Mheshimiwa Mbunge Joyce Mukya atoa misaada kwa watoto yatima Arusha

Rucho Ongiri

Member
Dec 23, 2011
7
3
Mheshimiwa mbunge wa viti maalum mkoa wa Arusha, Joyce Mukya jana ameamua kusherehekea Sikukuu ya Christmas na Mwaka mpya kwa kutoa zawadi mbalimbali kwa vituo vitano vya kulea watoto yatima vilivyoko Manispaa ya Arusha na wilaya ya Arumeru.

Misaada iliyotolewa na mbunge huyo ambaye hii ni mara yake ya kwanza kuingia bungeni ni pamoja na kilo 250 za unga wa sembe, mchele kilo 125, sukari kilo 100, ndoo tano za mafuta ya kupikia, mbuzi watano, katoni 25 za juisi, chumvi kilo 50, dazani tano za majani ya chai na mifuko mitano ya pipi.

Vituo vya kulea yatima vilivyopatiwa misaada hiyo katika hafla fupi iliyofanyika ofisini mbunge huyo zilizoko jengo la ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Arusha ni pamoja na Faraja Orphanage children home kilichopo eneo la Shangarai wilayani Arumeru, Kibowa centre, Medical Daughters of Merry, Tuamkeni Orphans care na Mama Hadija children home, vyote vya Manispaa ya Arusha.

Mbunge huyo aliwaomba watu wenye uwezo kuacha ubinafsi kwa kujifikiria wao na familia zao, badala yake wawafikirie wengine wenye shida na uhitaji katika jamii kama watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kwa kushirikiana nao kiasi kidogo walichojaaliwana Mwenyezi Mungu.

picha za tukio hilo baadaye...!
 
Hongera yako mh. Mbunge Joyce kwa kuwakumbuka hao watoto ili nao wapate kujumuika na watanzania wenzao kusherekea sikukuu ya xmass.
Jipange sasa kwa ajili ya kuwatumikia wana wa arusha vizuri zaidi mwaka kesho.
 
Mheshimiwa mbunge wa viti maalum mkoa wa Arusha, Joyce Mukya jana ameamua kusherehekea Sikukuu ya Christmas na Mwaka mpya kwa kutoa zawadi mbalimbali kwa vituo vitano vya kulea watoto yatima vilivyoko Manispaa ya Arusha na wilaya ya Arumeru.

Misaada iliyotolewa na mbunge huyo ambaye hii ni mara yake ya kwanza kuingia bungeni ni pamoja na kilo 250 za unga wa sembe, mchele kilo 125, sukari kilo 100, ndoo tano za mafuta ya kupikia, mbuzi watano, katoni 25 za juisi, chumvi kilo 50, dazani tano za majani ya chai na mifuko mitano ya pipi.

Vituo vya kulea yatima vilivyopatiwa misaada hiyo katika hafla fupi iliyofanyika ofisini mbunge huyo zilizoko jengo la ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Arusha ni pamoja na Faraja Orphanage children home kilichopo eneo la Shangarai wilayani Arumeru, Kibowa centre, Medical Daughters of Merry, Tuamkeni Orphans care na Mama Hadija children home, vyote vya Manispaa ya Arusha.

Mbunge huyo aliwaomba watu wenye uwezo kuacha ubinafsi kwa kujifikiria wao na familia zao, badala yake wawafikirie wengine wenye shida na uhitaji katika jamii kama watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kwa kushirikiana nao kiasi kidogo walichojaaliwana Mwenyezi Mungu.

picha za tukio hilo baadaye...!

Wa chama gani vile?
 
Mleta MADA karibu sana kwa mara ya kwanza majamvini!
Wewe ndiye Joyce Mkukya?
 
kutoa misaada si hoja wala lengo la kupewa ubunge na chama tunataraji wabunge watakaojaribu kuleta mabadiliko katika mfumo wetu ili watoto hao yatima wasiwepo kabisa.Namfahamu Mbunge Mukya tushauri wangu kwake ni kwamba asiitarajie kuwa bora kama ataendelea kufanya kazi kwa mfumo uleule wa chama cha magamba
 
Mheshimiwa mbunge wa viti maalum mkoa wa Arusha, Joyce Mukya jana ameamua kusherehekea Sikukuu ya Christmas na Mwaka mpya kwa kutoa zawadi mbalimbali kwa vituo vitano vya kulea watoto yatima vilivyoko Manispaa ya Arusha na wilaya ya Arumeru.

Misaada iliyotolewa na mbunge huyo ambaye hii ni mara yake ya kwanza kuingia bungeni ni pamoja na kilo 250 za unga wa sembe, mchele kilo 125, sukari kilo 100, ndoo tano za mafuta ya kupikia, mbuzi watano, katoni 25 za juisi, chumvi kilo 50, dazani tano za majani ya chai na mifuko mitano ya pipi.

Vituo vya kulea yatima vilivyopatiwa misaada hiyo katika hafla fupi iliyofanyika ofisini mbunge huyo zilizoko jengo la ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Arusha ni pamoja na Faraja Orphanage children home kilichopo eneo la Shangarai wilayani Arumeru, Kibowa centre, Medical Daughters of Merry, Tuamkeni Orphans care na Mama Hadija children home, vyote vya Manispaa ya Arusha.

Mbunge huyo aliwaomba watu wenye uwezo kuacha ubinafsi kwa kujifikiria wao na familia zao, badala yake wawafikirie wengine wenye shida na uhitaji katika jamii kama watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kwa kushirikiana nao kiasi kidogo walichojaaliwana Mwenyezi Mungu.

picha za tukio hilo baadaye...!

Kutoka JUKWAA HURU LA UCHAMBUZI tunaambiwa hivi:
“Sadaka ni SIRI, kama umetoa kwa mkono wa kushoto, basi hata ule wa kulia usijue kuwa umetoa nini, sio jambo la kutangaza kwa maana unapotoa unamtolea Mungu, naye anakuona, ukitoa kwa ajili ya kujipatia ufahari basi haiwezi kubarikiwa sadaka yako
Kwa muda wa kutosha tu nimekuwa nikiendelea kufuatilia hali ya kuongezeka kwa Wasamaria wema na Usamaria wema wao hapa nchini kwetu. Watu wenye moyo wa kusaidia yatima, wasio jiweza, wanaoishi katika mazingira magumu na hata hawa ndugu zetu ambao wanaishi na VVU.
Kwa wale ambao wamekuwa wakiyaona bila shaka wataungana nami kukiri kuwa hali hii imezidi kushamiri zaidi hasa katika kipindi hiki ambapo teknolojia pia imekuwa ikiwezesha usambazwaji na upatikanaji wa habari katika kona mbalimbali ndani na hata nje ya nji yetu hii.
Hata hivyo (sijui kwasababu nilizaliwa kuona mambo kinyume au vipi), kuna jambo ambalo nimekuwa kila nikilitafakari, basi limekuwa likinisukuma kuhoji uhalali wa misaada hiyo na watoaji wake. Hivi MSAADA sio sawa tu na SADAKA? Sasa kuna haja gani kwa mtoaji kuhanikiza “Jamani kesho naenda kutoa misaada mahali fulani mje mnione” au Leo nimetoa msaada kwa akina fulani jamani oneni”
Kwa wafuatiliaji wa taarifa zetu za habari katika vyombo vyetu mbalimbali, limekuwa jambo la kawaida kila siku (Narudia tena KILA SIKU), kukutana na habari za ama fulani kesho atatoa msaada sehemu fulani, au fulani leo katoa misaada sehemu fulani, na habari hizo hufuatiwa na mlolongo wa maelezo kibaaaaaaao yote yakimsifia mtoa msaada huyo kufikia hata hatua ya kupachikwa uheshimiwa.
Ukisoma kwa undani au kusikiliza kwa undani maelezo ya mhusika huyo, mengine huweza hata kukuletea maswali mengi sana kuliko uhalisia wa wasifu wake, na ukweli ndio uko hivyo. Kuwa wengi wa “Waheshimiwa Matajiri” watoa misaada, ni wale ambao utajiri wao huo una maswali mengi zaidi juu ya upatikanaji wake kuliko ukweli wa mambo ambao wananchi wanatakiwa kuuamini.
Ni watu ambao wamewageuza binadamu wenzao “migodi” kwa ajili ya kusakia fedha zao hizo na pia wamewageuza binadamu wenzao “majosho” kwa ajili ya kusafishia fedha zao chafu (Dirty money).
Wakati fulani nilipokuwa bado mdogo, nakumbuka maneno niliyoyanukuu hapo juu, kuhusiana na kitu msaada (unadhani ni tofauti na sadaka?) Sasa hawa jamaa zetu ambao wanatoa sadaka, ubani sijui, misaada nk, huku wakiwa wameitisha maluninga na magazeti kwa ajili wawatangaze kwa kile walichotoa, wao wanatoa kwa ajili ya kusaidia kweli au kwa lengo la kupewa sifa za duniani?
Hivi ikitokea tukachachamaa na kumkaba mmoja wao na kisha tukamwambia ashike kitabu kitakatifu na akiri kuhusu utajiri wake, ambao ana tusaidia, ni wangaopi watathubutu kufanya hivyo? Hivi msaada ukitolewa kimya kimya, kwa mtu kujiendea zake akatoa msaada na kisha akajirudia dukani au ofisini na hata nyumbani kwake, huo msaada hautakuwa msaada kweli? Hivi ni wangapi wanapowanunulia watoto wao nguo au kuwatoa out hujitangaza? Ebo! ukiwa na utajiri kusaidia wasio nacho si wajibu wako kwani?
Tena wengine unakuta wanachangisha na kuchangisha fedha kwa ajili ya kwenda kutoa misaada hiyo, na kisha kujipangia katika fedha hizo za michango kuwa mimi nitatumia kiasi fulani kwa ajili ya kuniwezesha kupeleka misaada sehemu fulani, Ebo! ndio misingi ya misaada hiyo jamani?
Nauliza tu lakini, msije mkanitoa roho maana hapa tayari kuna watu wakisoma hapa najua wataanza kuomba kila aina ya dua ili nifie mbali maana na nimewagusa pabaya. Ninachotaka kusema hapa ni kuwa, kama unatoa kwa ajili ya kuonyesha uchungu wako, basi ni vyema uchungu huo akauona Mungu aliyekuwezesha kuupata utajiri huo, na sio binadamu mwenzio akusifu.
@http://uchambuzi.wordpress.com/2006/11/13/wasamaria-wetu-na-usamaria-wa-vyombo-vya-habari/
 
Rtz, Rajao, Mwita25 na MS wataingia muda si mrefu kumponda Godbless Lema
 
Bwana Yesu pia alipogawa Mikate na Samaki hakufanya siri, hata Mungu aliposhusha Manna ya bure kutoka mbinguni kuwapa bure wana wa Israeli nae pia hakufanya siri, Mh. Joyce amefanya hivyo na anahamasisha wengine nao wafanye hivyo, kuongoza ni kuonesha njia, na inapokuwa kwa vitendo ni bora zaidi, sasa angeficha angehamasishaje wengine nao wajitolee? Keep it Up Joyce!
 
Ahsante kwa ufafanuzi murua.
Hawa wanaopinga misaada kutangazwa ndio hao hao wanakuwa wa kwanza kusupport watu wao wanapotoa misaada.

Hata kama sifahamiani na huyu mbunge lakini jambo alilofanya linastahili kuungwa mkono na kuigwa na wengine.
 
Kwanza kafanya vizuri kuweka bayana kwani kuna baadhi ya walezi wamekua na tabia ya kuchukua misaada inayotolewa kwa ajili ya watoto hao na kujinufaisha wenyewe, hongera Joyce na Mwenyezi Mungu akuongezee zaidi na akupe moyo huo huo wa utoaji.
 
Back
Top Bottom