Miaka 32 ya CCM - Upinzani wa Kweli "utatoka" CCM!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
M. M. Mwanakijiji

1220_D49.jpg

“KUZALIWA kwa chama kipya, tarehe tano mwezi wa pili sabini na saba, eh Mungu kipe baraka!” “Chama chetu Cha Mapinduzi eh chajenga nchi.”

“Ewe chama nguzo yetu, kiongozi wa taifa. “Twalalamika pembeni, Hatupewi madaraka, na huku nyuma nyuma twajiweka, Tutamuongoza nani eeeh.” “Nambari wani eeh, nambari wani CCM!”

Ndiyo, Miaka 32 ya Chama Cha Mapinduzi ndiyo hiyo inayoyoma!

Miaka ambayo kwa hakika imeacha alama ya kudumu katika utawala wa taifa letu. Ni miaka ambayo naweza kuiita ni ya msingi kabisa katika ujenzi wa taifa letu.

Ni miaka ambayo kizazi cha uhuru kimeanza kukabidhi madaraka taratibu kwa kizazi kilichozaliwa baada ya uhuru na muungano.

Ni miaka ambayo naweza kuiita kama maneno yale ya wimbo kuwa ni miaka ya “utukufu wa chama”.

Miaka hii iliyopita ni miaka ambayo Chama cha Mapinduzi kimetukuzwa kuliko chama kingine chochote kile ni miaka ambayo kama ni kuwa kileleni basi CCM ilikuwa juu ya kilele cha vilele vyote. Ndiyo! Ni miaka ambayo Tanzania bila ya CCM isingeweza kufikirika na viongozi wasio wana CCM wasingeweza kudhaniwa kuwepo! CCM imekuja, tumekiona, tumeifurahia, tumeichoka, na sasa taratibu tumeanza kuikataa! Tumeanza kuangalia mwanga mpya.

Imekuja kwa sababu ilikuwa ni lazima. Nchi yetu isingeweza kuongozwa na vyama viwili tofauti ambavyo vinaunda serikali moja. Kuwepo kwa chama cha ASP kule Zanzibar na TANU huko bara ilikuwa ni kasoro ya kisiasa.

Inawezekana vipi vyama viwili ambavyo vinaongoza serikali tofauti, vyenye katiba tofauti, vyenye mwelekeo tofauti na vyenye historia tofauti vikaweza kutawala nchi moja kwa uzuri? Kwa kipindi kirefu hilo lisingewezekana. Hivyo katika kuhakikisha nchi inakuwa katika uongozi mmoja siyo kimtazamo tu au malengo bali kichama pia vyama vya vya ASP na TANU vilibidi kuungana na kuzaliwa kwa chama “kipya”!

Kwa hakika chama kilichozaliwa kilikuwa ni kipya kwa maana ya kuwa jina, malengo, madhumuni na itikadi yake ilikuwa imenyambulishwa na kufafanuliwa upya.

Hata hivyo chama hicho kilikuwa ni cha watu wale wale!

Kilichobadilisha kimsingi kilikuwa ni nembo, ishara, alama, katiba, sera n.k lakini watu walikuwa ni wale wale; Nyerere wa Tanu akawa Nyerere wa CCM, Jumbe wa ASP akawa Jumbe wa CCM! Kwa maneno mengine kuzaliwa kwa chama kipya kulikuwa ni kuzaliwa kwa chama cha watu wa zamani. Ndiyo kimekuja!

Tumekiona; kwa miaka 32 sasa Watanzania wanakifahamu Chama cha Mapinduzi vizuri zaidi kuliko chama kingine chochote. Ni chama ambacho kwa wengi kimekuwa ni lile “zimwi tulijualo” la kwenye methali.

Wengi wetu tumekubali ukweli wa uwepo wa CCM, tumekumbatia sera na itikadi zake kwani katika maisha yetu hatujui chama kingine ambacho kimeyagusa maisha yetu na ya wazazi wote kama CCM.

Wakati wazee wetu wanakumbuka mambo ya vyama vingine kabla ya 1961 au 1964 wengi ambao wamezaliwa baada ya miaka ya sitini wanajua zaidi CCM kuliko vyama hivyo vingine. Kwao CCM ndio chama ambacho kimeacha alama katika maisha yao.

Hivyo ni chama ambacho watu wamekiona katika mazuri na mabaya, katika heri na shida, katika neema na adha, katika ujazo na upungufu!

Hata wale ambao leo tumegeuka kuwa wakosoaji wakubwa wa chama hiki fikra zetu, mawazo yetu na hata mwamko wetu wa kisiasa umepandikizwa na CCM aidha moja kwa moja au kwa namna nyingine. Nakumbuka mojawapo ya utunzi wangu ambao naukumbuka hadi sasa na ambao bado unarindima katika chembe za ubongo wao ni “Chama cha Mapinduzi Ng'oa eeh, viongozi wazembe sisi wametuchosha, wazembe maofisini; wala rushwa magendo ng’oa eh ng'oa eh!”

Tumeona pia jinsi chama hiki kilivyoshughulikia masuala mbalimbali ya kitaifa, wakati wa vita vya Amin, wakati wa mapungufu ya chakula ya miaka ya 80, kuchafuka kwa hali ya kisiasa Zanzibar, kustaafu kwa Mwalimu, sera za “ruksa” n.k.

Tumeona chama hicho hicho kikijaribu kuenenda na mabadiliko ya kisiasa duniani ya mwanzoni mwa miaka ya 90 na tukaona jinsi kilivyoshughulikia masuala ya kiuchumi ya miaka hiyo na hasa kuvunjwa kwa Azimio la Arusha, kuundwa kwa Azimio la Zanzibar na kuvunjika kwake, na hatimaye ujio wa sera ya “ubinafsishaji” ambao baadaye tumegundua kuwa ulikuwa ni “ujinafsishaji” wa watu wachache!

Tumeona mazuri yake, mapungufu yake, nguvu yake, udhaifu wake na ilipoingia karne hii ya 21 tumeona pia jinsi chama hicho kilivyochafuka na hata kuichafua nchi kwa kushindwa kusimamia hazina zetu na kuwapa funguo wezi hadi kuiba ndani ya ghala la fedha zetu! Haya yote tumeyaona!

Tumeona na kushuhudia ahadi ya mambo mema na ya neema, tumeshuhudia utamu wa ahadi nzuri za maisha yajayo.

Mara karibu zote kwa mamilioni yetu tumeendelea kunasa kwenye ulimbo wa maneno ya wanasiasa wetu na kama vipepeo ambao wamenaswa kwenye utando wa bui bui tumebakia kupiga mbawa zetu kwenye nyavu hizo tukizitikisa na kuzitingisha!

Wenyewe tunaamini tunaleta mabadiliko! Kumbe tunachofanya zaidi ni kumshtua buibui wetu kuwa njaa ikija atukumbuke! Ndiyo tumeyaona!

Tumeifurahia! Ni kweli kwa wengi wetu ambao tumekulia na kunufaika chini ya utawala wa CCM bila ya shaka tumeifurahia.

Tumefurahi tulipopata nafasi za kwenda kusoma bure, tumefurahi tulipopapata ajira kwa ‘undugunaizesheni’, tumefurahia tulipoweza kubebwa na kubebana katika nafasi mbalimbali na kwa muda mrefu tulikuwa kwenye CCM kama kwenye mgongo wa punda. CCM ikatubeba na kutufikisha hapa tulipo.

Katika kufurahia tumefikia mahali pa kukubali na kuamini kwa moyo wote kama alivyosema mwana CCM mmoja, “Ukitaka mambo yako yafanikiwe hamia CCM.”

Katika hili kokoro la CCM limevutia samaki wazuri na wabovu, vigae na maganda ya minazi! Minofu na mapanki!

Watu wameshaamini na kukubali kuwa mambo yako hayawezi kunyooka bila CCM kukuwekea mikono yake ya baraka.

Matokeo yake tumepata watumishi wanafiki, wanasiasa uchwara, viongozi bomu na wafanyabiashara wezi!

Wote hawa kwa fahari na wale walio majasiri na wazalendo wa kweli wote wamejifunga katika “zimwi” walijualo, na kama wadudu kwenye utando wa buibui wamewekwa kiporo kwa siku zijazo.

Na sasa tumeanza kuchoka. Tumeanza kuchoka na uongozi wa kiubabaishaji wenye mfano wa viongozi wababaishaji ambao msingi wao ni kubabaisha, sera zao za kibabaushaji, na maono yao ni ya kibabaishaji!

Tumewachoka viongozi ambao wanasubiri upepo uvume ndiyo waanze kutenda, bila makelele ya wananchi hawatendi, na bila ya kuibuliwa kashfa hawafanyi lolote!

Tumeanza kuchoshwa nao hadi tumefikia mahali ambapo hata wanapojaribu kutuzuga wanajikuta wanakamatana wenyewe kwa wenyewe!

Si umeyaona ya kina Mwangunga!? Huko nyuma ingekuwa ndiyo imetoka hiyo sasa wao wenyewe wanaanza kutafutana uchawi!

Tumeanza kuchoka maneno ya ahadi tupu. Maneno ya neema wakati wa njaa, maneno ya mafanikio wakati wa dhiki na maneno ya kupoza wakati wa maumivu.

Wanashindwa kutupa matumaini kwa matendo yao. Sasa wamefikia mahali pa kufanya mambo ili kutunyamazisha.

“Si unaona wamefikishwa mahakamani,” bila ya kujali wanashtakiwa na nini! Si unaona hadi waliokuwa mawaziri wanasimama Kisutu;” wanasahau tulishaona mawaziri kizimbani huko nyuma! Sasa wamepageuza Keko kuwa mahali pa kusalimia! Wananchi wanaridhika tu kwamba mtu kalala Keko siku moja au siku mbili!

Tumechoka na mazingaombwe tunataka kitu cha kweli!

Taratibu tumeanza kukataa. Kati ya vitu ambavyo bila ya shaka vinawashangaza watawala ni ujasiri wa wananchi kukataa uongozi mbovu.

Zamani watu walikuwa wanakataa pembeni na kunung’unika vijiweni. Zamani watu walikuwa wakisikia kiongozi kakohoa wao wanainamisha vichwa; miaka hiyo wakisema watu wanatetema!

Maskini siku hizo zimetoweka kama ukungu wa alfajiri! Leo wakisema wanatakiwa wapime tena maneno yao!

Wakisema imepaa tunawahoji “kupaa kwenda wapi?” Wakisema waueni wanaoua albino,” tunawaambia, “Wewe nani hadi uamuru watu wavunje sheria!”

Watanzania wanastahili viongozi bora na siyo viongozi; viongozi mikwara! Viongozi ambao wanazingatia sheria, ni wa kweli, wenye kujali hatima ya nchi yetu na ambao wanakumbushwa tena kuwa cheo bado ni dhamana na siyo haki yao wao na watoto wao.

Tumeanza kuona nuru ya mwanga mpya. Ndani ya chama hiki hiki tumeanza kuona nuru mpya. Nuru ambayo huko zamani mwanga wake ulikuwa unafifia kama unawekwa gizani.

Hata wale tuliowadhania kuwa wako gizani na wao sasa wanaanza kujitokeza kuja kwenye mwanga. Nuru hii ni mpya katika CCM.

Hata hivyo nuru na giza havikai pamoja! Uovu na uadilifu haviwezi kukumbatiana; na uongo na ukweli havina ubinamu.

Kama nilivyoandika huko nyuma jibu kubwa la mabadiliko ya kweli ya kisiasa ni kuvunjika na kumeguka kwa CCM.

Hili sitanii. Kama Tanzania kweli inataka kupiga hatua kubwa kimaendeleo, kurudisha nidhamu kazini, kurudisha heshima kwenye utumishi wa umma, kujenga vyombo vya utawala bora, kusimamia viongozi pasipo kusubiri hisani ya rais aliyeko madarakani, kunahitajika upinzani wenye nguvu, wa kweli, na ulio tayari kushika madaraka.

Upinzani ambao unahitajika Tanzania utakuwa ni ule wa watu ambao wanaweza kuliongoza Taifa kuelekea mafanikio.

Upinzani wa aina hiyo bado haupo. Sijasema hawapo wapinzani. Wapo wapinzani wazuri tu na makini, wapo wapinzani wenye uwezo mkubwa wa kuongozi kwani ushahidi upo tayari.

Wapo wapinzani wenye uzalendo wa kweli, na wenye hamu ya kweli ya kuona mafanikio katika taifa letu.

Hata hivyo naamini kitakachobadilika kweli siyo kitakachofanywa na wapinzani hawa bali kitakachofanywa na wana CCM.

Naamini ni lazima kabisa kwa kundi kubwa la wazalendo wa kweli, watu ambao wako tayari kuongoza (hata 2010), walio na maono ya mabadiliko ya kweli, wenye kujiamini kuwa Tanzania kwao ni bora zaidi kuliko wapi waliko.

Watu ambao wanaamini kabisa na wanajijua kuwa wako tayari kuweka rehani majina yao, vyeo vyao, hadhi zao, historia zao na hata hatima yao.

Watu ambao hawataunganishwa na chuki, bali matumaini, hawatatenganishwa na majimbo bali majambo, watu ambao hawatakutanishwa na woga bali ujasiri, na watu ambao watasimama kwa hoja na si vioja!

Kundi hilo lipo. Naamini limekaa ndani kwa muda mrefu lakini sasa limetambua kuwa halina tena cha kupoteza zaidi ya sifa za muda mfupi.

Kundi hili lenye ushawishi mkubwa bila ya shaka litasimama. Ni kundi ambalo halitaongozwa na kisasi cha magazeti au vyombo vya habari.

Litachagua marafiki zake na halitaacha kuchaguliwa maadui zake. Kundi hili litatoka CCM.

Ndiyo litatoka kama kuondoka bila kuaga. Litasimama peke na pweke. Litakuwa tayari kwa lolote lile na kutoka kwenye hilo ndipo naamini chama kipya cha upinzani nchini kitazaliwa.

Sijui kitakuwa ni chama cha aina gani. Sijui kama kitakuwa ni chama kipya kabisa au kitajiunga na vyama vilivyopo, sijui ni kina nani hasa watakuwa ndani ya chama hicho.

Ninachojua ni kitu kimoja. Chama hicho kinahitajika. Chama hicho lengo lake kubwa halitakuwa kuuchukua urais toka kwa Kikwete mwakani, bali kuchukua Bunge toka CCM.

Chama hicho kitaleta mwamko mpya wa kitaifa, kitawaungunisha Watanzania siyo kutokana na chuki bali matumaini.

Kitaleta pambazuko jipya la kitaifa. Kama vile Obama alivyoiamsha Marekani na kuishangaza dunia ndivyo vivyo hivyo chama hicho mbadala wa kweli wa CCM kitasimama kama shujaa vitani na kama nyota gizani!

Mtanzania ukisikia hili limeanza kutimia, ushauri wangu kwako wahi kujiunga nao kwani ndiyo nafasi mpya ya mabadiliko makubwa kabisa ya taifa letu yaja. Ukisikia limeanza kutokea usiwe wa mwisho uwe wa kwanza kusimama mstari.

Kuna wakati wa taifa kubadilisha mwelekeo, kunahitajika mabadiliko makubwa ya kifikra. Yameanza kutokea na ninaona fahari kuwa sehemu yake. Sasa tunaelekea kwenye mabadiliko ya kura!

Siyo kwamba tunakichukia CCM bali tunachukia kile CCM imewakilisha! Siyo kwamba tunawachukia wana CCM wote kwani hatuwezi kufanya hivyo wengine ni wazazi wetu, kaka zetu na ndugu zetu, tunachukia kile CCM imefanya kwa wana na mabinti wa taifa letu na kututaka tuwaimbie sifa.

“Kando ya mito ya Babeli ndiko tulikoketi, tulivitundika vinubi vyetu tukalia. Ndipo wale waliotuchukua utumwa walipotaka tuwaimbie nyimbo. Tutawezaje kuimba nyimbo za Sayuni katika nchi ya ugeni?”! Hivyo ndivyo tunavyojisikia. Wanataka tuwaimbie sifa na shangwe wakati sisi bado tuko katika mateka ya ufisadi!

Ndiyo, upinzani wa kweli utatoka CCM! Utaondoka CCM na kuingia Tanzania. Kwa kadiri CCM inavyoendelea kusimamia Ibara yake ya 15:1 ya Katiba yake na kwa kadiri inaendelea kufuatilia Muongozo wake wa 2002, CCM haiwezi kamwe kuendelea kuwa kiongozi wa taifa letu. Haiwezi kwa sababu haijaweza kubadilika.

Wengi wetu tuliamini kabisa kuwa serikali mpya ya Rais Kikwete itakuja na mabadiliko tuyatakayo.

Wengi wetu tuliamini kuwa wanaoingia ni viongozi bora zaidi. Tuliamini watumishi watapata mwamko mpya wa matumaini. Matokeo yake tumeyaona. Ni wale wale.

Kama upinzani wa kweli hautatoka CCM. Kama utaendelea kubakia ndani humo ukiamini kutoka ndani utaweza kuleta mabadiliko, basi upinzani wa kweli utatoka kwa Watanzania wenyewe.

Sasa hivi tunaona rasharasha zake lakini miezi michache ijayo tutaanza kushuhudia mgongano mpya wa kifikra, mgongano ambao ninaona fahari kuushiriki tena.

Swali kubwa ni kuwa katika mgongano huu wewe utakuwa upande gani? Je, utakuwa tayari kushiriki kuleta mabadiliko tuyatakayo au utabakia kuangalia wengine wakileta mabadiliko uyatamaniyo?

Je, utakuwa upande wa wale wenye kuliamsha taifa kuelekea ujenzi mpya wa taifa la kisasa, au utabakia kukebehi juhudi zao ukiamini kuwa hakuna kinachowezekana?

Je utakuwa ni sehemu ya wale waliosimama kuhesabiwa au utakuwa wale waliochutuma wasihesabiwe? Mimi nimechagua upande, nitakuwa ule wa mabadiliko tuyatakayo.

Ungana na timu ya mabadiliko hayo kwa kuniandikia: Mwanakijiji@mwanakijiji.com Kumbuka katika mabadiliko haya kutokuwa na upande si uchaguzi (neutrality is not an option). Kwani kutokuwa na upande ni uchaguzi wa waoga, na chaguo la wasiojiamini. Watu wasiokuwa na upande ni watu wanaosubiri upepo ili wafuate pa kwenda.

Hawawezi kusimama kwa kanuni zao bali kwa kanuni za wengine. Ni watu hao wasio na upande ndio wametufikisha hapa kwani kwao vikienda wamo, visipokwenda wamo, alimradi wao wamo wamo tu! Hawa ndio maadui wa mabadiliko. Katika yale yanayokuja hawa hawana nafasi tena.
 
Ninawatakia wanachama na wakereketwa wote wa CCM kila la heri kati kusherehekea Miaka 32 ya chama chao.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
 
Last edited:
Napenda kuungana na Wakerekwetwa na wanachama wote wa CCM katika kuadhimisha miaka 32 ya Chama.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi​
 
CCM imejaa mafisadi kupita kiasi na kamwe siamini kama upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM. Kama kweli ingekuwa hivyo basi tungeshaona upinzani huo ndani ya CCM ukishamiri lakini tumeona wale ambao walisimama kidete kupinga yanayojiri ndani ya CCM na kuweka mbele maslahi ya Tanzania kupigwa vita na hatimaye kujinyamazia kimya. Hawa ni akina Kilango, Lazaro, Nnauye na wengineo wachache.
 
Upinzani wa kweli utatokana na CCM kugawanyika kati ya mafisadi na wenye nia njema na TZ.
 
Ninawatakia wanachama wote wa CCM kila la heri kati kusherehekea Miaka 32 ya chama chao.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Is these sincere?
CCM should evaluate what it has done for this nation and what they have done if is worthy those celebrations.
Bad investment policies,health and education to mention but a few.
Corruption has been the order of the day.the poor are getting poorer.We can not go on listening to the economists telling us that people's lives are improving while many Tanzanians are going to bed with empty stomachs.
We the citizens should stop this madness as well as those CCM members with their celebratons coz the money they are playing around with is the taxpayers money!
 
Jamani, upinzani wa kweli utakuja pale viongozi wa vyama vyote watakapo kuwa wale ambao hawajala kiapo cha TANU na CCM (au wale ambao hawajawahi kuwa wanachama wa TANU wala CCM). Kwa sasa hivi ni kujitahidi kubridge hizi generations.

Hawa wote kina Zitto Kabwe, Makabe, Kitila, Halima Mdee, George Kahagwa et al walikuwa chipukizi wa CCM, walikula kiapo...hakuna kitu hapo!
 
Sijasema upinzani wa kweli utatotakana na CCM.. bali UTATOKA CCM... !! angalia matumizi ya maneno!
 
Unaona sasa!!! MANENO YA NYERERE!!! Huyu mzee ni kama MTUME wa Tanzania. Milele tutatumia maneno yake na kumtaja kila linapotokea tatizo. CCM, mhhhhh. Tulilia na CHADEMA ili hata sisi tuwe wanachama na kuhudhuria mikutano hata kama hatupo Dar, ila hadi leo wameingia mitini.

CCM wanatumia hali ngumu ya maisha kuwafanya watu mbumbumbu. Watu wakipata kishati wakati wa uchaguzi wanafurahi sana. Itakuwa bora mabadiliko yakija kabla Tanzania haijaanza kuchimba mafuta. Tukianza kuchimba basi TUMEKWISHA. CCM itakuwa MBOGO. Msaada wetu utabaki mmoja yaani MWISHO WA DUNIA MWAKA 2012, kama unaamini.
 
M. M. Mwanakijiji

1220_D49.jpg

“KUZALIWA kwa chama kipya, tarehe tano mwezi wa pili sabini na saba, eh Mungu kipe baraka!” “Chama chetu Cha Mapinduzi eh chajenga nchi.”

“Ewe chama nguzo yetu, kiongozi wa taifa. “Twalalamika pembeni, Hatupewi madaraka, na huku nyuma nyuma twajiweka, Tutamuongoza nani eeeh.” “Nambari wani eeh, nambari wani CCM!”

Ndiyo, Miaka 32 ya Chama Cha Mapinduzi ndiyo hiyo inayoyoma!

Miaka ambayo kwa hakika imeacha alama ya kudumu katika utawala wa taifa letu. Ni miaka ambayo naweza kuiita ni ya msingi kabisa katika ujenzi wa taifa letu.

Ni miaka ambayo kizazi cha uhuru kimeanza kukabidhi madaraka taratibu kwa kizazi kilichozaliwa baada ya uhuru na muungano.

Ni miaka ambayo naweza kuiita kama maneno yale ya wimbo kuwa ni miaka ya “utukufu wa chama”.

Miaka hii iliyopita ni miaka ambayo Chama cha Mapinduzi kimetukuzwa kuliko chama kingine chochote kile ni miaka ambayo kama ni kuwa kileleni basi CCM ilikuwa juu ya kilele cha vilele vyote. Ndiyo! Ni miaka ambayo Tanzania bila ya CCM isingeweza kufikirika na viongozi wasio wana CCM wasingeweza kudhaniwa kuwepo! CCM imekuja, tumekiona, tumeifurahia, tumeichoka, na sasa taratibu tumeanza kuikataa! Tumeanza kuangalia mwanga mpya.

Imekuja kwa sababu ilikuwa ni lazima. Nchi yetu isingeweza kuongozwa na vyama viwili tofauti ambavyo vinaunda serikali moja. Kuwepo kwa chama cha ASP kule Zanzibar na TANU huko bara ilikuwa ni kasoro ya kisiasa.

Inawezekana vipi vyama viwili ambavyo vinaongoza serikali tofauti, vyenye katiba tofauti, vyenye mwelekeo tofauti na vyenye historia tofauti vikaweza kutawala nchi moja kwa uzuri? Kwa kipindi kirefu hilo lisingewezekana. Hivyo katika kuhakikisha nchi inakuwa katika uongozi mmoja siyo kimtazamo tu au malengo bali kichama pia vyama vya vya ASP na TANU vilibidi kuungana na kuzaliwa kwa chama “kipya”!

Kwa hakika chama kilichozaliwa kilikuwa ni kipya kwa maana ya kuwa jina, malengo, madhumuni na itikadi yake ilikuwa imenyambulishwa na kufafanuliwa upya.

Hata hivyo chama hicho kilikuwa ni cha watu wale wale!

Kilichobadilisha kimsingi kilikuwa ni nembo, ishara, alama, katiba, sera n.k lakini watu walikuwa ni wale wale; Nyerere wa Tanu akawa Nyerere wa CCM, Jumbe wa ASP akawa Jumbe wa CCM! Kwa maneno mengine kuzaliwa kwa chama kipya kulikuwa ni kuzaliwa kwa chama cha watu wa zamani. Ndiyo kimekuja!

Tumekiona; kwa miaka 32 sasa Watanzania wanakifahamu Chama cha Mapinduzi vizuri zaidi kuliko chama kingine chochote. Ni chama ambacho kwa wengi kimekuwa ni lile “zimwi tulijualo” la kwenye methali.

Wengi wetu tumekubali ukweli wa uwepo wa CCM, tumekumbatia sera na itikadi zake kwani katika maisha yetu hatujui chama kingine ambacho kimeyagusa maisha yetu na ya wazazi wote kama CCM.

Wakati wazee wetu wanakumbuka mambo ya vyama vingine kabla ya 1961 au 1964 wengi ambao wamezaliwa baada ya miaka ya sitini wanajua zaidi CCM kuliko vyama hivyo vingine. Kwao CCM ndio chama ambacho kimeacha alama katika maisha yao.

Hivyo ni chama ambacho watu wamekiona katika mazuri na mabaya, katika heri na shida, katika neema na adha, katika ujazo na upungufu!

Hata wale ambao leo tumegeuka kuwa wakosoaji wakubwa wa chama hiki fikra zetu, mawazo yetu na hata mwamko wetu wa kisiasa umepandikizwa na CCM aidha moja kwa moja au kwa namna nyingine. Nakumbuka mojawapo ya utunzi wangu ambao naukumbuka hadi sasa na ambao bado unarindima katika chembe za ubongo wao ni “Chama cha Mapinduzi Ng'oa eeh, viongozi wazembe sisi wametuchosha, wazembe maofisini; wala rushwa magendo ng’oa eh ng'oa eh!”

Tumeona pia jinsi chama hiki kilivyoshughulikia masuala mbalimbali ya kitaifa, wakati wa vita vya Amin, wakati wa mapungufu ya chakula ya miaka ya 80, kuchafuka kwa hali ya kisiasa Zanzibar, kustaafu kwa Mwalimu, sera za “ruksa” n.k.

Tumeona chama hicho hicho kikijaribu kuenenda na mabadiliko ya kisiasa duniani ya mwanzoni mwa miaka ya 90 na tukaona jinsi kilivyoshughulikia masuala ya kiuchumi ya miaka hiyo na hasa kuvunjwa kwa Azimio la Arusha, kuundwa kwa Azimio la Zanzibar na kuvunjika kwake, na hatimaye ujio wa sera ya “ubinafsishaji” ambao baadaye tumegundua kuwa ulikuwa ni “ujinafsishaji” wa watu wachache!

Tumeona mazuri yake, mapungufu yake, nguvu yake, udhaifu wake na ilipoingia karne hii ya 21 tumeona pia jinsi chama hicho kilivyochafuka na hata kuichafua nchi kwa kushindwa kusimamia hazina zetu na kuwapa funguo wezi hadi kuiba ndani ya ghala la fedha zetu! Haya yote tumeyaona!

Tumeona na kushuhudia ahadi ya mambo mema na ya neema, tumeshuhudia utamu wa ahadi nzuri za maisha yajayo.

Mara karibu zote kwa mamilioni yetu tumeendelea kunasa kwenye ulimbo wa maneno ya wanasiasa wetu na kama vipepeo ambao wamenaswa kwenye utando wa bui bui tumebakia kupiga mbawa zetu kwenye nyavu hizo tukizitikisa na kuzitingisha!

Wenyewe tunaamini tunaleta mabadiliko! Kumbe tunachofanya zaidi ni kumshtua buibui wetu kuwa njaa ikija atukumbuke! Ndiyo tumeyaona!

Tumeifurahia! Ni kweli kwa wengi wetu ambao tumekulia na kunufaika chini ya utawala wa CCM bila ya shaka tumeifurahia.

Tumefurahi tulipopata nafasi za kwenda kusoma bure, tumefurahi tulipopapata ajira kwa ‘undugunaizesheni’, tumefurahia tulipoweza kubebwa na kubebana katika nafasi mbalimbali na kwa muda mrefu tulikuwa kwenye CCM kama kwenye mgongo wa punda. CCM ikatubeba na kutufikisha hapa tulipo.

Katika kufurahia tumefikia mahali pa kukubali na kuamini kwa moyo wote kama alivyosema mwana CCM mmoja, “Ukitaka mambo yako yafanikiwe hamia CCM.”

Katika hili kokoro la CCM limevutia samaki wazuri na wabovu, vigae na maganda ya minazi! Minofu na mapanki!

Watu wameshaamini na kukubali kuwa mambo yako hayawezi kunyooka bila CCM kukuwekea mikono yake ya baraka.

Matokeo yake tumepata watumishi wanafiki, wanasiasa uchwara, viongozi bomu na wafanyabiashara wezi!

Wote hawa kwa fahari na wale walio majasiri na wazalendo wa kweli wote wamejifunga katika “zimwi” walijualo, na kama wadudu kwenye utando wa buibui wamewekwa kiporo kwa siku zijazo.

Na sasa tumeanza kuchoka. Tumeanza kuchoka na uongozi wa kiubabaishaji wenye mfano wa viongozi wababaishaji ambao msingi wao ni kubabaisha, sera zao za kibabaushaji, na maono yao ni ya kibabaishaji!

Tumewachoka viongozi ambao wanasubiri upepo uvume ndiyo waanze kutenda, bila makelele ya wananchi hawatendi, na bila ya kuibuliwa kashfa hawafanyi lolote!

Tumeanza kuchoshwa nao hadi tumefikia mahali ambapo hata wanapojaribu kutuzuga wanajikuta wanakamatana wenyewe kwa wenyewe!

Si umeyaona ya kina Mwangunga!? Huko nyuma ingekuwa ndiyo imetoka hiyo sasa wao wenyewe wanaanza kutafutana uchawi!

Tumeanza kuchoka maneno ya ahadi tupu. Maneno ya neema wakati wa njaa, maneno ya mafanikio wakati wa dhiki na maneno ya kupoza wakati wa maumivu.

Wanashindwa kutupa matumaini kwa matendo yao. Sasa wamefikia mahali pa kufanya mambo ili kutunyamazisha.

“Si unaona wamefikishwa mahakamani,” bila ya kujali wanashtakiwa na nini! Si unaona hadi waliokuwa mawaziri wanasimama Kisutu;” wanasahau tulishaona mawaziri kizimbani huko nyuma! Sasa wamepageuza Keko kuwa mahali pa kusalimia! Wananchi wanaridhika tu kwamba mtu kalala Keko siku moja au siku mbili!

Tumechoka na mazingaombwe tunataka kitu cha kweli!

Taratibu tumeanza kukataa. Kati ya vitu ambavyo bila ya shaka vinawashangaza watawala ni ujasiri wa wananchi kukataa uongozi mbovu.

Zamani watu walikuwa wanakataa pembeni na kunung’unika vijiweni. Zamani watu walikuwa wakisikia kiongozi kakohoa wao wanainamisha vichwa; miaka hiyo wakisema watu wanatetema!

Maskini siku hizo zimetoweka kama ukungu wa alfajiri! Leo wakisema wanatakiwa wapime tena maneno yao!

Wakisema imepaa tunawahoji “kupaa kwenda wapi?” Wakisema waueni wanaoua albino,” tunawaambia, “Wewe nani hadi uamuru watu wavunje sheria!”

Watanzania wanastahili viongozi bora na siyo viongozi; viongozi mikwara! Viongozi ambao wanazingatia sheria, ni wa kweli, wenye kujali hatima ya nchi yetu na ambao wanakumbushwa tena kuwa cheo bado ni dhamana na siyo haki yao wao na watoto wao.

Tumeanza kuona nuru ya mwanga mpya. Ndani ya chama hiki hiki tumeanza kuona nuru mpya. Nuru ambayo huko zamani mwanga wake ulikuwa unafifia kama unawekwa gizani.

Hata wale tuliowadhania kuwa wako gizani na wao sasa wanaanza kujitokeza kuja kwenye mwanga. Nuru hii ni mpya katika CCM.

Hata hivyo nuru na giza havikai pamoja! Uovu na uadilifu haviwezi kukumbatiana; na uongo na ukweli havina ubinamu.

Kama nilivyoandika huko nyuma jibu kubwa la mabadiliko ya kweli ya kisiasa ni kuvunjika na kumeguka kwa CCM.

Hili sitanii. Kama Tanzania kweli inataka kupiga hatua kubwa kimaendeleo, kurudisha nidhamu kazini, kurudisha heshima kwenye utumishi wa umma, kujenga vyombo vya utawala bora, kusimamia viongozi pasipo kusubiri hisani ya rais aliyeko madarakani, kunahitajika upinzani wenye nguvu, wa kweli, na ulio tayari kushika madaraka.

Upinzani ambao unahitajika Tanzania utakuwa ni ule wa watu ambao wanaweza kuliongoza Taifa kuelekea mafanikio.

Upinzani wa aina hiyo bado haupo. Sijasema hawapo wapinzani. Wapo wapinzani wazuri tu na makini, wapo wapinzani wenye uwezo mkubwa wa kuongozi kwani ushahidi upo tayari.

Wapo wapinzani wenye uzalendo wa kweli, na wenye hamu ya kweli ya kuona mafanikio katika taifa letu.

Hata hivyo naamini kitakachobadilika kweli siyo kitakachofanywa na wapinzani hawa bali kitakachofanywa na wana CCM.

Naamini ni lazima kabisa kwa kundi kubwa la wazalendo wa kweli, watu ambao wako tayari kuongoza (hata 2010), walio na maono ya mabadiliko ya kweli, wenye kujiamini kuwa Tanzania kwao ni bora zaidi kuliko wapi waliko.

Watu ambao wanaamini kabisa na wanajijua kuwa wako tayari kuweka rehani majina yao, vyeo vyao, hadhi zao, historia zao na hata hatima yao.

Watu ambao hawataunganishwa na chuki, bali matumaini, hawatatenganishwa na majimbo bali majambo, watu ambao hawatakutanishwa na woga bali ujasiri, na watu ambao watasimama kwa hoja na si vioja!

Kundi hilo lipo. Naamini limekaa ndani kwa muda mrefu lakini sasa limetambua kuwa halina tena cha kupoteza zaidi ya sifa za muda mfupi.

Kundi hili lenye ushawishi mkubwa bila ya shaka litasimama. Ni kundi ambalo halitaongozwa na kisasi cha magazeti au vyombo vya habari.

Litachagua marafiki zake na halitaacha kuchaguliwa maadui zake. Kundi hili litatoka CCM.

Ndiyo litatoka kama kuondoka bila kuaga. Litasimama peke na pweke. Litakuwa tayari kwa lolote lile na kutoka kwenye hilo ndipo naamini chama kipya cha upinzani nchini kitazaliwa.

Sijui kitakuwa ni chama cha aina gani. Sijui kama kitakuwa ni chama kipya kabisa au kitajiunga na vyama vilivyopo, sijui ni kina nani hasa watakuwa ndani ya chama hicho.

Ninachojua ni kitu kimoja. Chama hicho kinahitajika. Chama hicho lengo lake kubwa halitakuwa kuuchukua urais toka kwa Kikwete mwakani, bali kuchukua Bunge toka CCM.

Chama hicho kitaleta mwamko mpya wa kitaifa, kitawaungunisha Watanzania siyo kutokana na chuki bali matumaini.

Kitaleta pambazuko jipya la kitaifa. Kama vile Obama alivyoiamsha Marekani na kuishangaza dunia ndivyo vivyo hivyo chama hicho mbadala wa kweli wa CCM kitasimama kama shujaa vitani na kama nyota gizani!

Mtanzania ukisikia hili limeanza kutimia, ushauri wangu kwako wahi kujiunga nao kwani ndiyo nafasi mpya ya mabadiliko makubwa kabisa ya taifa letu yaja. Ukisikia limeanza kutokea usiwe wa mwisho uwe wa kwanza kusimama mstari.

Kuna wakati wa taifa kubadilisha mwelekeo, kunahitajika mabadiliko makubwa ya kifikra. Yameanza kutokea na ninaona fahari kuwa sehemu yake. Sasa tunaelekea kwenye mabadiliko ya kura!

Siyo kwamba tunakichukia CCM bali tunachukia kile CCM imewakilisha! Siyo kwamba tunawachukia wana CCM wote kwani hatuwezi kufanya hivyo wengine ni wazazi wetu, kaka zetu na ndugu zetu, tunachukia kile CCM imefanya kwa wana na mabinti wa taifa letu na kututaka tuwaimbie sifa.

“Kando ya mito ya Babeli ndiko tulikoketi, tulivitundika vinubi vyetu tukalia. Ndipo wale waliotuchukua utumwa walipotaka tuwaimbie nyimbo. Tutawezaje kuimba nyimbo za Sayuni katika nchi ya ugeni?”! Hivyo ndivyo tunavyojisikia. Wanataka tuwaimbie sifa na shangwe wakati sisi bado tuko katika mateka ya ufisadi!

Ndiyo, upinzani wa kweli utatoka CCM! Utaondoka CCM na kuingia Tanzania. Kwa kadiri CCM inavyoendelea kusimamia Ibara yake ya 15:1 ya Katiba yake na kwa kadiri inaendelea kufuatilia Muongozo wake wa 2002, CCM haiwezi kamwe kuendelea kuwa kiongozi wa taifa letu. Haiwezi kwa sababu haijaweza kubadilika.

Wengi wetu tuliamini kabisa kuwa serikali mpya ya Rais Kikwete itakuja na mabadiliko tuyatakayo.

Wengi wetu tuliamini kuwa wanaoingia ni viongozi bora zaidi. Tuliamini watumishi watapata mwamko mpya wa matumaini. Matokeo yake tumeyaona. Ni wale wale.

Kama upinzani wa kweli hautatoka CCM. Kama utaendelea kubakia ndani humo ukiamini kutoka ndani utaweza kuleta mabadiliko, basi upinzani wa kweli utatoka kwa Watanzania wenyewe.

Sasa hivi tunaona rasharasha zake lakini miezi michache ijayo tutaanza kushuhudia mgongano mpya wa kifikra, mgongano ambao ninaona fahari kuushiriki tena.

Swali kubwa ni kuwa katika mgongano huu wewe utakuwa upande gani? Je, utakuwa tayari kushiriki kuleta mabadiliko tuyatakayo au utabakia kuangalia wengine wakileta mabadiliko uyatamaniyo?

Je, utakuwa upande wa wale wenye kuliamsha taifa kuelekea ujenzi mpya wa taifa la kisasa, au utabakia kukebehi juhudi zao ukiamini kuwa hakuna kinachowezekana?

Je utakuwa ni sehemu ya wale waliosimama kuhesabiwa au utakuwa wale waliochutuma wasihesabiwe? Mimi nimechagua upande, nitakuwa ule wa mabadiliko tuyatakayo.

Ungana na timu ya mabadiliko hayo kwa kuniandikia: Mwanakijiji@mwanakijiji.com Kumbuka katika mabadiliko haya kutokuwa na upande si uchaguzi (neutrality is not an option). Kwani kutokuwa na upande ni uchaguzi wa waoga, na chaguo la wasiojiamini. Watu wasiokuwa na upande ni watu wanaosubiri upepo ili wafuate pa kwenda.

Hawawezi kusimama kwa kanuni zao bali kwa kanuni za wengine. Ni watu hao wasio na upande ndio wametufikisha hapa kwani kwao vikienda wamo, visipokwenda wamo, alimradi wao wamo wamo tu! Hawa ndio maadui wa mabadiliko. Katika yale yanayokuja hawa hawana nafasi tena.

Mkuu Mwanakijiji, maneno yako hapo juu yanatoa hamasa mpya na yenye matumaini. Ila maswali ya kujiuliza ni kwamba, chama hicho au harakati hizo zimeshaanza? Kama hazijaanza, zinaanza lini? Nani hasa wanaoaminika kutuletea matumaini hayo? Chama hicho kinasimamia misingi ipi? Nikipata majibu ya maswali hayo, nitakuwa mmoja wa watakaotuma ujumbe kwenye address uliyoiweka hapo, haraka sana.

Mkuu, hadi sasa uongozi wa nchi hauna misingi inayosimamia. Walau wakati wa Nyerere tulisimamia Ujamaa na Kujitegema, japokuwa uli-fail. Tangu siasa hiyo/misingi hiyo ivunjwe bila taarifa, hatujawa na misingi mbadala. Na sioni dalili za kuwepo misingi mbadala kutoka angle yoyote. Ni kweli kwamba umefika wakati ambapo inabidi tuweke misingi inayokubalika kwa ustawi wa nchi yetu. Minsingi hiyo inatakiwa iwe inabuniwa kwa uangalifu na inayozingatia hali halisi ya nchi yetu. La sivyo, kila atakaeongoza nchii hii, atakuja na sera zake ambazo wala hazieleweki ama zikieleweka zitakuwa hazitekelezeki.
 
Is these sincere?
CCM should evaluate what it has done for this nation and what they have done if is worthy those celebrations.
Bad investment policies,health and education to mention but a few.
Corruption has been the order of the day.the poor are getting poorer.We can not go on listening to the economists telling us that people's lives are improving while many Tanzanians are going to bed with empty stomachs.
We the citizens should stop this madness as well as those CCM members with their celebratons coz the money they are playing around with is the taxpayers money!

Kevo,
Mimi ni muumini wa utawala wa demokrasia na sintosita kuwapongeza CCM pale wanapopiga hatua muhimu ya kujivunia katika Chama chao. Siasa si uadui, tuwapongeze na tuwakosoe pale inapobidi.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUUUUUZI!!!!!!!
 
Umri wa miaka 32, ni wa mtu ambaye anaweza kuwa kasoma mpaka kupata PhD, kuwa na familia nk. Ukiona mtu ana miaka 32 na hajui wanae awahudumie vipi, anauza mashamba, kupangisha nyumba za familia ili akapige ulabu, anaajiri jirani kwenye kazi zake na wanae hawana kazi, hawahudumii wanawe wakiugua lakini yeye akiugua anaenda kutibiwa nje ya nchi kama Afrika ya kusini, India (Apolo), UK nk. Basi huyo ni JUHA.
 
Upinzani wa kweli utatokana na CCM kugawanyika kati ya mafisadi na wenye nia njema na TZ.

Hii si concept nzuri kwa mitazamo ya fikra mbadala. Let other people struggle kwa kuleta fikra mbadala za kweli na wala siyo kutegemea kazi iliyokwishafanywa na CCM.

Kazi ya kujenga upinzani katika mfumo wa utawala wa kidemokrasia siyo lelemama na hakuna short-cut. CCM itaondoka madarakani pale tu wananchi watakapoamua kupitia box la kura na wala si utashi wa viongozi.

Mimi bado ninaiona CCM iko imara kwani kuna watu (vijana kwa wanawake) wengi wasafi, makini zaidi ya baadhi ya wale wanaongoza sasa hivi, ambao ni CCM damu kabisa.
 
kwa mfano sasa hivi atoke malecela,kinana na watu wao huko ndani ya ccm kwa nia thabiti kabisa kuwa wamechoka kuburuzwa na mtandao wa lowasa na mwaka 2010 watamsimamisha dr salim against kikwete au yeyote katika katika nafasi ya urais kwenye vikao vyao vya mchujo.
hivi ccm haitagawanyika?
ikishagawanyika,hautapatikana upinzani wa kweli tanzania?
 
Umri wa miaka 32, ni wa mtu ambaye anaweza kuwa kasoma mpaka kupata PhD, kuwa na familia nk. Ukiona mtu ana miaka 32 na hajui wanae awahudumie vipi, anauza mashamba, kupangisha nyumba za familia ili akapige ulabu, anaajiri jirani kwenye kazi zake na wanae hawana kazi, hawahudumii wanawe wakiugua lakini yeye akiugua anaenda kutibiwa nje ya nchi kama Afrika ya kusini, India (Apolo), UK nk. Basi huyo ni JUHA.

Chama Cha Mapinduzi ndiyo chama pekee chenye dhamana ya kuendesha serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Kwa hiyo basi, majukumu ya vyama vya siasa vyote vilivyopo Tanzania kwa sasa hayawezi kuwa sawasawa na yale ambayo CCM inayo. Kwa mazingira ya nchi zetu za kiafrika (bila ya kuiondoa Tanzania) hali zetu za kimaisha zinafanana kwa maana hali za kiuchumi ni zilezile za nchi zinazoendelea. CCM ina kazi ya kuhakikisha inatimiza ilani yake uchaguzi ambayo ndiyo mkataba wa ajira yake kati yake na wananchi. Imekuwa ikifanya hivyo kwa wakati wote licha ya kukabiliwa na hali ngumu za kiuchumi zinazosababishwana mambo ambayo yako nje ya uwezo wake. Kwa mfano hali ngumu ya kiuchumi duniani hili liko nje ya uwezo wa CCM.
Lakini pia wakati wakutekeleza majukumu yake makubwa ya kuendesha serikali inakumbana na matatizo ambayo kwa hakika inajitahidi kuyaweka sawa kwa manufaa ya nchi na wala siyo CCM. Kwa mfano, kitendo cha kupambana na rushwa, hatua ambazo zimechukuliwa na zinazoendelea kuchukuliwa hatuna budi kuipongeza serikali ili ipate nguvu zaidi ya kuongeza mapambano dhidi ya rushwa. Hatua zinazochukuliwa kuhakikisha kuwa kunakuwa na usalama ambao utawawezesha wananchi walau waweze kuamka na kufanya shughuli zao za kila siku bila ya bugdha.
Kuimarisha mapambano dhidi ya vifo vya watoto wadogo wenye umri chini ya miaka mitano.
Kupunguza vifo vya akina mama wajawazito.
Kuongeza vyumba vya madarasa kwa ajili ya watoto wetu nk.

Kazi hii ya CCM si kazi ndogo, ni kazi kubwa kabisa ambayo inafanyika kwa kuzingatia ilani ya uchaguzi.

Leo ninafuraha sana kuona uhuru wa kujieleza ndani ya nchi yetu umepanuka na ni wa mfano wa kupigiwa mstari barani Afrika. Nimefurahi kuona kuwa maneno aliyoyatoa Mh Kikwete wakati wa kuzindua bunge, kuwa atahakikisha kuwa vyama vya upinzani vinapata nafasi ya kuweza kufanya kazi vyema ndani ya kipindi cha utawala wake yametimizwa. Wabunge wa upinzani sasa hivi wana uhuru mkubwa wakufanya kazi zao bungeni kuliko wakati mwingine wowote.

Kazi ya CCM ya kuhakikisha vyama vya upinzani vinalelewa vyema na serikali yake nayo pia ni mfano wa kuigwa.

Tuendelee kuisifu na kuikosoa CCM pale inapobidi.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
 
kwa mfano sasa hivi atoke malecela,kinana na watu wao huko ndani ya ccm kwa nia thabiti kabisa kuwa wamechoka kuburuzwa na mtandao wa lowasa na mwaka 2010 watamsimamisha dr salim against kikwete au yeyote katika katika nafasi ya urais kwenye vikao vyao vya mchujo.
hivi ccm haitagawanyika?
ikishagawanyika,hautapatikana upinzani wa kweli tanzania?

Whoever ambaye atatoka CCM, in short hakuwa Mwana-CCM halisi na hapo ndiyo utakuwa wakati mwafaka kubakiwa na wanaCCM wa kweli
 
Chama Cha Mapinduzi ndiyo chama pekee chenye dhamana ya kuendesha serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kwa mazingira ya nchi zetu za kiafrika (bila ya kuiondoa Tanzania) hali zetu za kimaisha zinafanana kwa maana hali za kiuchumi ni zilezile za nchi zinazoendelea.

Unataka sema kama hali zetu ni sawa na nchi zingine zinazoendelea basi ndio kipimo kuwa hakuna kasoro za uongozi wa CCM. Namibia, Botswana tuko sawa?

CCM ina kazi ya kuhakikisha inatimiza ilani yake uchaguzi ambayo ndiyo mkataba wa ajira yake kati yake na wananchi. Imekuwa ikifanya hivyo kwa wakati wote licha ya kukabiliwa na hali ngumu za kiuchumi zinazosababishwana mambo ambayo yako nje ya uwezo wake. Kwa mfano hali ngumu ya kiuchumi duniani hili liko nje ya uwezo wa CCM.
Hali ngumu ya uchumi duniani ilianza lini?, unataka kusema huu mtikisiko wa kiuchumi una miaka 32?.

Lakini pia wakati wakutekeleza majukumu yake makubwa ya kuendesha serikali inakumbana na matatizo ambayo kwa hakika inajitahidi kuyaweka sawa kwa manufaa ya nchi na wala siyo CCM. Kwa mfano, kitendo cha kupambana na rushwa, hatua ambazo zimechukuliwa na zinazoendelea kuchukuliwa hatuna budi kuipongeza serikali ili ipate nguvu zaidi ya kuongeza mapambano dhidi ya rushwa. Hatua zinazochukuliwa kuhakikisha kuwa kunakuwa na usalama ambao utawawezesha wananchi walau waweze kuamka na kufanya shughuli zao za kila siku bila ya bugdha.
Kuimarisha mapambano dhidi ya vifo vya watoto wadogo wenye umri chini ya miaka mitano.Kupunguza vifo vya akina mama wajawazito.Kuongeza vyumba vya madarasa kwa ajili ya watoto wetu nk.Kazi hii ya CCM si kazi ndogo, ni kazi kubwa kabisa ambayo inafanyika kwa kuzingatia ilani ya uchaguzi.

Hizo hatua ni kazi na majukumu ya Chama chochote tawala, ni lazima wafanye.

Leo ninafuraha sana kuona uhuru wa kujieleza ndani ya nchi yetu umepanuka na ni wa mfano wa kupigiwa mstari barani Afrika.

Gazeti la Mwanahalisi la Kubenea!!!???.
Taifa Huru la Mohamed Seif Khatib!!!???.

Nimefurahi kuona kuwa maneno aliyoyatoa Mh Kikwete wakati wa kuzindua bunge, kuwa atahakikisha kuwa vyama vya upinzani vinapata nafasi ya kuweza kufanya kazi vyema ndani ya kipindi cha utawala wake yametimizwa. Wabunge wa upinzani sasa hivi wana uhuru mkubwa wakufanya kazi zao bungeni kuliko wakati mwingine wowote.
Hapa sikatai, wana uhuru kiasi fulani (kiasi nikikumbuka suala kama la kufungiwa Zito).

Kazi ya CCM ya kuhakikisha vyama vya upinzani vinalelewa vyema na serikali yake nayo pia ni mfano wa kuigwa. Tuendelee kuisifu na kuikosoa CCM pale inapobidi.
Haya ndio maneno.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom