MIAKA 35 ya CCM na changamoto za kiutawala LIVE ON Star TV

Yahya Mohamed

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
270
317
Karibuni katika mjadala unaoendelea sasa kuhusu MIAKA 35 ya CCM tija ili masuala kuhusu mwelekeo wa Taifa na hatamu za Uongozi
Wageni
Dr.Bana
Dr.Ayoub Ryoba
Nape Mnauye
Stephen Maurice
 
Goodmorning Yahya:
1. Ninamuuliza Nape anaridhishwa na mambo yanavyokwenda ndani ya chama chenye umri wa miaka 35?
2. Magamba yameshindwa kung'oka?
3. Je Nape ana imani na uwezo kuongoza wa mwenyekiti wake wa chama ambaye analaumiwa kwa kuasisi makundi ndani ya chama?
 
Dr bana atuambie: changamoto ambazo zinazoikabili ccm katika katika kulinda misingi iliyosisi chama hicho hasa 'miiko ya uongozi'
 
wa SAUT Mwanza. Si kweli kwamba misingi ya chama cha mapinduzi iliyoirithi kutoka kwa ASP na TANU mwaka 1977 ndio inakiongoza chama kwa sasa. Ushindani umekifanya chama kukosa muelekeo, hadi kuoneana aibu ya kuwajibishana kwa viongozi wakichelea kukichafua chama hiki mbele ya umma.
 
Namuuliza Nape
.Je katika miaka 35 CCM imeweza kuwapa watanzania maisha bora wakati maisha yanazidi kuwa magumu?
.Miaka 35 ya CCM tumeona watu wa kada za chini hawapati nafasi za uongozi,watu wanarithishana uongozi ndani ya chama,nini maoni yake?
 
HABARI ZA ASUBUHI


-Naomba kuuliza ni kwann ndani ya miaka 35 ya ccm umasikini unazidi kukua,
wakulima wanazidi kuwa duni,ufisadi unazidi kuongezaka
-Dr. Bana anamaslahi gani na ccm,mbona naona anaweka taaluma yake pembeni na kutetea maslahi ya chama na kusahau kufanya analytical yenye maslahi kwa wananchi !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
-Dr. Bana anaongelea vipi sintofahamu kati ya wabunge ccm,Raisi,Bunge juu ya posho kwenye maslahi ya wanachi katika kuadhimisha miaka 35 leo tarehe
5/2/
 
wamesema chama cha mapinduzi kilikua chama cha wakulima na wafanyakazi lakini kimebadilika kulingana na mabadiliko ili kiweze kuendelea kushika dola.swali..chama hicho bado ni chama cha wakulima na wafanyakazi au kina misingi mingine? Pili, wafanya biashara wanaonekana wanamchango mkubwa na wanachukuliwa kwa uzito wa juu sana ndani ya chama.. Hamuoni kwamba wafanyakazi na wakulima wameachwa na wafanyabiashara wamechukua nafasi?
 
swali kwa wageni: ikiwa chama ni misingi, je ccm kwa kuiacha misingi yake na kuwatelekeza wakulima, wafanyakazi, wakwezi na wavuvi, na sasa kukumbatia matajiri na wenye mitaji tutegemee ccm kusherehekea miaka mingine 35 baadae. yaani kitakuwepo miaka 35 ijayo?
 
Habari za asubuhi Mr. Yahaya ,
Naomba: Nape atuambie kama sera za kujivua gamba hazikua sera za kukurupuka tu na mpaka sasa hivi sera hizo zimeonekana kama wao wenyewe hawaziamini ,na kama wao wanaziamini basi wazitekeleze ila kama hawawezi kuzitekeleza basi watoe mbadala wake ili wanachama na wananchi wajiridhishe kwamba chama kimekomaa na kweli kinaonesha ukomavu wake.
 
wa SAUT Mwanza. Swali kwa Ndg. PHILIP CCM wamejiandaaje kukabiliana na changamoto ya kupoteza mvuto kwa rika la vijana ambao ndio Taifa la leo? Je, kujivua gamba ndio mwisho wa changamoto zinazokikabili chama au kuna Plan 'B'?
 
Je Nape ana kiri kuwa CDM ina wapa changamoto katika siasa za Tanzania?
Kwa nini CCM imepoteza mvuto kwa kada ya wasomi?hawaoni kuwa kupoteza mvuto kwa wasomi mi kujichimbia kaburi?
 
namuuliza huyo mzee hapo studio mwanza..hana lidhishwa na mfumo wa ccm kwa sasa, je anaonaje huu utaratibu mpya wa ccm wa kupiga kampeini za uraisi miaka 4 kabla ya uchaguzi wakipelekea malumbano ndani ya chama ni maana yake na kwanini ccm imekaa kimya na huyo mzee anasemaje na yeye mwenyewe anashuudia mambo hayo.
 
Yahya Kipindi Kizuri nafagalia tuongee asubuhi jumapili
CCM kwa sasa naona wanasera mfu kwa maoni yangu ,kwa sasa CCM ni ile inayosimamia serikali ya viongozi waliojisahau wanaodhani wako juu ya wananchi
 
Karibuni katika mjadala unaoendelea sasa kuhusu MIAKA 35 ya CCM tija ili masuala kuhusu mwelekeo wa Taifa na hatamu za Uongozi
Wageni
Dr.Bana
Dr.Ayoub Ryoba
Nape Mnauye
Stephen Maurice

Asante mkuu; tuko mbele ya luninga tunafatilia mdahalo.
 
CCM imepoteza DiraN hivyo nchi nayo imepoteza Dira, kuna kila sababu ya kukiondoa chama hiki madarakani ili kikajipange upya, maana wananchi hatuwezi kubeba gharama za chama hiki kuendelea kuwa chama tawala tutaendelea kulididimiza taifa hili!
 
Tatizo la Maamuzi ya Zanzibari kama sio Azimio ni kutokuweka mipaka ya umiliki wa Mali kwa wanachama wake (hii ilikuwa mwiko mkuu wa Azimio la Arusha).Kiasi cha kusababisha miiko ya Azimio la Arusha kumezwa.Kwa sababu hii, ndio maana tunasema Azimio la Arusha limekufa.
 
Yahya soma maswali vizuri, muuliza swali Makamuzi anasema Je Nape anakiri kuwa CDM inawapa changamoto? Siyo vyama vya upinzani upinzani!
 
Ndugu Nape hamuoni sasa umefika wakati wa kutenganisha kofia hizi mbili za uenyekiti wa chama na urais? yaani Rais asiwe mwenyekiti wa chama ili chama kiweze kuisimamia serikali ipasavyo?
 
Nape anaweza kutueleza fedha ngapi zimetumika kwenye sherehe hizi ,hapo Mwanza kuna watoto wanakaa chini darasani,kuna zahanati hazina magari ya wagonjwa ,jee hayo mapesa wanayoyafuja jee wasingesherehekea kwa kununua vifaa hivyo kwa niaba ya wananchi
 
Habari,

Je CCM imewahi kufikiria kuwa siku moja kitatoka madarakani? Kipo tayari kutoka madarakani kupitia sanduku la kura katika uchaguzi huru na wa haki?
 
Back
Top Bottom