Miaka 35 ya ccm: Wananchi watokwa machozi ya furaha (picha)

Vipi waolikuwa wanalia wenyewe haikuruhusuwa kuwapiga picha?. Maana hazijaonekana hapa

aaah mkuu picha zipo nnazo hapa tatizo ni kwamba wale waliozirai wengine walibaki uchi wakati wanatapatapa pale chini sasa kuweka picha hapa haitakuwa vizuri kuwadharirisha
 
Waungwana ebu manyeni mautundu mutuwekee hotuba ya Mwenyeti wa Chama Cha Mapinduzi,CCM.
 
Hawa mbinu zao tunao mifukoni!



2015 ndiyo tujajua kilichomnyima Kanga ndege manyoa ya shingo!

chichiem itabaki jina tu!

Taifa ni VIJANA!
 
Kuna jambo ambalo mara mbili sasa limeushangaza ulimwengu, ni vile jinsi Wakorea wa kaskazini walivyolia alipokufa Kim Il Sung na juzi juzi tu, Kim Il Jong. Wengi waliuliza ni kilio cha kuonyesha uchungu wa kweli, au wanatakiwa waonekane wakilia?
 
Okey,...
hawakusema ndani ya miaka 35 wameifanyia nini Tanzania zaidi ya
kuiba mali za nchi?
 
soma vizuri ni kilio cha furaha watu walifurahi kupita kiasi ndo wakaanza kulia
Umesahau kuwa sherehe hizo zilirushwa live na star tv pia tbc 1, waliopewa kadi za ccm ni 30 na wala hawakutajwa wanatoka chama gani.Sasa hao wanachama 4500 wa chadema wewe umewatowa wapi? Mtu mzima hovyooo!
 
amini usiamini ewe ndugu, kijana, mama, kaka, mjomba, shangazi, dada CCM inapendwa na kada zote za kijamii, hayo yamedhihirika leo mwanza ambapo watu takribani 100,000 walikuwa uwanjani kirumba kushuhudia mtoto mpya akizaliwa baada ya kujivua gamba. Umaarufu wa chama cha mapinduzi umewashangaza wengi leo na mbaya zaidi ni pigo kwa cdm baada ya kuondokewa na wanachama wake zaidi ya 4500 wakiongozwa na vigogo wao, huku wengine wakiahidi kurudisha kadi baada ya sherehe.

kwa macho yangu nimeshuhudia wamama kwa wababa wakilia machozi yaliyoambatana na mayowe na baadhi ya watu walianguka hii nikutokanana na kulia muda mrefu

ccm%2B6.jpg


ccm%2B5.jpg

Mama leo aligeuka kivutio uwanjani na mara tu baada ya kuingia uwanjani vifijo na nderemo vilitawala

ccm%2B10.jpg

furaha
ccm%2B11.jpg

watu wamepagawa na mtoto mpya

ccm%2B7.jpg


ccm%2B8.jpg


vigogo walihudhuria
ccm%2B3.jpg

Watu laki moja? magamba noma nimewakubali...kweli nyie namabari wani
 
soma vizuri ni kilio cha furaha watu walifurahi kupita kiasi ndo wakaanza kulia

Hahaha,ume nikumbusha mbali sana.
Mhubiri mmoja alikua akitoa somo kanisani,...
basi alipokua akiendelea sana mama mmoja akaanza kulia sanaaa.

Mhubiri yule alivo sikia sauti za kulia akajua somo lime muingia sana
yule mama na akawa ana refusha mda wa mahubiri ili ujumbe uwaguse watu wengi zaidi.
Lakini alilia mmoja tu.

Baada ya ibada,alimfuata yule mama kujua alikua "ametenda dhambi gani"....

Basi yule mama akasema sijafanya dhambi yoyote,ila kila nilipo kua nikikuona nilikumbuka
beberu wangu aliye ibiwa jana,....alikua na ndevu kama zako.

Mhubiri akachoka sana.

Unaweza dhani hao walio kuwa wanalia walikua wanalia kwa furaha lakini ikawa sivyo.

Walikua wanalia kwa maisha mabovu waliyo yapata chini ya chama cha mafisadi.
Ugumu wa maisha chini ya ahadi ya maisha bora.
Hasira za kutaka kuwatafuna ila wanashindwa kwa sababu mmelindwa sana.
Hasira za kukalishwa mda mrefu bila kupewa minyama mliyo ahidi.
Hasira za kunyimwa posho kama mlivo ahidi,...etc.

Don't ever be fooled by a smile or some tears.
Nothing is as it seems to be.
 
vipi kauli ya kujivua gamba alisemaje leo?
maendeleo yamefikia wapi?
na hao walio goma kujivua gamba chama kitawachukulia hatua kali lini ?
 
Umesahau kuwa sherehe hizo zilirushwa live na star tv pia tbc 1, waliopewa kadi za ccm ni 30 na wala hawakutajwa wanatoka chama gani.Sasa hao wanachama 4500 wa chadema wewe umewatowa wapi? Mtu mzima hovyooo!
Mkuu niliona na kusikia kwamba wale 30 walikuwa ni wawakilishi wa wanachama wengine. Nimesahau idadi ila ninachokumbuka kuona ni kwamba kati ya hao 30 wazee walimuwa wengi.
 
Back
Top Bottom