Mheshimiwa Kikwete hivi wazo la Mabilioni liliishia wapi na tathmini yake ni vipi? Hebu chukua ushau

Kasimba G

JF-Expert Member
Jan 19, 2011
3,428
2,609
Wanajf,

Mheshimiwa Kikwete wakati anaingia madarakani, kulikuwa na mpango wa mabilioni ya Kikwete ambapo alielekeza the so called mabilioni kwa kuwakopesha wachuuzi! Hivi sijui tathmini yake ikoje au ndio ulikuwa mradi wa kuwanufaisha wachache? Kwani waliokopa waliisharudisha au ndio mkopo ukageuka msaada kwa walionacho?

Ningekuwa mimi ndio JK nisingeelekeza mkopo huo kwa wachuuzi, labda ningewapa baadae, ningewekeza kwa ku-create jobs, yaani ningejitahidi saana watu wengi wakimbilie vijijini through kilimo, ningetoa mikopo ya masharti nafuu kwa vijana wasomi ana wasio wasomi wakalime, nadhani wakiwa na incentives wangeenda tuu, yaani hapo ndio makosa viongozi wetu wanafanya, they are lucking charisma!

Kwa urban- lural kwa nchi kama yetu hii, inge-boost uchumi via production kubwa ya bidhaa za shambani, hebu fikiria kama wakati ule wa mabilioni yangekuwa yamefanyika haya, si ungekuta TZ inakuwa msambazaji mkubwa wa bidhaa za mashambani kwa ukanda wetu huu wa Africa mashariki na kati? Hata marufuku mnayopiga ya kuuza mazao nje isingekuwepo! Kwa sababu mtaji wa kilimo sio mkubwa na kama ni mazazao ya chakula muda wa kusubiri sio mwaka, maximum of five months!

Nadhani hata urudishaji wa mikopo ungekuwa rahisi kwa watu wenye uelewa! Kwakweli tunakosa ubunifu haswa kwa viongozi wan chi zetu hizi!

Nawasilisha.
 
Uliishia mifukoni mwa wajanja

Una habari kuwa Ridhiwani Kikwete ni moja kati ya mabilionea Tanzania?
 
aaaa wapi wakati anaingia ikulu alikuta hazina imejaaa kila kitu dolar pound tsh kibao akaanza kugawa yeye alijuwa zitakuja tu...duuu kumbeni kazi kujaza hazina sio sawa na kucheza ngoma
 
aaaa wapi wakati anaingia ikulu alikuta hazina imejaaa kila kitu dolar pound tsh kibao akaanza kugawa yeye alijuwa zitakuja tu...duuu kumbeni kazi kujaza hazina sio sawa na kucheza ngoma

Yaani utadhani kama mchezo wa kuigiza vile

Mabilioni yote aliyoacha Mkapa yameteketea hivi hivi tukiangalia kwa macho yetu
 
Back
Top Bottom