AirTanzania
JF-Expert Member
- Mar 17, 2011
- 1,139
- 1,033
Angalia Signature inajieleza sina cha kuongezea, Mimi sio tu kama sina Imani nayo bali naichukiya kwa jinsi ilivyojaa Rushwa na kulindana.
Angalia Signature inajieleza sina cha kuongezea, Mimi sio tu kama sina Imani nayo bali naichukiya kwa jinsi ilivyojaa Rushwa na kulindana.
Kuna mtu kaninong'oneza, eti nchi hii inaongozwa kisera
Mnakiamini chama cha Mapinduzi kinachoongoza serikali hiyo?
Mkuu ni kimjini mjini au mishen town
Teh teh teh!!!
Mzee namna gani?Mnakiamini chama cha Mapinduzi kinachoongoza serikali hiyo?
Mzee namna gani?
Kwani chama cha Nyerere bado kipo?
Hakipo hicho, Chama Cha Mapinduzi hakipo. Kuna CCM nyingine kirefu chake nadhani nii...
Ukiondoa majengo, viwanja vya michezo, wiwanja vya kulaza magari na mali zinginezo za CCM ambazo kimsingi ziliachwa na Mwalimu [mali ya Watanzania - baada ya hapo hazikuwahi kuongezeka bali zinapungua], binafsi sidhani kama kuna chama bali hizo mali. Watu waliozizunguka ndiyo tunawaita wanaCCM lakini ukiangalia hakuna hata mmoja anayetimiza masharti ya chama.
Kwa hiyo huwezi kuwaamini watu amabao wenyewe hawaamini misingi (katiba) ya chama chao!
Chama Cha Ma...........
Tunawatazama wamalizie walichosahau ili tuunde serikali halisi. Sitaki hata kuiita serikali kwa matendo yanayofanyika kama genge la wahuni
Hadi hivi sasa kama Mtanzania umesikia mengi kuhusu uongozi na utawala na matokeo yake katika maisha ya Watanzania. Umesikia sera mbalimbali zikifanyiwa kazi na mafanikio yakitangazwa. Kuanzia ujenzi wa barabara, mahospitali, kliniki, miundo mbinu mingine mingi na mipango kadha wa kadha ya maendeleo. Yawezekana umeweza kushuhudia juhudi mbalimbali za maendelo zinazofanywa na serikali. Utakuwa umesikia mipango na malengo mbalimbali ya serikali na pia kuna mambo umeyaona mwenyewe au kusimuliwa jinsi serikali ilivyofanya kuleta maendeleo.
Na siku za karibuni bila ya shaka umesikia hatua mbalimbali za jinsi gani serikali imechukua kuonesha uongozi. Kuanzia sakata la Ngeleja na Jairo, sakata la BP na Mafuta na sasa sakata la Maige na wanyama. Yote yamefanyika katika kuonesha kuwa serikali iko "on top" of things; Bunge liko "on top" na kuwa viongozi waliochaguliwa "wanasikiliza wananchi".
Lakini muda wote huo yawezekana umeona mengine mengi ambayo yameacha maswali. Katika kuadhimisha miaka hii hamsini unajisikiaje zaidi:
a. unaamini serikali zaidi?
b. Unaiamini lakini unataka uthibitisho?
c. Unaishuku mara zote?
d. Unashuku maamuzi yake?
e. Huamini kabisa?
f. Unaangalia watu gani wa serikali wanasema au kuamua; yaani unaamini katika watu binafsi kuliko taasisi zao?
g. Hujali lolote linalofanywa na serikali?
Kwanini?
Mnakiamini chama cha Mapinduzi kinachoongoza serikali hiyo?
you have explained well my view:Chama cha Mapinduzi kilijulikana kama chama cha wakulima na wafanyakazi, na kilianzishwa katika misingi ya udugu - African Socialism. Now, changes nyingi zimefanyika kimfumo na kimtazamo ndani ya hiki chama na vigumu kuelewa wakubwa hawa wanaposema kuwa bado zile 'founding principles' zinatekelezwa!
Sasa, swali kuwa nakiamini chama cha mapinduzi linanifanya nijuilize chama cha mapinduzi kipi? na kiko wapi? Kinaongozwa na nani?
Kwa mtazamo wangu, Tanzania hatuna chama cha mapinduzi, ila tuna watu wanaoomba kura na wengine kupata dhamana za uongozi kwa kutumia 'brand name ya chama cha Mapinduzi'. Na msingi wa jibu langu ni huu, kile chama cha wakulima na wafanyakazi kinafanana na hiki cha leo?