Gamba la Nyoka
JF-Expert Member
- May 1, 2007
- 7,022
- 9,285
Nadhani ni bora spika ajibu hoja,
kwa sababu kukataa hoja ya msingi ya kupitia upya adhabu ya Mh ili kuangalia usahihi wa adhabu yenyewe kwa misingi ya kanuni wala haliisaidii Bunge kujiboresha na kuwatumikia wananchi kwa ubora zaidi.
Kwa Spika mwenye kujiamini kwamba hatua alizochukua zilikuwa ndani ya kanuni na muongozo wa Bunge, haikuwa na haja tena kuzalisha hoja ndani ya hoja, bali ni kuisolve hoja ya kwanza kwa kuonyesha kwa uwazi kabisa kanuni kadha wa kadha. basi mambo yakesha.
Sasa badala ya kujibu hoja at hand yeye analeta personal attack(adhominems) mara ooh, "namuonea huruma kijana Zitto", mara ooh" unajua Zitto bado Mtoto kisiasa".
unajua nikitafakari kauli hizi za mh Sitta ninakumbuka kisa cha Karama na Majivuno(waziri mkuu wa kusadikika} katika kitabu cha kusadikika cha Shaaban Robert, majivuno alikuwa anaamini kabisa kwamba Karama hana busara eti kwa sababu hana mvi kichwani..sasa haya mambo ya kusadikika ndo leo tunayashuhudia katika Tanzania huru.