Mheshimiwa Sitta asimikwa kuwa Mzee wa Karagwe ;akemea wanaotafuta uongozi kwa kutumia fedha

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,573
Mhe. Sitta alitembelea kikundi cha Wanawake wajane Wazee na Watoto yatima Wilayani Karagwe ambapo kikundi hicho kilijumuisha Wazee wa Karagwe na Kyerwa waloimsimika Mheshimiwa Sitta kuwa Mzee wa Karagwe. Baada ya kusimikwa kuwa Mzee wa Karagwe Mheshimiwa Sitta aliwahutubia wanawake wajane, Wazee, watoto yatima na wananchi waliofika kumskiliza. Katika hotuba yake aliwaomba wananchi kuwa makini na viongozi wanaotafuta uongozi kwa kutumia fedha. Pia alikemea tabia ya Viongozi kujilundikia mali na kuwaomba watanzania kurudia maadili aliyoyaacha baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

Katika siku yake ya tatu Wilayani Kyerwa Mhe. Sitta ameweza kutembelea mpakani mwa Tanzania na Uganda Murongo na Kikagati Wilaya Isingiro nchini Uganda kujionea mradi wa pamoja wa umeme wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kati ya Tanzania na Uganda ambao utanufaisha vijiji vyote vya pande zote mbili mara baada kukamilika. Mradi huo wa umeme wa maji ambao utafanyika katika mto Kagera tayari umewekewa msukumo na serikali zote mbili za Uganda na Tanzania ili uweze kuanza kuzalisha umeme baada ya miezi mitatu ijayo. Mhe.

Sitta katika ziara yake hiyo alikutana Waziri wa nishati wa Uganda ambaye aliwaakilisha nchi yake pia na mshauri muendelezi wa mradi huo. Mhe. Sitta alihaidi katika kikao hicho kutia msukumo zaidi katika serikali ya Tanzania ili mradi huo uweze kukamilishwa haraka iwezekanavyo ili wananchi wa pande zote mbili waanze kunufaika . Mheshimiwa Sitta ataendelea na ziara yake Mkoani Kagera kwa Kutembelea mpaka wa Kabanga Wialayani Ngara. Imetolewa na:
 
Attachments

  • SITA 4.jpg
    SITA 4.jpg
    44.5 KB · Views: 91
  • SITA 5.jpg
    SITA 5.jpg
    44.2 KB · Views: 92
  • SITTA 1.jpg
    SITTA 1.jpg
    174.9 KB · Views: 259
  • SITTA 7.jpg
    SITTA 7.jpg
    37.9 KB · Views: 77
ndo mwendelezo ule ule wa siasa za ki udhaifu ziara ya kiserikali anachanganya na mambo ya u CCM wakati ni kodi zetu wote..kuna umuhimu wa katiba mpya kulitambua hili
 
yuko kakika pilika pilika za kutaka kuungwa mkono ili agombee uraisi. 2015 ninavyoamini sidhani kama atafanikiwa
 
Kumbe, yeye kaona hiyo inafaa kuliko ile ya Ben kuomba nafasi ya kuwa mwana ukoo wa wazanaki. lakini awe makini asije akawatibua wanyambo kama Ben alivyowtibua wazanaki na watanzania kwa ujumla.
 
yuko kakika pilika pilika za kutaka kuungwa mkono ili agombee uraisi. 2015 ninavyoamini sidhani kama atafanikiwa

Nimejiuliza ziara kama hii kwanini hakuongozana na Blandes? Si mnakumbuka matokeo ya uchaguzi wa wa wabunge? Sitta angewatambua vizuri wanyambo maana ingekuwa ni kupopolewa kwa mawe mwanzo mwisho.
 
Hao wazee walikutana lini na kuamua kumtunukia uzee wa Karagwe? na kwa sifa zipi? Hizi fix za wajanja fulani.
Ndio maana mwaka uleee JK akisimikwa na wazee (kikundifulani) wa kisukuma Mzee mmoja akaona huo ni utapeli akamvaa jukwaani. Jamaa alikula kifungo ila ujumbe ulieleweka.
 
Hivi haya makabila mengine sijui yameishiwa na wazee!!!!
Jitu halijui hata lugha yenu mnalipa uzee wa klan, na lenyewe linakubali.
Inatia kichefuchefu kwa kweli.
 
Hivi haya makabila mengine sijui yameishiwa na wazee!!!!
Jitu halijui hata lugha yenu mnalipa uzee wa klan, na lenyewe linakubali.
Inatia kichefuchefu kwa kweli.

Nafikiri Sitta kapigwa changa la macho au katapeliwa maana hakuna kitu kama wazee wa kabila la Wanyambo.
Kama ilivyo kwa wahaya, wanyabo nao walikuwa na utawala unaojulikana kana "obukama" na hakuna kitu kama jopo la wazee. Omukama hapigiwi kura wala kuteuliwa bali anarithi kwa utaratibu maalumu.
Nafikiri Sitta amepewa uzee wa CCM na si wanyambo.
Nani kiongozi wa wazee hao?
 
Nakubaliana na wewe kwamba kilicho fanyika ni utapeli wa kisiasa,jamii za Wahaya na Wanyambo hazina kitu kinaitwa baraza la wazee!
 
Alijenga ofisi ya Spika kule Urambo akidhani ataendelea kuwa spika hadi urais. Chezeya ccm weye!
 
Nafikiri Sitta kapigwa changa la macho au katapeliwa maana hakuna kitu kama wazee wa kabila la Wanyambo.
Kama ilivyo kwa wahaya, wanyabo nao walikuwa na utawala unaojulikana kana "obukama" na hakuna kitu kama jopo la wazee. Omukama hapigiwi kura wala kuteuliwa bali anarithi kwa utaratibu maalumu.
Nafikiri Sitta amepewa uzee wa CCM na si wanyambo.
Nani kiongozi wa wazee hao?

Wazee wenye kushabikia CCM ndo wamempa uzee wa kimila kwenye kundi lao, hivyo hawezi kutambuliwa na wanyambo wote. Pia kwa utaratibu wa wanyambo hakuna litu kama hicho. Mzee kadanganywa live. Eti wanakutana kwenye jengo/ ukumbi. Hawajui hata ni mahali gani wazee walikuwa na utaratibu wa kukutania. Kweli siasa mchezo mchafu. Mtu anadanganywa live. Nimejaribu kufikiria, ni lugha gani ingetumika iwapo wazee hao pamoja na Sitta watakuwa na kikoa kujadili mambo ya Wanyambo! Laiti wangetutajia wazee hao waliomteua usije kuta ni jopo la Massawe na wenzake ambao kwanza si wanyambo.
 
Kweli kabisa kapewa uzee na genge la matapeli. Tena wasijaribu kusema eti ni wazee wa Karagwe, inawezekana kawalipa wamsimike uzee maana hata mkuu wa mkoa Massawe nasikia anaitwa "Mulokozi". Sitta amekuwa "self made mzee wa Karagwe!" A non recognised title!
 
Hao wazee walikutana lini na kuamua kumtunukia uzee wa Karagwe? na kwa sifa zipi? Hizi fix za wajanja fulani.
Ndio maana mwaka uleee JK akisimikwa na wazee (kikundifulani) wa kisukuma Mzee mmoja akaona huo ni utapeli akamvaa jukwaani. Jamaa alikula kifungo ila ujumbe ulieleweka.
Huenda Sita kalipia zoezi lote hilo
 
Back
Top Bottom