Mhifadhi wa Taifa, Iddi Mashaka, akamatwa na Polisi Kesi ya kutungua helikopta

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884
Mhifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro, Iddi Mashaka, amekamatwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuhusika na tukio la utunguaji wa helikopta namba 88HF na kusababisha kifo cha rubani wake, Rogers Gower, raia wa Uingereza.

Imeelezwa kuwa Mashaka, ambaye pia ni ofisa intelijensia wa hifadhi hiyo, anadaiwa kuwa kinara mkubwa wa ujangili katika hifadhi mbalimbali zilizoko Kanda ya Ziwa kwa kutoa ushirikiano kwa majangili pamoja na kuwaazimisha silaha za kufanyia uhalifu huo.

Hii ni aibu sana, wale tunaowaamini ndio wanaotuangusha. Nashauri sheria za hifadhi za taifa zifanyiwe masahihisho ili watu kama hawa wanyongwe na kufilisiwa.
12662043_1431082663572814_2521319126372665652_n.png
 
Kama ni kweli Wahifadhi wenyewe wanahusika na ujangili basi ni vigumu vita hii kushinda.
 
Sasa Tiba inaanza kupatikana! Inasemekana hata baadhi ya "Wajeiwi " wakikosa ela wanazozihitaji ushika bunduki nakwenda kutafuta meno ya tembo kwenye hifadhi. screening ni muhimu sana kwa askari wote.
 
Hivi wewe ulitegemea kazi hii inafanywa na kina nani ??? Jk alazimishwe ataje majina ya vinara wa ujangali walioko Arusha ,Wanaofanya ujangili ndio hao hao tuliowapa dhamana ya kusimamia hifadhi zetu ,vitalu vya uwindaji na maafisa wa serikali

Ndio kisa cha kumuua yule Afisa wa Tanapa Arusha na kumweka kwenye buti na kutuletea stori za mkewe sijui na houseboy ndio wahusika wakuu
 
Serikali ya ccm imeozesha kila sekta, watu wanaona madudu huko wizarani, imefika mahali hata mtu alie ktk sekta ya huduma ya afya anauza dawa mgonjwa afe, tutashangaa mangapi? hii nchi ni shida.
 
Mhifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro, Iddi Mashaka, amekamatwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuhusika na tukio la utunguaji wa helikopta namba 88HF na kusababisha kifo cha rubani wake, Rogers Gower, raia wa Uingereza.

Imeelezwa kuwa Mashaka, ambaye pia ni ofisa intelijensia wa hifadhi hiyo, anadaiwa kuwa kinara mkubwa wa ujangili katika hifadhi mbalimbali zilizoko Kanda ya Ziwa kwa kutoa ushirikiano kwa majangili pamoja na kuwaazimisha silaha za kufanyia uhalifu huo.

Hii ni aibu sana, wale tunaowaamini ndio wanaotuangusha. Nashauri sheria za hifadhi za taifa zifanyiwe masahihisho ili watu kama hawa wanyongwe na kufilisiwa.
View attachment 322006
hana tofauti na mwenyekiti wa bunge, waalifu ndio wanaosimamishwa kupinga ualifu
 
Kwan akipatikana na hatia adhabu yake ni ipi maana tujue kwanza kabla izo sheria unazotaka zibadilshwe hazijabadilishwa
 
Back
Top Bottom