Mi nilishindwa sijui nyie.

Kwa nini mnapenda kulazimishia watu marafiki? yaani uporoto 01 ameishiwa marafiki mpaka lazima na urafiki na huyo mwanamke? humu inaonekana wengine bado wadogo haya mambo yanakera na yanauma kuliko unavyoweza kuamini, maana mtu unaweza ukawa umejitoa muhanga na kudevort ur time kwa ajili mapenzi na huenda hata ndugu zako wengine mlikosana kwa ajili ya mapenzi then demu anakuzinguwa eti baadae unasema tuwe marafiki?
Naona mnaleta mzaha wa makusudi.
Hakuna hata aliyelazimisha urafiki ndio maana hujapangiwa marafiki na mtu ni wewe tu na moyo wako, u make ur own choices na wengine wana make their choices, wewe kama unakerwa na moyo wako unauma sana pole but still hakuna tatizo mtu akiamua kuwa rafiki wa Ex wake
 
badly,kisa chenyewe kilikuwa hivi kuna mzee wa kihindi alikuwa boss wake akawaita wafanyakazi wake(sita) na kuwaambia yeye anafunga ofisi na kuhamia Canada,na kwakuwa wamemfanyia kazi nzuri atawakopesha kila mmoja milioni 20 za kufanyia biashara ambazo anataka warudishe baada ya miaka mitano bila riba yoyote. Sasa bibie akaingia tamaa akaona anaweza kupata zaidi kama atamliwaza mzee wa watu na labda hata kusamehewa kulipa hiyo mil 20.
Akaniacha na kuanza kumfukuzia mzee wa watu lakini mzee akamtolea nje kwamba hahitaji mpenzi ana mke na watoto anachotaka wafanyakazi waendelee na kurudisha mkopo KWISHA KAZI.Baada ya muda akataka kurudi nikamtolea nje na sasa baada ya muda ndio anataka tuwe marafiki. Kibiashara kaendelea kidogo ana gari na vi-boutique viwili na anajenga nyumba yake kwa sasa.
Oh! so hivi ndio ilivyokuwa, atleast umeweka bayana kile kilichotokea ili wachangiaji wawe na uwanja mpana zaidi
 
Mkuu labda tuambie faida za kuwa maadui baada ya mapenzi kuisha. Sidhani kama ni vibaya kuwa na urafiki wa kawaida na ex wako unless your ex has something else in mind. La muhimu ni kujiuliza ni kwa nini huyo ex thinks about the whole friendship thing. Investigate. Ukiweka mipaka na kumweleza wazi kuwa intention yako ni kuwa marafiki wa kawaida tuu and nothing more else sidhani kama kutakuwa na tatizo. Ukiwa muwazi na kama alitaka zaidi, then s/he will back off hata huo urafikiri wenyewe. Tatizo la wanaume wengi ni kutokuweza kuwa friendship na ex wao. lazima utamchakachua tena. Ili ku avoid hili, ndio maana tunaamua kukata mawasiliano kabisa.

Lakini ku support idea ya friendship after relationship haina maana kuwa wengine ni wadogo. Kumbukuka kuna watu ambao wameshakuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na watu wengi. Kwa argument yako ina maana mtu kama huyo awe adui na hao watu? Urafiki na mapenzi ni vitu viwili tofauti. Kuna watu wengi wanaanza na urafiki unaishia kwenye mapenzi. Sasa kama mapenzi yakivunjika, then sioni sababu ya kuvunja pia urafiki ambao mlikuwa nao hata kabla ya kuanza uhusiano wa kimapenzi. Lakini kama mlianza na mapenzi motomoto tuu bila kuwa na urafiki wowote kabla, then mapenzi yakifa, hakuna kitakachobakia hapo.

Lakini pamoja na hayo bado naamini kuwa milima haikutani, lakini binadamu hukutana.
Unajuwa Mkuu kwa sisi tuliosoma mjini hapa na tupo over 30 nadhani utakuwa na makoloni mengi ambayo ulishayapitia na ni kweli you can be a friends, kumbuka wengine ndio tumejifunzia nao barehe zetu tukiwa secondary school, lazima utakuwa na ma x wengi tena mimi huenda hata FUSO lisitoshe kuwabeba, laabda FUSO mbili.

Lakini point yangu hapa ni mtu uliyepanga nae maisha na ukaamni mimi hapa ndio mwisho wa reli, halafu anakuzinguwa tena vibaya huyu mtu wewe unahitaji nae urafiki ili iweje? haufahamu kwamba kuna waliojiuwa kwa kushindwa kuwa na mioyo ya kijasili ya kuukubali ukweli? cha msingi hili eneo halimgusi kila mtu, kama demu ulimpata Fiesta na baada ya miezi 2 mkaachana huyu ataendelea kuwa rafiki kwenye mupe muruke.
 
Inawezekana mimi ni mgeni jukwaa hili kwahiyo sielewi taratibu zake, lakini kama niko sahihi nadhani wale wanaopenda kuchart wangekwenda kwenye JF chit chart. hii thread mngeacha wachangie wenye point na subject husika. Am standing to be collected.

Kama ni mgeni wa hili jukwaa, then ungeuliza kwanza taratibu zake kabla ya kujaribu "ku impose" rules zako. Kumbuka hili ni jukwaa la mahusiano, mapenzi na urafiki. Katika kuendeleza mahusiano, mapenzi na urafiki wetu kwenye jukwaa hili, ndio maana sometimes, huwa tuna chit chart in between. Kama tukiwa tuu serious na hoja, then sidhani kama tutakuwa tunalitendea haki hili jukwaa na kuna hatari kubwa mahusiano, mapenzi na urafiki wetu ukavunjika. Mkuu huku ni kazi na dawa. Hata Faiza Foxy na Mwanakijiji wakija huku ni mahusiano, mapenzi na urafiki mtimdo mmoja wakati huwa tunatoleana povu kwenye lile jukwaa la siasa. In case hupendezwi na hizo chit chat always bofya REPORT ABUSE. Its there for you to use.
 
badly,kisa chenyewe kilikuwa hivi kuna mzee wa kihindi alikuwa boss wake akawaita wafanyakazi wake(sita) na kuwaambia yeye anafunga ofisi na kuhamia Canada,na kwakuwa wamemfanyia kazi nzuri atawakopesha kila mmoja milioni 20 za kufanyia biashara ambazo anataka warudishe baada ya miaka mitano bila riba yoyote. Sasa bibie akaingia tamaa akaona anaweza kupata zaidi kama atamliwaza mzee wa watu na labda hata kusamehewa kulipa hiyo mil 20.
Akaniacha na kuanza kumfukuzia mzee wa watu lakini mzee akamtolea nje kwamba hahitaji mpenzi ana mke na watoto anachotaka wafanyakazi waendelee na kurudisha mkopo KWISHA KAZI.Baada ya muda akataka kurudi nikamtolea nje na sasa baada ya muda ndio anataka tuwe marafiki. Kibiashara kaendelea kidogo ana gari na vi-boutique viwili na anajenga nyumba yake kwa sasa.

Let's see if Matola will buy this now. Andaa bei. lol
 
Kama ni mgeni wa hili jukwaa, then ungeuliza kwanza taratibu zake kabla ya kujaribu "ku impose" rules zako. Kumbuka hili ni jukwaa la mahusiano, mapenzi na urafiki. Katika kuendeleza mahusiano, mapenzi na urafiki wetu kwenye jukwaa hili, ndio maana sometimes, huwa tuna chit chart in between. Kama tukiwa tuu serious na hoja, then sidhani kama tutakuwa tunalitendea haki hili jukwaa na kuna hatari kubwa mahusiano, mapenzi na urafiki wetu ukavunjika. Mkuu huku ni kazi na dawa. Hata Faiza Foxy na Mwanakijiji wakija huku ni mahusiano, mapenzi na urafiki mtimdo mmoja wakati huwa tunatoleana povu kwenye lile jukwaa la siasa. In case hupendezwi na hizo chit chat always bofya REPORT ABUSE. Its there for you to use.
Point noted mkuu,........huku hakuna mambo ya ubishi huku ni kujiachia, hili litakuwa jukwaa langu la kupumzikia instead log in facebook.
 
Unajuwa Mkuu kwa sisi tuliosoma mjini hapa na tupo over 30 nadhani utakuwa na makoloni mengi ambayo ulishayapitia na ni kweli you can be a friends, kumbuka wengine ndio tumejifunzia nao barehe zetu tukiwa secondary school, lazima utakuwa na ma x wengi tena mimi huenda hata FUSO lisitoshe kuwabeba, laabda FUSO mbili.

Lakini point yangu hapa ni mtu uliyepanga nae maisha na ukaamni mimi hapa ndio mwisho wa reli, halafu anakuzinguwa tena vibaya huyu mtu wewe unahitaji nae urafiki ili iweje? haufahamu kwamba kuna waliojiuwa kwa kushindwa kuwa na mioyo ya kijasili ya kuukubali ukweli? cha msingi hili eneo halimgusi kila mtu, kama demu ulimpata Fiesta na baada ya miezi 2 mkaachana huyu ataendelea kuwa rafiki kwenye mupe muruke.

Nakubaliana with what you say, but the ideal scenario, when it works to remain friends after breaking up a relationship, would be when the break up is mutual. And what would help even more is if you were friends before you became lovers. But if it was a violent breakup, then itakuwa ngumu ku maitain a normal friendship. Bado sijui kwa uporoto01 kusema waliachana "vibaya" alikuwa na maana kuwa the breakup was violent. Kuhusu "mtu uliyepanga nae maisha na ukaamni mimi hapa ndio mwisho wa reli", mbona wapo mpaka walio oana wakaishi pamoja kwa miaka mingi, then waka break up na bado wakaendelea kuwa marafiki? Ex anayetaka urafiki tuu utamjua na unaweza kumtofautisha na yule anayetaka kutumia urafiki for something else.
 
Point noted mkuu,........huku hakuna mambo ya ubishi huku ni kujiachia, hili litakuwa jukwaa langu la kupumzikia instead log in facebook.

Yea uwe makini b'se wale ex wako wanaojaza Fuso mbili wanaweza kuwa humu pia, halafu wakuombe muwe marafiki. AB have sent you a friend request. lol
 
Na wewe tupe mchango wako, from a female point of view. Would you be friend with your ex, if any, and why?
Nishachangia EMT siwezi, coz kwanza siwezi ruhusiwa na partner wangu, napenda uhusiano wetu uwe kwenye mambo muhimu tu, na sio urafiki kama watu wenginne ambao kila mara tunaonana kupata moja moto, siwezi kabisa, ni kukaribisha kumkosesha raha current partner tu
 
Jamani tuonane asubuhi, naona shemeji yenu kaniivalia kanga moja ndembe ndembe alafu anilegezea macho, hapa inabidi nishut down laptop niingie kwenye jukumu lingine.
Hii JF ukiifatisha kila siku utakuwa kwenye mahusiano mapya kumbe tatizo internet, huna muda wa kumpetpet partner. Alamsiki.
 
  • Thanks
Reactions: EMT

Poa usije tu ukawa unawahi bafuni, unatudanganya hapa, all the best ila sasa hakikisha mshike mkono usimwache nyuma
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom