2. Inasikitisha kuona kwamba miaka 50 ndani ya uhuru uzungu unahusishwa na "intelligence" na utajiri.

3. Inasikitisha kuona kwamba miaka 50 ndani ya uhuru, viongozi waafrika weusi wanadiriki hata kutamka hadharani kwamba waswahili (weusi) ni wababaishaji ukilinganisha na waarabu au wahindi.

4. Kama hiyo haitoshi Inasikitisha kuona kwamba miaka 50 ndani ya uhuru baadhi ya akina dada weusi wanaamini bwana au boifrendi wa kizungu ni mwaminifu zaidi ya mweusi na ni tiketi ya kuaga umasikini.

5. Inasikitisha kuona kwamba miaka 50 ndani ya uhuru kuna vijana wa kitanzania wanaona mabinti wa kizungu, kutokana tu na rangi ya ngozi zao ni waaminifu na ukimpata huyo basi umeaga umaskini.

6. Inasikitisha kuona kwamba miaka 50 ndani ya uhuru kampuni za weusi zinaonekana si lolote mbele ya viongozi wa serikali ambao ni weusi, lakini zinageuka lulu mara tu mzungu anapotangulizwa ndani ya kampuni hiyo hiyo.

7. Inasikitisha kuona kwamba miaka 50 ndani ya uhuru bado mtanzania mweusi ndani ya nchi yake mwenye ujuzi na uzoefu zaidi analipwa chini ya mara 10 ya mzungu anaefanya kazi hiyo hiyo.

8. Inasikitisha kuona kwamba miaka 50 ndani ya uhuru kuna watu wanaamini watoto wa kizungu wana akili zaidi kuliko watoto weusi.

9. Inasikitisha kuona kwamba miaka 50 ndani ya uhuru kuna watanzania wanawadharau watanzania wenzao eti tu kwa sababu ya weusi wa rangi zao.

10. Inasikitisha kuona kwamba miaka 50 ndani ya uhuru watanzania wengi hawafahamu kuwa kutamka mbele ya kadamnasi mfano wachina wote wanafanana si ustaarabu na inaumiza sawasawa na wewe ukiambiwa waafrika "they all look the same".

11. Inasikitisha kuona kwamba miaka 50 ndani ya uhuru kuna baadhi ya watanzania wanajisikia raha kuongozwa na mzungu au mwarabu lakini si mweusi mwenzie. Mara nyingi ukizisikia sababu zinazotajwa wala hazihusiani na rangi.

12. Inasikitisha kuona kwamba miaka 50 ndani ya uhuru watanzania wengi hawaelewi kwamba rangi ya ngozi haihusiani chochote na "intelligence", ujinga au uzinzi. Na kwamba hakuna binadamu wanaongozwa na "centralized brain". Kwamba watu ni watu wawe wachina, wahindi, wazungu n.k Pia hakuna busara wala upumbavu uliotumika kuumba binadamu wa rangi hii au ile.

Updated
13. Tanganyika tunatarajia kuadhimisha miaka 50 ya uhuru Disemba bado viongozi wetu wanaamini matibabu nje ya nchi (kwa weupe nk) ni bora kuliko ya dakta mweusi wa THI

14. Miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika viongozi wetu bado wanaamini kwa dhati kwamba misaada inapatikana kwa "weupe"

15. Miaka 50 ya uhuru bado tunaamini mtu kujua "Kidhungu" ndio ufahamu, kisukuma, kikwere, kimasai , kiswahili nk hakina nafasi

My Take:
Si maana yangu kutaka kumbagua mtu yeyote kwa rangi yake bali watanzania wana kila sababu kuangalia namna ya kuondokana na ulimbukeni huu hasa ikizingatiwa mengi ya niliyoyataja ndiyo haswaa wazee wetu waliyoyapigania zaidi ya miaka 50 iliyopita. Hiyo haswa ndiyo itakuwa namna ya kuwaenzi.

 
Mkuu Nyambala,
Inasikitisha pia Rais anaamini bila wawekezaji wa nje nchi haiwezi kundelela!! Anaamini kuendelea ni kwenda kwao kukinga bakuli!!!
 
Mkuu sana Nyambala,

Heshima mbele

Niongezee kidogo hiyo listi:

>Tanganyika tunatarajia kuadhimisha miaka 50 ya uhuru Disemba bado viongozi wetu wanaamini matibabu nje ya nchi (kwa weupe nk) ni bora kuliko ya dakta mweusi wa THI
>Miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika viongozi wetu bado wanaamini kwa dhati kwamba misaada inapatikana kwa "weupe"
>Miaka 50 ya uhuru bado tunaamini mtu kujua "Kidhungu" ndio ufahamu, kisukuma, kikwere, kimasai , kiswahili nk hakina nafasi
>nk
 
Mkuu sana Nyambala,

Heshima mbele

Niongezee kidogo hiyo listi:

>Tanganyika tunatarajia kuadhimisha miaka 50 ya uhuru Disemba bado viongozi wetu wanaamini matibabu nje ya nchi (kwa weupe nk) ni bora kuliko ya dakta mweusi wa THI
>Miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika viongozi wetu bado wanaamini kwa dhati kwamba misaada inapatikana kwa "weupe"
>Miaka 50 ya uhuru bado tunaamini mtu kujua "Kidhungu" ndio ufahamu, kisukuma, kikwere, kimasai , kiswahili nk hakina nafasi
>nk

Ni kweli kabisa mkuu, naziongeza hizi ishuz kwenye post ya mwanzo!!!!!!!!!!
 
Ni ukweli unao uma sana mkuu

Leo hii hata nyumba ukitaka kupanga hapo hapo Tanganyika, wewe na mzungu kodi ile ile, mzungu anapewa preference ati hawa wanajua kutunza nyumba!!!!!!! Ulimbukeni huu wa kuhusisha rangi ya ngozi na tabia za watu sijui utaisha lini ni aibu na kujidharaulisha kusiko mfano!!!!!!!
 
A bit of self-criticism: kweli mbantu bwana ana baadhi ya mambo hayo: ukosefu wa uaminifu (na ndiyo maana hatuendelei kibiashara), uongo, upendaji wa njia za mkato-mkato, wizi na udokozi (wengi wanaona hizi isifa na ni aina ya intelligence).
Hizi ni sifa ambazo katika kila watu watatu wabantu mmoja atakuwa nazo. Sisemi wazungu hawana, lakini ratio pengine ni katika mia mmoja atakuwa hivyo.
Na mimi pia nakasirishwa na dhana hizo, lakini ukweli usemwe, na ndipo labda tutaanza kujirekebisha. Kutoendelea kwa Waafrika kunatokana zaidi na wao wenyewe!
 
A bit of self-criticism: kweli mbantu bwana ana baadhi ya mambo hayo: ukosefu wa uaminifu (na ndiyo maana hatuendelei kibiashara), uongo, upendaji wa njia za mkato-mkato, wizi na udokozi (wengi wanaona hizi isifa na ni aina ya intelligence).
Hizi ni sifa ambazo katika kila watu watatu wabantu mmoja atakuwa nazo. Sisemi wazungu hawana, lakini ratio pengine ni katika mia mmoja atakuwa hivyo.
Na mimi pia nakasirishwa na dhana hizo, lakini ukweli usemwe, na ndipo labda tutaanza kujirekebisha. Kutoendelea kwa Waafrika kunatokana zaidi na wao wenyewe!

Mkuu nimeishi nakuendelea kuishi katika mahali ambapo kazini mimi ni mwafrika peke yangu, mtaani the same, ni familia yangu tu almost everywhere tuko wenyewe tu. Lakini nakutana na karibu yote uliyoyataja hapo almost kila siku. Hiyo pia ni sababu iliyonisukuma kuanzisha hii thread. Lakini pia say ulichosema ni sahihi unawatambuaje kwa kuwaangalia tu watu wenye tabia hizo?????????? Au hii ndiyo justification ya kuiwaona weusi wote sio waaminifu, waongo, wapenda njia za mikato????
 
Back
Top Bottom