Miaka 35 ya ccm: Wananchi watokwa machozi ya furaha (picha)

soma vizuri ni kilio cha furaha watu walifurahi kupita kiasi ndo wakaanza kulia

Usiseme inapendwa toa sababu za kupendwa hiyo ccm imefanya kipi bora ili ipendwe?hata hiyo kusema eti wanachama wa cdm wamerudisha kadi kwa idadi hiyo ni uzushi.ndio yale ya jk aliyosema ccm bila kuimarisha propaganda chama kitakufa.hiyo pia ndio propaganda unayoleta.ccm imeshakua mfamaji lazima itapetape
 
Yani mtu analia mpaka kuanguka kisa anafurahia chama kilichofikisha Tanzania hapa ilipo? Kweli waTanzania ni zaidi ya uwaonavyo!!
 
Usiseme inapendwa toa sababu za kupendwa hiyo ccm imefanya kipi bora ili ipendwe?hata hiyo kusema eti wanachama wa cdm wamerudisha kadi kwa idadi hiyo ni uzushi.ndio yale ya jk aliyosema ccm bila kuimarisha propaganda chama kitakufa.hiyo pia ndio propaganda unayoleta.ccm imeshakua mfamaji lazima itapetape

Leo kweli tumeshuhudia wakitapatapa, na wewe hukutazama TV? si uliona pale sungu sungu walivyo piga gwaride lao la kutapatapa na kipekee na kihistoria?
 
CCM WAMECHUKUA VIKUNDI VYA UTAMUDI ILI KUPATA WATU WENGI-SIJUI HIVYO VIKUNDI WAMELIPWA SHILINGI NGAPI-
HALI ZA WANANCHI WALIOHUDHURIA ASILIMIA 100 WAMECHOKA NA MAISHA,HAWANA MATUMAINI.
kimsingi kilichofanyika ni kuchosha wananchi
 
Haya mm napita na mmeambiwa wote wenye tuhuma wasipitishwe, ww bado na mafisadi kwani hakuna wengine wa kugombea mpaka upite nae nchi nzima?
 
Kusema ukweli hawakwenda kwa sababu ya ccm walienda kumuona huyo kucheza ngoma za kwao maana siku hizi ni adimu na kula nyama maana bei yake hawaiwezi. Raha iliyoje usafir bure, soda bure, na nyama kwa nini isiwe weekend ya simulizi na wanangu.
 
Hongera...maisha yamekuwa bora ndo maana wamefurahi na alivyoingia mama ambaye anajua uchungu wa masiha na kupanda kwa gharama...wakazidi kuwehuka..kwa kweli hiki ni chama cha kuwajali wanyonge.....
mmefanikiwa mno na uchumi unapaa hata huku mtaani mnapendwa mno kwani hali za uchumi zimeboreka na raia hawalali njaa.

mkuu huo ndo ukweli wenyewe kuhusu chama chetu, vipi wewe umeshajipatia kadi yako tuijenge nchi yetu?

mtoa mada hebu nijibu swali langu au wewe ni mmoja wa kitengo cha propaganda ccm?

mkuu kirumba ni uwanja mkubwa kuliko viwanja vyote tz halafu haikuwa mechi ya mpira wa miguu watu walijaa mpaka kwenye pitch.
 
Jamani kuna mwenye fununu zimetumika kiasigani na zimetoka fungu lipi kule hazina ? Hawa akina Makinda wamekumbuka mgomowa Madaktari ai wao wanasonga mbele tu ?JK hakuendelea mgomo wa madaktari huko?
 
je kuna ufahari gani wa kuwa na sherehe njema iwapo nduguzo wanakufa kwa madaktari kugoma. Are u sure that nduguzo wote wanapata huduma za msingi ipasavyo. Uishipo kwenye jamii inayohangaika kamwe hutakua na amani.
 
...Kwa wale waliofatilia ama kwa kuwepo uwanjani au kama sisi tulioangalia kupitia TV kuna vioja,vituko na vitimbwi vilivyotokea leo pale uwanjani ambavyo havikuwa vya kawaida hata kidogo.Na kati ya hivyo hivi ni mojawapo;
  1. CCM kmtafuta kijana waliyemuita kuwa mwenyekiti wa wamachinga jijini Mwanza,na akaja pale kutoa hotuba iliyojaa unazi badala ya kuwakilisha matatizo ya wamachinga.Kwa hiyo wanaojua kusoma majira na nyakati wakagundua kuwa hii ilikuwa geresha ya CCM...
  2. Kuna vijana wa GreenGuard,hawa walitia fora kwa gwaride lao lililojaa njaa na udhaifu mkubwa.Yani atawakati wanatembea unaweza ukasema ni msafara wa wagonjwa wanaandamana kwenda kumuona dokta.Kwa kweli walikuwa dhaifu kuanzia miili,muonekano wa nje nk.Ni kama walikuwa na njaa sana.
  3. Mbunge wa viti maalumu Vicky Kamata,leo aliibuka na wimbo uliosema kuwa ulitungwa na akina mama wa Geita.Na wimbo unasema,mageuzi usinifuate mimi nimekwishaolewa na mume wangu ni CCM,na anajua mambo ambayo wewe uwezi kunipa...nikajiuliza Je,hayo mambo anayopata ni mambo gani?
  4. Mwimbaji Suma Lee,huyu ni wa Bongo Fleva..yeye alipopanda jukwaani baada tu ya muda mfupi Vicky Kamata aliposhuka,yeye alianza kusema "Kama mlivyosikia kuwa Vicky amesema ana mwanaume asifuatwe,mimi ndio mwenyewe,akasema wanaume oyeeeeeeee!!!"
  5. Kubwa kuliko M/kiti wa CCM mkoa wa Mwanza akatangaza kuwa watu wasiondoke uwanjani baada ya kumalizika kwa sherehe,maana kuna chakula kimeandaliwa kinachotosha watu wote waliokuwepo pale uwanjani...sijui baada ya hapo mambo yalikuwaje...
  6. Kwa mara ya kwanza SUNGUSUNGU wametambulishwa kama kikosi cha CCM,sasa hapa unajiuliza SUNGUSUNGU tangu lini wamekuwa kikosi cha CCM?
  7. Kwa mara ya kwanza Lowasa na Rostam awakuhudhuria kwenye sherehe kubwa zinazohusu chama chao....na JK akatoa kauli ya mwaka "Kama unadhani falsafa ya kujivua gamba ni hovyo,basi wewe ndio wa hovyo zaidi" hapa alikuwa anamgusa white hair bila shaka...
  8. Kwa mara ya kwanza nimemuona Bi Anna Makinda akicheza taarabu akiongozwa na mama Salma ingawaje yeye ni mtaalamu kwa vidole juu....na hii ilikuwa baada ya JK kuwaamsha na kuwaambia wanyoonye vidole juu wakati Vicky Kamata akiimba,maana wimbo wake ulikuwa na maadhi ya pwani kidogo.
Haya ndiyo niliyoyaona kwa leo,na nimeona nishiriki nanyi hapa JF.
 
..Mkuu asante kwa taarifa maana matukio uliyotujuza mengi hatutaweza kuyasma ktk magazeti wala kuyaona ktk TV
 
Vipi waolikuwa wanalia wenyewe haikuruhusuwa kuwapiga picha?. Maana hazijaonekana hapa
 
Back
Top Bottom