<br />
<br />
Hatupaswi kuendelea kuweka makalio yetu chini na kuendelea kulalamika...Tumenung'unika sana,tumelalamika sana,sasa inatosha.Hatuna haja ya kuendelea tena kuumiza makoo yetu wala kuzidi kutia mikono mifukoni mwetu tukitafuta shilingi dhaifu (ambayo hata hivyo imekuwa adimu kwa wengi)ili eti tufanye jambo la mfano kwa watawala.Ni muda muafaka wa kutumia nguvu yetu ili kuleta mabadiliko chanya kwa ustawi wa taifa letu!
Mkuu nakuunga mkono na hili ndio tunapaswa tufanye mabadiliko sio kwa njia ya kupiga tuu kelele ambazo washirika wa upende wa pili hata haziwaumizi, wao wanaendeela kupokea ten percent zao na hali inaendelea kuwa ile ile naona sasa muda wa kufanya kile watawala hawataki umefika wa kutetea haki zetu na kupata kile ambacho tunakitaka kwa ajili ya kusaidia Tanzania ambayo inalemaa na kuendelea kudidimia