Mheshimiwa Masha mbona unachemsha kuelekea katika uchaguzi...

FirstLady1

JF-Expert Member
Jul 29, 2009
16,792
5,374
Wadau wa Blog hii salaam
Mie sio mwandishi mzuri lakini .

Hii ni tetese ambayo nimekumbana nayo katika Pita pita zangu hebu wana JF jaribuni kuifanyia kazi ndani ya vyanzo vya waandishi wa habari na Raia wema Stone city

News yenyewe ni kuhusiana na Sakata zima la kivuko cha kamanga feri Mwanza

Habari za kuaminika na zisizoaminika sana zinasema ,baada ya mmiliki wa kivuko cha kamanga Feri kupass away aliacha urithi wa vivuko vyake viwili kilichoko Mombasa na Mwanza kwa watoto wake wa wawili.

Mtoto wake mmoja alieyekuwa anasoma majuu alipewa kumiliki na kuendesha kivuko cha Mwanza City lakini katika mazingira ya kutatanisha Mke wa marehemu akishirikiana na Mheshimiwa Masha na baba mzazi wa Masha waliweza kufanya manuva na kubadili hati za Kivuko hicho na kutaka kumnyang'anya kijana urithi huo katika mazingira ya kutatanisha.

Pia kijana aliwekwa wanted kutokukanyaga nchini kwao/Nyumbani lakini sijajua ni kwa sababu gani ila yeye aliweza kufika Mwanza katika njia alizojua yeye..

Raia wanaoishi maeneo hayo walighafika na kudai Masha ndo kazikosa kura zao 2010 kwa sababu ameharibu na hakuwahi kufanya vizuri katika kipindi chote alichokuwa madarakani

Wachunguzi wa mambo hebu pelekeni macho yenu jijini Mwanza muibuke na habari hii ya utata na yenye mvuto kwa waziri wetu
 
na ndio hapo mie nimejaribu kuomba waandishi wa habari na vyombo vyetu vilivyo mkoani Mwanza vikafukue mambo haya ni kutuwekea hadharani la itabidi nitinge mwenywe mdau ili niweze kulimuvuzisha hili news fasta
 
Masha anakoelekea si kuzuri kisiasa. Ila with politics anything is possible. Ila jamaa anaonekana bogus kabisa huko kwao.
 
Hii mbona ilishawahi kuandikwa sehemu? Sikumbuki wapi ila nakumbuka mama wa Kijeruman na watoto wake kama sikosei. Anyway, ngoja niitafute kwenye mtandao.
 
masha si huyuhuyu aliyelikoroga la vitambulisho? sasa hawa hawaridhiki pamoja na wadhifa mkubwa bado anataka kudhulumu?
Kwa kuwa ni tetesi ngoja tusubiri tuone....vinginevyo tuhuma hizo ni nzito sana....
 
Hii mbona ilishawahi kuandikwa sehemu? Sikumbuki wapi ila nakumbuka mama wa Kijeruman na watoto wake kama sikosei. Anyway, ngoja niitafute kwenye mtandao.



kwa kuongezea hati iliyobadilishwa nasikia imebeba jina la mke wa pili, yule wa kwanza ambaye alifunga nae ndoa tangu zaman huko kitambo jina lake limeondolewa pamoja na watoto aliozaa nae..sasa hati imebeba jina la mke wapili wakidai kwamba alifunga nae ndoa tena Imma Adv walithibitisha...hizi habar nilizisoma sehem japo nimesahau wapi..tutafute zaid news
 
Hilo nimewahi kukutana nalo kwenye kama sikosei RAIA MWEMA. Na nafikiri Masha aliulizwa akakana kufanya ujanja na huyo mama. Since then sijui nini kiliendelea. Kwani wakati ule huyp kijana alikuwa hajaja kwani alikuwa anamalizia masomo yake hivi. Pia ndani ya ile story walitaja mama wa watoto (alikuwa ameolewa na huyo mzungu huko kwao).
 
Masha hafai kuwa kiongozi kabisa, ni bora aendelee na shughuli zake tu, huyu anappata jeuri kwa hisani ya JK, JK analipa fadhira kwa hawa jamaa lakini inatosha sasa, masha sio kiongozi wa kuwa mfano wa kuigwa, kiongozi lazima awe na miiko na nidhamu, huyu malaya, mlevi, kila sehemu za starehe yupo na malaya wenzie....
tuwaombe wananchi wa jimbo lake wafanye uamuzi wa busara kutomrudisha bungeni tuone kama JK atamteua...
 
Hilo nimewahi kukutana nalo kwenye kama sikosei RAIA MWEMA. Na nafikiri Masha aliulizwa akakana kufanya ujanja na huyo mama. Since then sijui nini kiliendelea. Kwani wakati ule huyp kijana alikuwa hajaja kwani alikuwa anamalizia masomo yake hivi. Pia ndani ya ile story walitaja mama wa watoto (alikuwa ameolewa na huyo mzungu huko kwao).

huu ....sijui ni utapeli ,ufisadi au dhuluma kijana sasa yuko ndani ya nchi kitabu kamaliza na tetesi ni kwamba anataka kufungua kesi labda watampoza
 
Back
Top Bottom