Miaka 48 ya JWTZ

Kweli umenikuna sana ndugu yangu kwa uzalendo wako unaouonyesha kwenye Jeshi letu pekee, tena pekee kabisa kwa uzalendo hapa nchini. Kimsingi hili jeshi ni katika majeshi bora hapa Duniani pamoja na zana zao duni walizonazo.

Mimi kwa akili yangu niliyonayo ukitamka JWTZ mwili unasisimuka kwa vile maisha yangu na watoto wangu nimeyakabidhi kwa hili jeshi. Watoto wangu wanafahamu chombo pekee kwenye nchi hii kinacholinda maisha yetu ni JWTZ na si kingine chochote.

Kwa hali iliyopo kwenye majeshi mengine kama Polisi, Magereza na Usalama wa Taifa ambayo yamegubikwa na rushwa na uharifu mkubwa dhidi wa wananchi wao ni JWTZ ndiyo nguzo pekee ya watanzania iliyobaki. Kimsingi mimi naliheshimu JWTZ kulipo taasisi yoyote hapa Nchini ikiwa ni pamoja na RAIS.

Vilevile napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange kwa ujasiri alionao katika kulinda wananchi wake ikiwa ni kuboresha maisha ya askari hasa wa ndazi za chini kwenye Mishahara, nyumba za kuishi, usafiri na vifaa vya kutendea kazi (Zana za Kijeshi) ambao wamekuwa katika maisha ya shida kwa muda mrefu sana. Huyu ni Mkuu wa Majeshi wa mfano kabisa hapa nchini kwanza kwa kutojihusha na masuala ya kisiasa na kuwa na msimamo kuhusu maisha ya watanzania.

Nafahamu vizuri ambavyo amekuwa akishawishiwa kulinda maslahi ya wakubwa lakini amekuwa na msimamo wa kwake kuhusu watanzania na kusimamia hilo.

Hata hivyo nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipowapongeza makamanda wote wa JWTZ kwa kazi nzuri wanazozifanya kwa ajili ya watanzania, ingawa mara nyingi wamekuwa wakibezwa na baadhi ya wananchi wasiokua na uzalendo na nchi na wasiofahamu umuhimu wa Jeshi hilo lakini nawaomba wasife moyo kwani wengi tunawaunga mkono kwa kazi nzuri wanayofanya kwa watanzania.


JESHI PEKEE LILILOBAKI KWA MASLAHI YA WATANZANIA NI JWTZ NA SI VINGINEVYO.

spot on! U understand comrade!
 
Pole.
Unajivunia kuwa Mtanzania wakati Twiga na wanyama wengine wakipandishwa kwenye Ndege na kutokomea umangani, unajivunia kuwa mtanzania wakati watu wanakomba pesa nchini na kwenda kuzificha nje ya nchi kwa maslahi yao na familia zao.

Nyerere alisema “Siku inakuja ambapo watu watachagua kifo
kuliko fedheha na ole wao wale watakoiona siku
hiyo!. Na ole wao wale watakaoifanya siku hiyo
iepukike''.

Sasa hiyo siku haiko mbali, na ole wao hao JWTZ wajaribu kuizuia.

Kaka kama haujivunii u Tanzania unataka ujivunie ukenya, malawi, marekani,uchina, uindia! Ukizaa mtoto kilema utasema siyo wako? Mimi sizungumzii uzalendo bali utaifa! ​Umezaliwa Tanzania utakuwa Mtanzania labda ununue uraia wa nchi nyingine!
 
Kaka kama haujivunii u Tanzania unataka ujivunie ukenya, malawi, marekani,uchina, uindia! Ukizaa mtoto kilema utasema siyo wako? Mimi sizungumzii uzalendo bali utaifa! Umezaliwa Tanzania utakuwa Mtanzania labda ununue uraia wa nchi nyingine!

ni kweli, wazungu husema, u cant choose parents!
 
To be honest JWTZ ndio taasisi pekee ambayo haijawa corrupted. Mimi kama kijana wa kitanzania natamani sana kuitumikia, elimu yangu ni ya juu ila uzalendo wangu ni PHD. Taratibu zikoje za kujiunga? Umri? MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU BARIKI JWTZ!

Zile trilioni za Shimbo zilifisadiwa wapi vile? KMKM eeh, na yale majenereta na magari ya kukodi kule Sudan? Usinikumbushe jinsi wajeda wetu walioshiriki operesheni za AMESOM walivyopigwa panga mpunga wao...
Mwisho nadhani uadilifu wao umewafanya silaha ziwalipukie mara mbili ndani ya miaka miwili.
Jeshi la Wakurya Tangu Zamani!
 
1.jpg

"The only easy day was yesterday" uzalendo kwanza, good day!
Moshe..Nakumbusha Israel commanders.

At least physically wanaonekana kuwa maulti-purpose.Si wafupi ,wala warefu saana na si wachovu, wala si manyama uzembe.

Pia uwepo wa vijana wenye mwamko wa kuwa fit na physically fit and presentable inatupa jeshi zuri na linaloweza kimbia na time.
 
Pole.
Unajivunia kuwa Mtanzania wakati Twiga na wanyama wengine wakipandishwa kwenye Ndege na kutokomea umangani, unajivunia kuwa mtanzania wakati watu wanakomba pesa nchini na kwenda kuzificha nje ya nchi kwa maslahi yao na familia zao.

Nyerere alisema “Siku inakuja ambapo watu watachagua kifo
kuliko fedheha na ole wao wale watakoiona siku
hiyo!. Na ole wao wale watakaoifanya siku hiyo
iepukike''.

Sasa hiyo siku haiko mbali, na ole wao hao JWTZ wajaribu kuizuia.
Jesus alisema siku zaja....watu watawaua wakidhani wanamtolea Mungu dhabihu....Isaya ..aliwalaani wale wajisifuo kuwa wana maagano na kifo.God bless our Jeshi as long as wanakufa ili kuokoa uhai na values zinazotupa utaifa si kuungamiza.
 
1.jpg


Jeshi la Wananchi wa Tanzania, kesho litatimiza miaka 48 tangu kuanzishwa kwake.

Ikumbukwe kua JWTZ lilizaliwa baada ya uasi ulotokea January 1964 wa jeshi la kikoloni (Kings African Rifle), chini ya muingereza.

Madai ya "waasi" yalikuwa kwa ujumla ni kuhusu kupinga uongozi wa kijeshi wa waingereza (nchi tayari ilikuwa huru) maslahi duni na kuboresha mazingira ya kufanyia kazi, mwalimu Nyerere aliona madai yana msingi, na akavunja jeshi la kikoloni na likaundwa jipya ambalo halikua na uongozi wa weupe na hapo ndipo likazaliwa jina la JESHI LA WANANCHI TANZANIA, vuguvugu la uasi lilizuka tena january 1983, makamanda na askari walikua na madai ambayo hata kwangu yalikua ya msingi sana, ila sitapenda kuyazungumzia kwenye mada ya leo.

Mkuu wa majeshi wa kwanza alikua mkuu sarakikya(alistaafu kama major general) na mkuu wa majeshi saivi ni jenerali davis mwamunyange.

Jeshi lina kamandi (command) tatu, ila lina matawi makuu matano, nayo ni:
1. Land forces command
2. Naval command
3. Air defence command
4. Military intelligence
5. National service (JKT)

Jeshi limepigana vita nyingi za wazi(all out war-total war) e.g kagera war, comorro na pia covert operations, in mozambique, seychelles (regime change), congo drc, nigeria, etc, pia jeshi limefanya peace-keeping missions, eg darfur, Lebanon, etc

Vita ambayo inakumbukwa zaidi ni ile ya kagera ambayo chokochoko zilianza mwaka 1972 na ilipofika november 1978 majeshi ya uganda yaliingia tanzania.jeshi lilijipanga vizuri na april mwaka 1979 kampala ilianguka kwa majeshi yetu

pamoja na mapungufu machache yaliyopo, ningependa wananchi mulitie moyo jeshi letu na kuwa na imani nalo KWANI ILIPOBIDI NA INAPOBIDI JESHI LETU HULINDA MIPAKA YETU NA MAISHA YA MTANZANIA KWA GHARAMA YOYOTE

Tusahau wachache wanaoharibu sifa ya jeshi ila tuwakumbuke wengi wanaofanya kazi kwa bidii kuitumikia nchi yetu, na tuwakumbuke mashujaa wote waliokufa kwenye mapambano.

Askari+JWTZ+wakiendelea+na+ujenzi+wa+daraja.JPG


"The only easy day was yesterday" uzalendo kwanza, good day!

Asante sana kwa mchango wako juu ya historia ya jeshi letu. Wasiwasi wangu mkubwa ni kwa hawa wadogo zetu na wanetu-wanapata hata muda wa kusoma makala na maandiko mbalimbali juu ya historia ya nchii hii na taasisi zake?
 
Shin Bet? An Israel trained "katsa"?

Well, mimi nni mmoja wa vipenzi vya jeshi letu. Nisichoelewa ni kwanini historia yake haiandikwi ikachezewa filamu kama zile za Korea, au Gen. Douglas McArthur, Dwight Eisenhower etc...

Tukilijua vizuri tutalipenda zaidi. Wengine wanalijua kwasababu ya vipigo wanavyopata wananchi kutoka maeneo mbalimbali.



Mkuu hapo umeongea,yaani kwa hali ilivyo ni kama hawa jamaa wapo juu ya sheria,yaani wanapiga raia kama hawana akili nzuri lakini hakuna wa kuwachukulia hatua.Hili linanikera sana aisee.
 
Naombba nirekebishe hapo, ni kweli jeshi Lina kamandi tatu ila Lina Malawi Sita! Umesahau Central Command(NGOME) nayo hua inahesabika Kama tawi la Sita kimuundo



Taratibu Mkuu,mbona unataka kuchafua jukwaa!!!
 
Sorry mkuu nimesharekebisha, ilikua ni typing error tu! Mjadala uendelee tafadhali
 
Mambo ya jeshi ni siri. Kumbuka sakata la Meremeta kule kwenye mgodi wa Buhemba-Mara

Kuna information zinaendelea kuwa classified as long as it takes. Kuna nyingine zinaweza kutolewa with time. Ukiona kila kitu ni siri ujue kuna tatizo. I read stories about espionage during world war two...why are they being divulged?
 
Hahaaaa, nimependa post yako, unaonekana unasoma vitabu, kuna mtu alikua anaitwa patton, alikua general wa marekani kipindi cha world war 2, tactics zake za vita za wakati huo hadi leo zinasomwa kwenye vyuo mbali mbali vya kijeshi duniani, alikua maarufu kwa kiko mdomoni all the tym kama winston churchill vile

George Patton nimeona movie yake tu na jinsi alivyokuwa arrogant akipambana na yule muingireza sir Mc something...But in short the life blood of any sustainable system does require people to read and educate their minds bila kuchoka. Ninapopata muda I read...and I read some of the literature because of my passion for quality leadership. The army all over the world is assumed to produce the best leadership individuals. No matter we do in life, leadership comes first...Pengine kuna mtazamo mwingine..
 
Back
Top Bottom