Miaka 125 ya Jumba la Maajabu...

Kibunango

Platinum Member
Aug 29, 2006
8,416
2,264
Leo ni miaka 125 ya Jumba la Maajabu huko Zenj... Karibuni katika sherehe hii adhimu! Bonyeza hapa kwa detail. sherehe hizi zitadumu kwa mwezi mmoja..
 
Kamanda tembelea hapa kwa majibu ya swali lako...

Nimetembelea blog yako na kukutana na maneno haya yafuatayo:

Nanukuu... Wataalamu wa histori ya Zenj wanasema umarufu wa jengo hilo umejengwa kwa sifa zifuatazo;-
1. Ni jumba la kwanza Afrika ya Mashariki kuwa na Umeme.
2. Ni jumba la kwanza Afrika ya Mashariki kuwa na lifti( elevator)
3. Ni jumba la kwanza Afrika ya Mashariki kuwa na mfereji ndani ya nyumba( Bomba la maji)...
mwisho wakunukuu.

Je hayo ndo kweli yamesababisha kuwa jumba hilo kuwa la maajabu mpaka hivi leo?

Hivi unamchukuwa mtoto wako aliye zaliwa karne hii na kumpekeleka hapo kisha unamfahamisha kuwa hili ni jumba la maajabu, atakuelewa kweli? Kisa ni jumba la kwanza Afrka mashariki (wengine wanasema in Sub-Sahara Africa)kuwa na umeme, lift na bomba la maji ndani.

Kwani haitoshi tu kuelezea kuwa ni Jumba la kwanza Afrika mashariki kuwa na vitu hivyo mpaka tuongeze neno maajabu? Labda nashindwa kuelewa neno maajabu katika karne hii tulikuwa nayo sasa...!

Anyway ahsante mkuu kwa taarifa yako...! Nikipata nafasi nitatembelea tena Jumba hilo linaloitwa Beit al Ajaib...!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom