Elections 2010 Mheshimiwa John Pombe Magufuli awe Rais wetu

ninachosikitika ni ile hali ya watanzania ''kuamini kuwa'' JPM is working independently!yani watanzania seriously tunaamini JPM IS NOT ONE OF THEM!lol!

i am so so sorry for my country

Tanzania ya sasa ni kweli inao viongozi wazuri ambao hatuwajui kwa sababu hawajapata nafasi kuonekana. Tena basi, ni vigumu kuwaona viongozi wazuri kwa sababu sio wapayukaji ila ni watendaji wazuri. Ukibahatika kuona vitu vyao ndio unatambua. Si unajua debe tupu haliachi kutika?

Sio lazima atoke CCM, mimi sina chama tangu vyama vingi vilipoanza 1992, lakini hilo haliniweki pembeni kutafakari nani anafaa kuwa kiongozi wangu, kwani ni lazima atakuwapo kiongozi tu nitake nisitake. Kweli ubabaishaji wa viongozi wangu umenilazimisha nisuse hata shughuli za uchaguzi, kwa sababu dhahiri - anayemzidi mwenzie kwa ufisadi ndiye anachaguliwa kuwa kiongozi mara nyingi. Siku ikitokea JPM anagombea urais nakuhakikishia nitajiandikisha kupiga kura na kumpigia.

Leka
 
Pinda ni bora mara mia kuliko Pombe. Bahati mbaya sana Pombe tunafahamiana kiasi cha kutosha. Hatufai kwa ngazi ya Urais.
...Vyovyote iwavyo hawa jamaa wawili Pombe na Pinda kiukweli ni watu ambao kama watakuwa viranja wa kaya wanaweza ufanya mambo mazuri. So hata mimi nakubaliana na wazo la pombe kuwa rais na mizengo abaki hapo hapo alipo!!
 
Kama ni kutoka CCM, kwangu mimi anayefaa kuwa Rais baada ya uchaguzi ujao ni Pinda. Kama ni kutoka upande wa upinzani nchi tumpatie Dr. Slaa.
 
Mzee Yahya kishatabiri kuwa mtu atakayejaribu kuisimama na JK atakufa ghafla. Hivi unategemea wana CCM wanavyoamini matunguri kuna mtu atathubutu kusimama???
 
Mzee Yahya kishatabiri kuwa mtu atakayejaribu kuisimama na JK atakufa ghafla. Hivi unategemea wana CCM wanavyoamini matunguri kuna mtu atathubutu kusimama???

Kwa kweli hii imethibitisha kuwa Yahya ni mchawi na anaifanya CCM iamini uchawi zaidi kuliko vitendo halisia.
 
Mzee Yahya kishatabiri kuwa mtu atakayejaribu kusimama na JK atakufa ghafla. Hivi unategemea wana CCM wanavyoamini matunguri kuna mtu atathubutu kusimama???

Mkuu sijaelewa hapa just nieleweshe.
Atakaefariki ni ataempinga JK ndani ya CCM or hadi wagombea wa vyama vya upinzani wataosimama kuwania URAIS 2010??
 
Mkuu sijaelewa hapa just nieleweshe.
Atakaefariki ni ataempinga JK ndani ya CCM or hadi wagombea wa vyama vya upinzani wataosimama kuwania URAIS 2010??

Mkuu SiDe, Hii kali, ila ni swali la ukweli.
Je ni wote NDANI na NJE ya CCM kushnehi?
Watakufa vipi? Au watalogwa?

Anyway, ningependa wakati ujao Rais awe:
-Kama ni CCM, awe Dr. JOHN MAGUFULI,
-Kama ni Chama kingine, awe Dr. WILBROD SLAA.
 
hana lolote magufuli kashafulia ndio maana kapewa wizara ya mifugo na uvivu, alafu uliyeleta mada hii tunakujua mnatoka wote jimbo la chato!!
 
Kumbe mtunzi wa mapambio siku hizi wa kanisa gani kakobe au kwa lwakatare?

Pambio linaendelea (toka kwa Lwakatare music ministry)

Mwanzilishi: Neema neema neema imefunuliwa

Waitikiaji: Neema neema neema imefunuliwa


rudia hapo juu

x3

Mwanzilishi: Neema kwa vijana neema imefunuliwa

Waitikiaji: Neema neema neema imefunuliwa

Mwanzilishi: Neema kwa Tumaini neema imefunuliwa

Waitikiaji: Neema neema neema imefunuliwa

Rudia tena tokea juu
 
Khe khe khe makundi ya JF ni sawa na makundi yaliyo kwenye Chama Cha Majambazi.

Yaani hata haiwachukui muda kujianika (kwa vile walivyojaa ufisadi hadi akili zao zimedata) mbele ya kadamnasi ya JF wakiwa uchi.
 
Haijalishi kiongozi ajaye atakuwa nani au anatoka wapi; kama mfumo wa ufisadi utaendelea kusimama basi mazao yake yataendelea kuwa yale yale.
 
Usipendekeze majina ya kipumbavu. Amewakamata wavuvi haramu bandarini,ambao kesi yao inaigharimu Serikali pesa nyingi.Kwa sababu yeye anatimiza wajibu wake,na hao wengine watajijua wenyewe,kama angekuwa Presidential Material,angerudi nyuma hatua moja,kuamua tendo la kuwakamata wale wavuvi lingeweza kuleta athari gani kwa Nchi.
Na wakati ule alipowakamata,nilisema,just as a joke,kwamba atafute gharama ya wale samaki,awambie walipe,halafu waende zao. Nikitafakari yaaliyotokea baadaye,naona kwamba that was the best way.
 
Haijalishi kiongozi ajaye atakuwa nani au anatoka wapi; kama mfumo wa ufisadi utaendelea kusimama basi mazao yake yataendelea kuwa yale yale.

What is this? crap! au dalili za kukata tamaa kwakuwa yule mtu wako hawezi pita aagh!

Unafikiri mfumo unabadilishwa na mbu! lazima atokee mtu wa kubadilisha mfumo na lazima awe kiongozi kutoka mahali fulani inaweza ikawa upinzani au ccm

mandela hakusubiri boers wabadilishe system, walipambana kubadilisha system, of course magufuli ni kanyaboa!
 
Minister for Livestock Development and Fisheries Dr John Magufuli said the distribution was cleared after the fish was proved to be fit and safe for human consumption. The fish was examined by the Government Chief Chemist and at the ministry's laboratory at Nyegezi, Mwanza.

"Storage cost of the fish at Bahari Food Limited since March this year had risen to 1.2bn/-. We have already paid some of the money and we will complete the rest after the distribution," the minister said.

http://www.dailynews.co.tz/home/?n=6327
 
Halafu ilikuwepo incident,many months ago,maybe a few years ago,ambapo Polisi walisema wameamriwa wauondoe ulinzi wao nyumbani kwa Magufuli. Hizi habari ziliandikwa katika gazeti,kwamba,''kuanzia sasa Magufuli hatalindwana Polisi,kwa sababu Polisi wamekatazwa kumlinda.'' Sababu haikutolewa. Ina maana kwamba hata kama yupo mwandishi wa habari alikuwa anaifahamu sababu,labda alikuwa amezuiwa kuitaja.
Sijui ilikuwa ni sababu gani. Mimi sijui ilikuwa ni sababu gani. Labda hawa watu wanaotuambia kwamba Magufuli anafaa kuwa Rais,wanaweza kutueleza kwamba wanajua kwamba it is very scandalous kusema kwamba Polisi wamekatazwa kumlinda Waziri? And what was the problem? Can it be that he is not well liked in the Government?
 
Back
Top Bottom