Watanzania
JF-Expert Member
- Jul 7, 2009
- 727
- 42
Ni haki kwa wananchi kujiridhisha kama rais anaipenda nchi yetu. Kuna mambo kadhaa ambayo rais anawezapimwa kama anaipenda nchi yake. Hili suala la Mh. Rais Kikwete kufanya safari nyingi nje ya nchi kwa nchi maskini kama ilivyo yetu ni mojawapo ya kigezo cha kumpima rais kama anapenda nchi . Ukimwangalia Rais Kikwete akiwa nje ya nchi utagundua kuwa anafurahia kuwa nje ya nchi kuliko Tanzania. Rais ambaye anatarajiwa kuwa na muda wa kutosha kutafakari matatizo ya nchi na kuyapatia ufumbuzi yeye anafunga safari nyingi na anafurahia kuwa nje ya nchi yake kuliko kutulia nchini na kutoa uongozi unaohitajika. Je hii si dalili ya rais kutoipenda nchi yake kwa dhati?