EJM_
JF-Expert Member
- Jul 8, 2011
- 3,836
- 2,091
Jana tumeadhimisha miaka 12 tangu kifo cha baba wa Taifa Mwl. JK Nyerere. Kumefanyika sherehe kubwa pale Butiama zilizoambatana na kuwashwa kwa mwenge, pia kukawa na midahalo mbalimbali yote ikiwa na lengo la kutathmini na kurudia yale yote ambayo Mw. Nyerere aliyaamini.
Baada ya kuangalia sana yote hayo hii ndio tathmini yangu;
Mtazamo juu ya Mwl. Nyerere
Kwa mara ya kwanza mwaka huu nimeona watu wakiweza kutamka mapungufu ya mwalimu katika uongozi wake, kwa muono wangu hili ni jambo jema sana kama ni kweli lina lengo la kuweka kumbukumbu sawa na kutusaidia hasa sisi vijana kujifunza jambo kutokana na hiyo. Lakini kama ni kwasababu sasa watu wanataka kuhalalisha uozo wanaoufanya sasa kwa kusema hata mwalimu pia alikuwa anakosea naona ni mbinu ya kinafiki ambayo tunatakiwa tuepukane nayo.
Mtazamo wa Mwl. Nyerere juu ya viongozi bora
Katika hotuba yake ya uchaguzi wa mgombea wa uraisi wa CCM wa mwaka 1995 mwalimu aliwahi kusema maneno haya "Lazima tukubali kwamba ni kweli kiongozi wa nchi hii anaweza kutoka nje ya CCM, lakini mimi naamini kiongozi bora ni lazima atoke ndani ya CCM" lakini akaendelea kusema kwamba kiongozi huyo pamoja na kuwa anatoka ndani ya CCM lazima awe na sifa kuu nne,
Viongozi na unafiki wa kumuenzi mwalimu
Imekuwa desturi sasa kwa viongozi kila 14 October kwenda Butiama na kujifanya wanamuenzi mwalimu. Tukiwa wakweli tutagundua kuwa kwa sasa hakuna kiongozi yoyote wa juu nchi hii anayemuongelea Mwalimu Nyerere kwa falsafa yake hata mmoja, kwanini? Sababu ni kwamba hakuna mtu anayefuata falsafa hiyo na kwasababu wanajua kuwa watanzania wengi bado wanaamini mwalimu ndiye alikuwa kiongozi bora na si bora kiongozi kama ilivyo sasa, hawathubutu kumpinga kwakuwa wanajua wataishia kupigwa mawe.
Tathmini yangu
Nchi yetu imekosa mwelekeo kwa kuwa tumekosa nahodha, sitaki kusema tunahitaji nahodha kutoka upinzani au CCM bali tunahitaji nahodha anayejua mahitaji yetu kwa sasa na kuendelea mbele. Sera ya Ubepari imeshindwa si tu Tanzania au Afrika pekee bali dunia nzima (mfano ni Ugiriki, Italia, Hispania na nchi nyingine za ulaya) tazama mtikisiko wa kiuchumi ulioipata Dunia ambao kimsingi uliletwa na sera hizi za kibepari, kama nchi hebu turudi na tuamue ni namna gani tunaenda mbele na sio kusubiri watu wengine watuamulie namna ya kuishi.
Mwalimu alipinga sana rushwa, kwa sasa sio tena rushwa ni wizi na kibaya hao wezi hawashughulikiwi kwasababu huenda wakawa wanakula wizi na wanaotakiwa kuwashughulikia au ni marafiki zao hivyo wanaoneana haya. Tumekuwa nchi ya walalamikaji, juzi nimemsikia jaji Warioba akisema kuwa tumekuwa taifa la walalamikaji, cha kuchekesha ni kwamba hata yeye pia alikuwa anawalalamikia hao wanaolalamika (kila mtu ni mlalamikaji)
Zamani tulikuwa tunatarajia majibu kutoka kwa viongozi na ndipo tunapommiss zaidi mwalimu. Leo hata raisi pia analalamika tena anawalalamikia watu wake wa kumsaidia kuwa hawafanyi kazi na anatulalamikia sisi sijui tumsaidieje! Mwisho sitaki mchukue muda mrefu kusoma haya, kama nchi tunahitaji kufanya review kama nchi na kuachana na habari za nani kasema nini na kamlaumu nani.......
Karibuni..........

- Apingane na rushwa kwa nguvu zake zote
- Ajue kuwa nchi hii inaundwa na wakulima na wafanyakazi ambao ni masikini hivyo ajue ni namna gani atawatoa kwenye umasikini
- Asiwe na Udini
- Asiwe mkabila