Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mia imeenda wapi

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by ARV, Oct 13, 2011.

 1. ARV

  ARV JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2011
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 1,100
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  CHEMSHA AKILI.
  Nguo inauzwa sh. 10,000 we huna pesa, ukaamua kukopa kwa dada yako sh. 5000 na kwa kaka sh. 5000 ukapata sh. 10,000. Ukaenda kugalaliza na kununua kwa sh. 9,700 ukarudishiwa sh. 300. Ukaamua kupunguza deni. Ukatoa sh. 100 kwa kaka na 100 kwa dada, ukabaki na 100. Hivyo ikawa una deni kwa kaka 4900 na dada anadai 4900, ukijumlisha ya kaka 4900 na dada 4900 unapata 9800 Ukiongeza na ile 100 ya kwako, inakua 9900. Je, 100 imekwenda wapi?
   
 2. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,533
  Likes Received: 117
  Trophy Points: 160
  ukae ukijua hapo imebakia ile mia ulioichukua wewe..
   
 3. ARV

  ARV JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2011
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 1,100
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Nadhani hujasoma vizuri. Sentensi hii hujaiona? 'ukiongeza na ile mia inakuwa 9900'

   
 4. J

  JF2050 JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0

  Ahsante kwa swali lako ARV, Jibu ni kama ifuatavyo:

  Nimekopa kwa dada sh. 5000 na kwa kaka sh.5000, kwa hiyo nadaiwa sh. 10000. Nikinunua nguo kwa sh. 9700, nabakiwa na sh. 300. Nikaamua kumrudishia dada sh. 100 na kaka sh. 100. Kwa hiyo dada bado ananidai sh. 4900 na kaka sh. 4900, jumla nadaiwa sh. 9800 ambazo ni sawasawa na 9700 niliyonunulia nguo + 100 niliyobaki nayo.


  Kwa maana nyingine: Nikinunua nguo nabakiwa na sh. 300 lakini nadaiwa sh. 10000, nikitoa sh. 200, yaani mia kwa dada na mia kwa kaka, nabaki na deni la sh. 9800. Kwa hiyo ukitaka iwe 10000, chukua deni la sh. 9800 ninalodaiwa, kisha jumlisha na mia mbili ambayo nimekwishalipa, yaani, sh. 9800, deni + sh. 200 ambayo nimelipa, jumla = sh. 10000.

  Kuna namna nyingi za kujibu swali hili, naona niishie hapa.
   
 5. J

  JF2050 JF-Expert Member

  #5
  Oct 13, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kwa maana hiyo ARV, mia nimebaki nayo kwa sababu hesabu niliyoifanya hapo juu inaonyesha bado nadaiwa sh. 9800. Ili nisiwe na hiyo mia nilitakiwa kubaki na deni la sh. 9700 tu ambayo ni hela niliyonunulia nguo. Rejea hesabu hapo juu.
   
 6. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #6
  Oct 13, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,448
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  sh.100 ya kwako unajumlisha ya kazi gani? Unadaiwa sh. 9800 kwa sababu ulilipa sh. 200 katika sh. 10,000 uliyokopeshwa. Hapo hakuna sh. 100 isiyoonekana, kosa ulilofanya unajumlusha asset na liabilities kwa pamoja wakati ni vitu viwili tofauti.

  Ni kaquiz kazuri kama hujasoma btn the lines.
   
 7. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #7
  Oct 13, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,448
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  kwa hiyo hiyo equation ina balance kama ifuatavyo;

  on the asset side kuna cash on hand sh. 100 na nguo uliyonunua (stock) sh. 9,700 total sh. 9,800.

  On the liabilities side kuna deni la dada sh. 4,900 na deni la kaka sh. 4,900 jumla ni sh. 9,800. So mizania yetu imebalance, na hakuna mia inayopungua au kuzidi sehemu.
   
 8. A

  Alexism JF-Expert Member

  #8
  Oct 13, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 1,211
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  25/5 =14
  14x5=20+5=25
  14+14+14+14+14=25
  :. 14
  14
  14
  14
  +14=25
   
 9. v

  valid statement JF-Expert Member

  #9
  Oct 13, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 2,723
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  hayo ni mahesabu ya theory, kakope kweli, na urudishe ivo.wala mia haitapotea.
   
 10. J

  JF2050 JF-Expert Member

  #10
  Oct 13, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hii ipo kama abstract algebra!
   
 11. ARV

  ARV JF-Expert Member

  #11
  Oct 13, 2011
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 1,100
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Ahsanteni wandugu,Hapo sasa nimeelewa.kumbe njia rahisi ni kuweka upande mmoja wa assets na mwingine wa liabilities,halafu inabalance kiulaini. Aksanteni ilinisumbua sana hii kitu.
   
 12. O

  Old Moshi Senior Member

  #12
  Oct 13, 2011
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  jibu sahihi ni hili hapa. Sh 100 ipo ktk sh9700 uliyonunulia nguo. Ikiwa umepunguza deni na kua sh9800, sh100 uliyobakiwa nayo na sh 100 iliyopo kwenye sh 9700 zitafanya jumla ya sh 10000. Sijui nimeeleweka!
   
Loading...