Mheshimiwa Zitto na wana-CHADEMA.....

labda kejeli ni kwa "mtu mzima kuambiwa aombe msamaha na akiri kosa" si unajua tamaduni kwamba mtu mzima haambiwi kaj**ba?

aidha inategemea barua iliandikwa kwa nani. yaani spika au mh. sita. sasa kama iliandikwa kwa spika na ikawa imefikishwa ofisi ya spika na kupokelewa na haikuwa imeandikwa "siri/confidential" itabidi tujiulize ni nani aliyeivujisha kwenye vyombo vya habari?

nakumbuka zitto alipoiweka barua hapa jf alisema nia ni kuwapa wanachama kile chote alichoandika badala ya wanatu kutegemea nusu habari za magazeti

Mkuu la kuongeza hapo sina, ukweli uko wazi barua ilisha sambaa magazetini ndo Zitto kuiweka hapa, sasa?
 
One thing is clear.JF is very notable.Either Spika au wapambe wake wanaingia hapa.

In my humble opinion hiyo barua haina nature yoyote ya usiri na in the spirit of "ukweli na uwazi" the speaker would do well to discard unnecessary confidentiality.Watu safi wenye hoja za nguvu hawana cha kuficha, watu wasio na hoja za nguvu na wenye uchafu wanaogopa uwazi kwa sababu naturally wanaogopa ku expose weakness ya arguments zao pamoja na uozo wao.

Sasa hapa cha siri sana nini?
 
Kwani spika anaikataa barua kwa kuwa imekuja hapa JF ama anaikataa kwa kuwa ni mbabe na anaweza kukataa tu ? Mimi sijaona hasa sababu ya baua hii kukataliwa. Mimi nasema Zitto komaa na Bunge hadi litoe tamko liingine kwenye hansard ama wakupe barua ya kukataa .Wewe umeandika na wao waandike ndiyo uratatibu . Hata kama ungalipeleka barua wapi bado si kosa si siri ile .
 
Spika ana uwezo wote wa kuamua analotaka kufanyika Bungeni na si Zitto au Rais anayeweza kumlazimisha vinginevyo unless Bunge zima lioneshe kutokuwa na imani nao na kumwondoa kwa taratibu za kibunge (impeachment).

Haya mimi sichangii tena kwa sababu kurudia kusema kitu kile kile kwa watu wale wale na kwa namna ile ile kutarajia watafanya vitu tofauti na wao wakaendelea kufanya vile vile basi ni dalili ya kurukwa na akili. Nafikiri bado nina akili timamu. Wamelikoroga wenyewe, walinywe.
 
Masatu

Sasa shida iko wapi hapo. Zito alitoa barua hiyo hapa baada ya kuona kwamba aliyeandikiwa kesha ipata na kumpa muda wa kutafakari. Ulitaka Daily News waitoe ya uongo? CCM na Watanzania MAFISADI ndio wametufikisha hapa wanataka kila kitu kiwe siri. Hakuna ujinga ujinga huu wa siri kila kitu, kwani kuna ubaya gani hata kama hiyo barua ipo kwenye luninga. Technologia mjomba twende na wakati tupo karne ya 21 siyo ya 10.

Waambieni watoe report ya BOT au bado wanaipika. Jamani tuweke Utanzania mbele na tuache longolongo ambazo hazina faida na taifa.

Dua

Shida ni wewe ulietaka ushahidi....
 
Dua

Shida ni wewe ulietaka ushahidi....

Hatujadili hapa bila kuwa na ushahidi wa yale uliyosema na tunaangalia yameandikwa vipi huko yalikotoka ndio maana ya Forum. Kama hulipendi hilo pole sana. Utaombwa ushahidi tena sana, Karibu JF.
 
Hatujadili hapa bila kuwa na ushahidi wa yale uliyosema na tunaangalia yameandikwa vipi huko yalikotoka ndio maana ya Forum. Kama hulipendi hilo pole sana. Utaombwa ushahidi tena sana, Karibu JF.

Hujakatazwa kuomba ushahidi umeuomba na umepewa then unauliza shida nini! Anymore?
 
my question, ni nani washauri wa karibu (advisors) na wasiri (confidants) wa Zitto ambao wanaweza kumpa ushauri bila kuwa na maslahi yao ya pembeni? This is really getting on my nerves..
 
Baada ya kupokea barua hiyo, Spika kupitia Katibu wake, Daniel Eliufoo, alitoa taarifa kwa vyombo vya habari akieleza kuwa Zitto atapelekwa kwenye Kamati ya Maadili na Madaraka ya Bunge kwa kuwa barua yake imejaa kejeli, ufedhuli na ubabe dhidi ya Bunge na Spika.

Tulikosea sana kuwaita hawa ndugu zetu waheshimiwa na kuliita bunge tukufu. Kwa nini barua isijibiwe tu yaishe? Upinzani Tanzania una adabu sana. Angalia lugha zinazotumiwa katika bunge la uingereza! Angalia Taiwan walivyokuwa wanatwangwana mingumi! Bunge liko pale kuhakikisha maslahi ya waliowapeleka pale yanalindwa, period. Hiyo lugha ya kejeli, ufedhuli na ubabe iko wapi? Au alitakiwa aanze na shikamoo? Whether mwandishi aliitoa kwenye internet au pengine ni besides the point. Tujibu yaliyomo kwenye barua na si mengineyo.
 
my question, ni nani washauri wa karibu (advisors) na wasiri (confidants) wa Zitto ambao wanaweza kumpa ushauri bila kuwa na maslahi yao ya pembeni? This is really getting on my nerves..


mkjj...

labda tumsubiri mwenyewe Mheshimiwa aje ajibu hili.



Mheshimiwa Zitto......

mie kwa mtazamo wangu unastahiki upate elimu ya PILITICALS SCIENCE,naamini itakusaidia katika maisha yako ya SIASA haswa za TZ
.
 
Naomba kuuliza, Hivi Mh. Zitto(MB) kama alimwandikia Spika barua nani mwingine alijua kuhusu hilo hasa tukifahamu wazi kwamba haya yanakuwa wazi ndani ya vikao vya Bunge baada ya spika kusema nimepokea xxx na kwa hiyo naomba Bunge lijadili, Hivi Mheshimiwa aliona tatizo gani kusubiri hiyo barua yake ifike huko na kufanyiwa kazi?

Je aliita waandishi wa habari? Je kulikuwa na sababu hiyo?

Au ndio hivyo tena, yuko kwenye dhamira yake ya Kujenda Jina la Chama na La kwake?!!!

Unajua waweza ku-mprovoke mtu bila sababu yoyote!!! hili Spika angelipata kabla ya vyombo vya habari haya yasingekuwepo akijibu tofauti kiungwana etc etc....

Hivi kila jambo likiwa la ku-reportiwa kwenye vyombo vya habari si tutafika mahali,,,,tunatumia muda mwingi kukanusha mambo ambayo yasingekuwa na sababu ya kufika kwenye hali hiyo?!!!

Ikumbukwe pia nchi hii ina matatizo mengi sana,,, Mh. Zitto(MB) anafahamu wazi maamuzi ya vitu kama hivi yanahitaji vikao vya bunge au kamati,,, ambavyo vinahitaji kutumia hela nyingi zaidi!!! yeye Mh. Zitto(MB) anafahamu umaskini wetu vizuri,,, mimi nilidhani signal iliyotumwa kipindi kile ilikuwa inatosha kabisa kumweleza kila mtu,,, kuanzia spika, wabunge na wananchi kwamba kunahitajika umakini mkubwa bungeni wakati wa kutoa adhabu,,, mantiki ya kurudia haya tena,,, kutumia hela zingine kwa kweli mimi kama mwananchi sitendewi haki kwa jasho langu kutumika ovyo!!!
 
Mbona barua iko clear ...sioni kejeli yoyote hapo...language iliyotumikas ni ya 'Kiungwana".
Unajua sisi mtu akitaka maelezo kuhusu haki yake anaonekana "ana kiburi"!
 
Nawaomba chadema muwe na msimamo, muunge mkono mheshimiwa Zitto mapambano haya ni mazuri yatawasaidia.na Zitto pia epuka kuwa unaisifu serikali unamuhudhi sana mh. Wangwe, na Mh wangwe jaribu kuwa unawasiliana na zito anapokosea siyo mlaumiane kwenye vyombo vya habari.mkishakuwa pamoja kama kweli barua ndo hiyo iliyoko hapo, kweli spika kachemka muungeni zitto mkono mtashinda, wananchi wengi tuko nyuma yenu
 

Zitto kuwekwa kitako na wapinzani Maulid Ahmed
HabariLeo; Tuesday,January 01, 2008 @19:02

MALUMBANO kati ya Spika Samuel Sitta na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, juu ya barua ya adhabu ya mbunge huyo, yameingia sura mpya kwani sasa Kamati ya Uongozi ya Wabunge wa Kambi ya Upinzani itakutana na Zitto kwa ajili ya kumshauri juu ya suala hilo.

Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni ambaye ni Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohammed (CUF), alisema kamati hiyo itakutana na Zitto ili kumshauri juu ya barua yake aliyomuandikia Spika akilalamika kutotendewa haki kwa kusimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge pamoja na Spika alivyomjibu.

“Mimi nimeipata jana nakala ya barua ya Zitto na nimeshampigia kumuambia kuwa tutakutana naye katika Kamati ya Uongozi kushauriana naye,” alisema Hamad. Alisema kamati hiyo itakutana wakati wowote kuanzia Januari 14, mwaka huu ambao wabunge watakuwapo mkoani Dar es Salaam kujiandaa kuhudhuria kikao cha Bunge kitakachoanza Januari 29, mwaka huu.

Akizungumzia maoni yake binafsi, Hamad alisema “binafsi ningeshauri Spika kwa upande wake aliache jambo hili liishe na Zitto naye kwake liishe na kusiwe na malumbano yoyote.” Desemba 24, mwaka jana, Zitto alimwandikia barua Spika, akitaka kuipitia upya adhabu ya kumsimamisha kutokana na kwamba imesababisha adhalilike na kushushiwa hadhi ndani na nje ya nchi.

Alidai adhabu hiyo aliyopewa haikuwa halali kutokana na kutofuata Kanuni za Bunge na kutopewa nafasi ya kujitetea. Sambamba na hilo, anataka Spika Sitta na mawaziri wengine kadhaa wachukuliwe hatua kwa madai walinukuliwa na vyombo vya habari wakisema yeye ni mwongo bila madai hayo kuthibitishwa.

Hata hivyo, katika majibu yake, Spika alilikataa ombi hilo na kuahidi kuifikisha barua ya mbunge huyo kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge. Sitta ameahidi kufikisha barua hiyo ambayo sasa haitashughulikiwa na Bunge, kutokana na maneno yaliyotumiwa na Zitto kujaa ufedhuli na ubabe dhidi ya Bunge kama taasisi na dhidi ya viongozi wa Bunge na Spika.

Katika taarifa ya majibu ya Spika Sitta iliyotolewa na Katibu wake, Daniel Eliufoo, ilisema kuwa barua hiyo ya Zitto itapelekwa kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa ajili ya kupata ushauri wake. Hata hivyo, hakusema lini ataipeleka barua hiyo zaidi ya kudai utakapofika wakati muafaka.

Spika alisema mbunge huyo kwa tiketi ya Chadema, ana hiari ya kwenda mahakamani ikiwa anadhani hatua hiyo itamsaidia kupata haki yake aliyonyimwa na Bunge. Katika majibu yake, Spika aliyeeleza kusikitishwa na maneno yaliyotumika yaliyojaa kiburi na fedhuli dhidi ya Bunge na viongozi wake, alisema barua ya Zitto ya rufaa si ya mbunge, bali ni waraka wa propaganda binafsi za kisiasa.

Zitto alisimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge Agosti 14, mwaka jana kwa madai ya kusema uwongo dhidi ya Waziri wa Nidhati na Madini, Nazir Karamagi, kuhusiana na mkataba wa madini wa mgodi wa Buzwagi. Adhabu hiyo imekwisha na anatarajiwa


mie mwenzenu bado sijaelewa hii issue,Mheshimiwa anasema ndio kwanza ameipata,mheshimiwa ZITTO anasema inawezekana mkuu 6 au HR ndio waloitoa ktk net,SO WHICH IS WHICH............hebu wajuzi wa MAMBO TUWEKENI SAWA HAPA.
 
Kama 6 kakataa ombi la Heavy na kudai barua ni ya kifedhuli, kwa nini aipeleke kwenye Kamati ikajadiliwe tena wakati yeye kishatoa hukumu?
 
Siasa za Bongo bwana zinachekesha sana, mkubwa ana-behave kitoto na mtoto ana-behave kikubwa!
 
Asha
Nakuunga mkono,cha muhimu contents zinajulikana hivyo mjadala ni je kweli kuna maneno ya kejeli na kifedhuli au la. KITU MUHIMU HAPA NI KUJADILLI HOJA ILIYOKO MEZANI
 
Back
Top Bottom