Gaijin
JF-Expert Member
- Aug 21, 2007
- 11,812
- 5,284
Si umeona hapo juu pendekezo langu Gaijin.., alafu nikianza kulipigia debe hili suala nani ataendelea kulima haya majaruba ya mpunga (unajua tena classification and division of labor) (wapo watu ambao hii ndio kazi yao na posho wanakula)
Ndio maana nikasema mimi nipo tayari kutoa mchango wa hali na mali na kuwaomba wananchi wenzangu tujaribu hata kuonyesha kwamba inawezekena..., unajua tena sisi wananchi tumeshatoa mchango wetu sana wa kodi zetu ingawa tunaowapa kodi hawawezi kazi hivyo basi inabidi tuwaonyeshe na jinsi ya kufanya kazi yao
Sheria ya Tanzania hairuhusu mtu mwengine yoyote kuuza umeme reja reja isipokuwa Tanesco. Kwa hiyo hata TANESCO ikipatiwa mafuta haitajalisha nani katoa kiasi gani, akiwasha umeme TANESCO itabidi usambazwe kwa wote na kama ukidumu kwa nusu saa tu kutokana na demand ya kukidhi eneo lote, tutashindwa kuwadhibiti.
Bado hatujafika hasa kwenye solutions mkuu, hebu tufikiri tena