Mheshimiwa Mtoto wa mkulima, na hili la tofauti ya mishahara lisisubiri mgomo

Njaare

JF-Expert Member
Sep 26, 2010
1,081
275
Kwa hili najua wengi mtauliza source. ANGALIA WARAKA WA MSAJILI WA HAZINA KUHUSU MISHAHARA.
Kuna ubaguzi wa makusudi unaofanywa na serikali kwa kutoa mishahara tofauti kati ya wahadhiri wenye vyeo sawa katika vyuo vya elimu ya juu. Huu ubaguzi umesababisha hata baadhi ya wahadhiri kuanza kutoka chuo kimoja kwenda kingine na kusababisha upungufu mkubwa wa wahadhiri katika vyuo vikuu.

Ubaguzi ulio wazi ni ule unaofanywa kati ya wahadhiri wanaopata mishahara katika ngazi ya PHTS na PUTS. Kwa mfano Ukiangalia waraka wa hazina utagundua kuwa Assistant Lecturer aliyeko PHTS 13 anamzidi assistant Lecturer aliyeko PUTS kwa zaidi ya shilingi 250,000/= japo wote ni majukumu sawa na kazi wanafanya pamoja na muda wa kufanya kazi ni sawa. Ukienda mbali zaidi assistant Lecturer aliyeko PHTS 14 anamzidi mshahara Lecturer aliyeko PUTS 15.

Je hili linafanywa maksudi na serikali au linafanywa maksudi na viongozi wa chuo kama kina mlacha?
 
nadhani tunahitaji kufanya mabadiliko ktk hilo ili kepuka mkanganyiko unaojjitokeza sasa

mapinduziiii daimaaa:ban:
 
aghaaaaaaaaa hayo ndio mauvundo yaliyoko vyuo vya elimu ya juu, unyanyasaji na ubaguzi uko kwa kiwango cha juu, hio ni upande wa wahadhiri ukienda kwa upande wa waendeshaji ndio utatia akili full kuchakachua ngazi za mishahara, hili linahitaji kweli kweli limulikwe ili lisiendelee.Mtabaka yanaumiza taaluma kwenye vyuo vyetu lazima tuelewe.
 
haa, mi nilidhani kwa vyuo vya umma upande wa taaluma wanatuymia wote PUT, na waendeshaji wantaumia PHTS, kama kweli kuna kitu kama hicho ni uhuni na aingii akilini, inabidi warekebishe hii kitu mara moja!
 
Kwa hili najua wengi mtauliza source. ANGALIA WARAKA WA MSAJILI WA HAZINA KUHUSU MISHAHARA.
Kuna ubaguzi wa makusudi unaofanywa na serikali kwa kutoa mishahara tofauti kati ya wahadhiri wenye vyeo sawa katika vyuo vya elimu ya juu. Huu ubaguzi umesababisha hata baadhi ya wahadhiri kuanza kutoka chuo kimoja kwenda kingine na kusababisha upungufu mkubwa wa wahadhiri katika vyuo vikuu.

Ubaguzi ulio wazi ni ule unaofanywa kati ya wahadhiri wanaopata mishahara katika ngazi ya PHTS na PUTS. Kwa mfano Ukiangalia waraka wa hazina utagundua kuwa Assistant Lecturer aliyeko PHTS 13 anamzidi assistant Lecturer aliyeko PUTS kwa zaidi ya shilingi 250,000/= japo wote ni majukumu sawa na kazi wanafanya pamoja na muda wa kufanya kazi ni sawa. Ukienda mbali zaidi assistant Lecturer aliyeko PHTS 14 anamzidi mshahara Lecturer aliyeko PUTS 15.

Je hili linafanywa maksudi na serikali au linafanywa maksudi na viongozi wa chuo kama kina mlacha?

Nafikiri ni muhimu kuzingatia quality ya lecturer ktk mshahara, lecturer ana experience kiasi gani amesoma wapi na vinginevyo. Sidhani kua unaweza kumlipa lecturer aliegraduate let say Tumain university na yule aliegraduate oxford, hivi navyo ni vitu vya kuzingatia kama tunataka kunyanyua kiwango cha elimu. Hii utaiona umuhimu wake kama unakubali kua university nazo zina rank.
 
kifupi kuna madudu mengi sana kwen remuneration, naamini hata ktk sekta binafsi ndo balaa kbs hata scale hawana, ujanja wako tu
 
Back
Top Bottom