Mheshimiwa nzota atiwa hatiani na sasa anaelekea jela

FDR.Jr

JF-Expert Member
Jun 17, 2008
1,359
353
HTML:
mheshimiwa henzron mwankenja wa mahakama ya kisutu amemtia hatiani mheshimiwa mwenzake nzota kwa kesi ya kudai na kupokea rushwa. Waliopo kisutu waende kazini kwa picha na habari zaidi.
Kazi ni kazi muraaa! Mwankenja anastaafu na kichwa cha mahakama yenyewe kwa sentensi!!!!
 
Ndio nani huyo na ametiwa hatiani kwa kosa gani?
 
Unajua huyo Jamillah Nzota alikula hela na kumwachia jamaa mmoja ambae ushahidi wote ulimuonyesha kwamba alimlawiti mtoto mdogo wa kiume. Toka siku hiyo nikamuombea alipe kwa hili baya alilolifanya. Hatimae Analipa kwa ubaya alioufanya.
 
Huyu Nzota ndiyo hakimu yupi na anasikiliza kesi yanani iliomfanya kamatwe kwa rushwa??
 
Hakimu mkazi wa mahakama ya temeke jijini dsm, alikamatwa last year kwa mtego wa pccb huko whitesand alikokuwa ameahidiwa akachukue mpunga wake.

Kesi ikaletwa kisutu mbele ya mh.mwankenja wa mahakama hiyo.
 
Kula na kulipa ni mtindo wa kisasa. Lakini wakimfunga atapelekwa gereza gani maana si atakutana na wamama aliowapiga mvua
 
Hakimu Jamila Msota aliyekuwa anatuumiwa kuomba na kupokea rushwa ameukumiwa leo asubuhi kwenda jela miaka kumi na moja aliyeongoza jopo la mahakimu kutoa hukumu hiyo ni Hakimu Estron Mwakenye
 
Wafungwe pia na mahakimu wengine wanaopindisha sheria na kufanya favouritism kwa mafisadi. Km wale wali handle case ya the late Ditto and still living Chenge.
 
Hakimu Jamila Msota aliyekuwa anatuumiwa kuomba na kupokea rushwa ameukumiwa leo asubuhi kwenda jela miaka kumi na moja aliyeongoza jopo la mahakimu kutoa hukumu hiyo ni Hakimu Estron Mwakenye

...naamini ratio ya mahakimu wanawake dhidi ya wakiume ni ni ndogo sana. Linapokuja suala la kudai na kupokea rushwa, ningetarajia mahakimu wengi wa kiume wangekuwa Lupango hivi sasa.

Isije ikawa 'alitegwa' akanasa!

Rushwa zimekithiri, lakini pia chuki binafsi pia mnh!
 
Alichukua rushwa ya milioni tano, miaka 11, lakini waliochukua rushwa ya pesa nyingi utaona wanaachiwa, kuna baadhi ya mafisadi kesi zao ziko kwa mwankenja tuone na wao atawapa miaka mingapi, au atasema ushahidi hakuna wa kuwatia hatiani?
 
Hakimu Jamila Msota aliyekuwa anatuumiwa kuomba na kupokea rushwa ameukumiwa leo asubuhi kwenda jela miaka kumi na moja aliyeongoza jopo la mahakimu kutoa hukumu hiyo ni Hakimu Estron Mwakenye

Una maana Mwankenja? :confused:
 
Kula na kulipa ni mtindo wa kisasa. Lakini wakimfunga atapelekwa gereza gani maana si atakutana na wamama aliowapiga mvua

Mkuu, mfungwa hachagui gereza. Atajua huko huko kama abembeleze ushoga au awe mbabe kama alivyokuwa mh hakimu.
 
Mhh hukumu yake mbona ndefu sana jamani duuuh!

Amehukumiwa kifungo cha miaka 11, lakini atatumikia adhabu hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu (3) tu. Kwa wale mnaofahamu taratibu za hukumu hasa pale unapokuwa na kosa zaidi ya moja mtaelewa ina maana gani. Yaani kila kosa lina individual penalty, sasa zile penalties ukijumlisha ndio inafikia hiyo miaka 11. Lakini katika kutumikia hizo penalties, unafanya zote wa wakati mmoja. So, she will be in jail for three years only.
 
Tukitega mtego wa rushwa kwa mahakimu na makarani wa mahakama, wote watafungwa, serikali itaajiri upya. Thye are corrupt, very corrupt bila kusahau Jeshi la polisi!!!
 
Una maana Mwankenja? :confused:

Mwankenja=Mwakenye?

Watanzania wengi tuna huu ugonjwa wa ukosefu wa jitihada za umakini kwenye mambo mengi tuyafanyayo...Pole Masanilo. Ni ugonjwa huo pia unaelezewa kumkumba Fungamtama kwenye barua yake kwa Mwanahalisi, na ugonjwa huo upo pia mahakama kuu walipomwndikia "Auditor" wa Mwanahalisi.
 
Back
Top Bottom